Vita Kali: Samwel Sitta Vs Maaskofu

Vita Kali: Samwel Sitta Vs Maaskofu

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
* KWA NINI WATANZANIA TUMCHAGUE MGOMBEA URAIS ANAYETUKANA VIONGOZI WA DINI?

Kweli duniani kuna maajabu mengi. Na katika nyakati hizi maajabu yanazidi kuongezeka kila kukicha... Nani alitegemea yule mwanasiasa aliyediriki kuwatukana wachungaji leo hii awe na ujasiri, dhamira na ndoto ya kugombea urais..

Pamoja na kutaka kwake urais ni jambo la wazi Samwel Sitta amejiweka katika wakati mgumu pale alipozua mgogoro mpya dhidi ya viongozi wa dini ya kikristo. Hii ni baada ya kuita waraka walioutoa wakristo kuwa ni wa kijinga, kipuuzi na wa ovyo..

Kama tunavyojua ujumbe/waraka wa viongozi wa dini ni wa kinabii wenye maslahi mapana kwa wananchi ila ni Samwel Sita huyu huyu aliyeita waraka huo kuwa ni wa kipuuzi, kijinga na ovyo... Tafsiri yake ni kwamba viongozi wa dini saizi wamekuwa wa ovyo, wapuuzi na wajinga mpaka watoe waraka wa kipuuzi na ovyo, watanzania tusimame pamoja kukemea tafsiri hii ya Sita kwa viongozi wetu wa dini...

Kitendo hicho kiliwafadhaisha na kuwakasirisha maaskofu kitendo kilichopeleka maaskofu hoa kumfananisha Sita na Goliati wa kwenye Biblia aliyeshindwa na Daudi kwa sababu ya jeuri, kiburi na matusi kwa Mungu.

Naomba ikumbukwe kipindi cha bunge la katiba Sita alitoa maneno ya dharau, kejeli, matusi dhidi ya viongozi wa dini wa kikristo, hasa jukwaa la kikristo, kauli hiyo ya Sita mpaka sasa bado ni mwiba mkali kwake, kwani iliwauzi na umeendelea kuwauzi viongozi hao....

Askofu wa kanisa la KKKT Dayosisi ya Karangwe, Dk. Ben Bagonza alipata kunukuliwa akisema "Nimemsikia Sita akitushambulia wachungaji... Sasa natumia hekima kumjibu kwamba maandiko matakatifu katika Biblia; 1 Samwel 17:36~37 hasa mstari wa 36 unasema, Goliati alipogombana Daudi ushindi wake ulitokana na Goliati kumtukana Mungu...

Na ukiona Goliati anaanza kumtukana Mungu, ujue ushindi wa Daudi umekaribia. Hivyo ndivyo Sita sasa anatukebehi na kututukana viongozi wa dini. Hapo tunakumbushwa na maneno ya Mungu yanayosema "Awatukanaye nyinyi niliowatuma amenikataa mimi" Tazama Luka 10:16", Alisema Askofu Bongaza (Tanzania Daima)...

Askofu jimbo la Katoliki la Bunda Mhashama Renatus Nkwande alisema "Kwa kweli Mzee Sita ametutukana, ametafuta ubaya kwa viongozi wa dini kwa kuwa tumesema ukweli! Sisi tulikuwa tunatimiza wajibu wetu wa wakristo..... Tulizungumza kutokana na hitaji la wakati na ulikuwa waraka wa unabii" alisema

Askofu wa KKKT Dayosisi ya kaskazini, Dk. Steven alisikika akijibu mapigo ya Sita kwa kusema "Hatuwezi kujibizana na mtu kama Sita bali tutaanzia pale atakapoishia. Ukibishana na mjinga utakuwa mjinga pia. Tunasubiri amalize kazi ya kula fedha za wananchi sisi viongozi wa dini tuna watu wengi zaidi (Tanzania Daima)....

Huyu ndiyo Samwel Sita, ambaye leo hii ana mategemeo, ana ndoto na dhamira ya kuwa kiongozi mkuu wa Nchi hii ifikapo Oktoba...

Mzee wangu Sita, kama unadiriki kutukana viongozi wa dini, je leo hii utapata wapi ujasiri wa kuomba kura zao na waumini wao?

Mzee wangu Sita, kama unadiriki kutukana viongozi wa dini ni kundi lipi litasaidia kuliombea Taifa letu?

Mzee wangu Sita, leo hii jamii unataka ikuelewaje hasa kundi la wakristo wakati ulishatukana viongozi wao wa kiroho?
 
Samweli Sitta anapaswa awaheshimu viongozi wa dini. Anatakiwa ajue kuwa viongozi wa dini wana nguvu sana kwa maana ya ushawishi kwa waumini wao. Ambao kwa Sitta ni wapiga kura kwa upande wake.
 
Nilishawahi kusema, kwa sasa hakuna mwanasiasa mnafiki na mwenye chuki kama Sita..... Sita akiona madaraka mbele yake anaweza hata kumsaliti mke wake
 
Adhabu ya Goliati inamuhusu....yakukatwa kichwa ndege wa angani wajipatie chakula.
 
Mh Sitta matusi hayajengi hasa kuwatukana watumishi wa Mungu.Mbona unazo mbinu mbadala za kupata kura nyingi?Wasukuma na Wanyamwezi wakiamua wote kukupigia kura za uraisi utawashinda wenzako kwa mbali sana sababu ya wingi wao.Lakini unalikoroga unapotukana watumishi wa Mungu.Bado hujachelewa waombe msamaha.
 
6 ni uchafu kama uchafu mwingine hapa TZ, asingeweza kulazimisha kura eti kutengeneza katiba mpya ambayo haina ridhaa
 
Aliahidiwa kwamba kama akifanikisha hila za kupitisha katiba mpya basi atasimamishwa kuwa mgombea urais wa JMT kupitia CCM.

Akaona kwamba maaskofu hawana tena nafasi kwake, kwani alifikiri hizi ni zama zile za kuuziwa mbuzi kwenye gunia (read CCM wakishampendekeza mtu wao basi automatically watanzania watampatia kura)
 
Hili lizee ni linafiki hakuna mfano. Kuhusu heshima kwa wenzake hususan viongozi wa dini limeachwa mbali mno na EL. Labda hayo mengine tusiyoyajua ila linapokuja suala la unyenyekevu na heshima, EL kalizidi hili zee far x far. Sijawahi kuona mnyamwezi wa ajabu hivyo.
 
6 umefanya kosa kubwa sana hutapata uraisi kamwe.
 
Samuel 6x6, umefikia mwisho wa safari yako ya uongozi. usitegemee utapanda zaidi ya hapo. Vizuri kuwa umejiwekea historia, kama mtu aliyeharibu mchakato wa katiba Tanzania. Watakukumbuka kwenye historia miaka 50 ijayo.
 
Amejishushia heshima na hadhi aliyokuwa nayo kutokana na kuwakashifu viongozi wa dini.....
 
Hata penye ukweli mnaingiza mambo ya Team..... Sita hana adabu kwa viongozi wa dini

Sitta anaongea facts afu wewe unaleta opinion zako hapa ambazo ziko very biased! Acha kutumika na mafisadi wewe! Ukitaka nchi inyooke pigania yafuatayo...

Magufuli: Rais wa JMT
Sita: Waziri Mkuu
 
Back
Top Bottom