Vita dhidi ya umasikini, ujinga na maradhi vimekwisha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita dhidi ya umasikini, ujinga na maradhi vimekwisha?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwalimu Jr., Sep 4, 2008.

 1. m

  mwalimu Jr. Member

  #1
  Sep 4, 2008
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 51
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  BABA WA TAIFA alituambiaje mara baada ya kupata uhuru wa bendera?

  Mwalimu Mkuu alisema: 'Tuko katika vita. Vita dhidi ya ujinga, umasikini na maradhi.'

  Je ni wangapi wetu kweli wanajihesabu wako vitani. Kadri mtu anavyopanda ngazi kwenda juu anajihesabu tayari yeye hayuko kwenye vita hiyo!


  Vizito na Vigogo wananishangaa Tanzania iko kwenye vita kweli? Vita gani? Na nani? Toka lini?

  Waache wafanye mzaha. Mimi sitanii hapa. Ukweli ni kuwa vita hivi pengine havionekani, havisikiki, havizungumzwi tena maana wakubwa wameshashiba. Vita hivi kweli havina kwa muda huu tunaozungumza hakuna pande mbili au zaidi zinazopigana kwa silaha. Lakini majeshi yapo. Majeshi ya masikini dhidi ya wakubwa,matajiri na vibarakala wao yapo. Yapo, kama vile yametulia lakini yanaangalia na yanajiandaa tayari kwa mpambano. Mpambano huo utakuwa wa namna gani. Hatujui! Itakuwa kwa mgomo? Kuvunja ushirikiano na serikali na wanasiasa? Hatujui. Kwa maandamano [ingawa salama ziaidi polisi watawazuria], hujuma?
  Kuna watakaogura nchi kabisa [Zanzibar walishaanza]. Hatujui.

  Na ubinafsi, roho mbaya, chuki, choyo, tadi, inda, wivu na dhuluma [ za mmoja kwa mmoja au wachache kwa wengi] zikizidi vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa viwango mbalimbali inaweza kuanza. Hivi sasa tayari kuna watu wanawachukia wengine tu kwa sababu wana nyumba, wengine kwa sababu mwenzao kasomwa, mwingine kwa sababu mwenzao ana gari na kdhalika, na kadhalika. Na chuki hiyo ni zao la mfumo ambao haumpi imani labda mwalimu au daktari na wengineo kuona kama siku moja na wao wataukata. Milango yote ya kupanda yaelekea imefungwa lakini ya kushuka iko mingi mno.

  Vita vipo maana kile baba wa taifa alichotahadharisha miaka kadhaa iliyopita sasa kimegeuka ni ukweli wa maisha. Tofauti kati ya mtu wa chini Tanzania na mtumishi wa wizara tayari ni 1:50 je, kati, ya masikini huyo na matajiri au wakubwa wengine sio 1: 150 kweli? Hili linafanya vita dhidi ya umasikini iwe ni hadithi ya Alinacha na la kuchekesha zaidi ni kuwa wanaopewa dhamana ya kupiga vita hivyo badala ya kuondoa umasikini kwa wengi wanaamua kujitajirisha zaidi wao wenyewe!

  Ujinga sasa hivi ni 50:50 au nusu ya Watanzania ni wajinga. Hata mazuri aliyotuanzishia muasisi wa taifa hili tumeyazika bila huruma. Hivi tunashindwa kweli hapa tulipofika kuwa na mfumo wa elimu ya watu wazima unaofanya kazi badala yake tunawaachia vibwanyenye uchwara kuwanyang'anya masikini kile kidogo walichonacho pindi wanapotaka kuondokana na ujinga? Kwa msisimko wa 'privatization' !

  Hali ya watu wetu ni mbaya. Ugonjwa unaowasumbua sio ukimwi tu. Magonjwa mengine hata hayaeleweki wala kujulikana. Watoto, vijana kwa wazee hawana afueni katika nchi yao wenyewe. Wakati huo huo wakubwa lazima waende nje kwa tiba. Danganya toto ya watu wawili watatu wanaposaidiwa haitujengei moyo wa huruma wala heshimaya wagonjwa wengine.

  Kinachotakiwa ni sisi kuhakikisha hospitali zetu ni imara; zina vifaa vyote vinavyohitajika; madaktari na manesi wanalipwa vyema na sio kuwatoa wagonjwa upepo kila siku iendayo kwa Mungu. Maana ni vigumu kujua hapa kama ni daktari au nesi mwenye roho mbaya ndiye anayetakiwa kwenda motoni au SERIKALI isiyomjali na inayomlipa mshahara wa kutania wakati mashangingi yanakula mabilioni ya fedha za umma!

  Ninaamini kwamba ili tuwe vitani kikweli kweli lazima kila mtu kuanzia Rais mpaka tarishi awe na malengo YANAYIOELEWEKA, YANAYOWEZEKANA, YANAYOTATHMINIKA NA YANAYOMWAJIBISHA MTU.

  . Kila baada ya miezi sita au mwaka lazima tathmini ifanyike na anayeshindwa amuachie Mtanzania mwingine ajaribu.

  . Kila wizara iwe na VISHENI na MISHENI yake pamoja na malengo yanayostahili kufikiwa kila baada ya miezi sita au mwaka mmoja.

  . Iwe ni mwiko kuliachia tatizo kuwa tatizo pindi jambo linapoonekana tayari ni tatizo.

  . Utawala wa kisheria lazima uwe wa kikweli kweli na sio wa utani utani hivi.

  . Mikoa iwe huru kufanya maamuzi na utekelezaji wa masuala yao ya uchumi na jamii.

  . Wizara kadhaa ziondoke Dar es salaam na kwenda Dodoma na kwingineko mkoani ili fedha za serikali zifaidiwe na wakazi wa mikoa mingine.

  . Kama tunavyojenga Chuo Kikuu Dodoma pajengwe Ghorofa 30 au jengo lenye wingi 3 la ghorofa 10 na hela tunazoibiwa na NSSF au PPF ili serikali yote iwe kwenye eneo/jengo moja pale inaphitajika.

  . Hapa Dar es salaam serikali iondoke kabisa Magogoni na kuhamia Kibamba au Kiluvya. Majengo ya serikali yauzwe kwa bei nzuri itakayotosha kulipia gharama za majengo mapya bila naksi yoyote.

  . Tanzania ijiingize katika Utafiti unaozaa bidhaa au huduma bora na nafuu zaidi ikiwemo matumizi ya nishati mbadala.

  . Badala ya kuendelea kutapanya fedha kujenga shule mpya tuangalie kwanza kama shule moja iwe msingi au sekondari haiwezi kufanywa iwe yote mawili kwa maana ya kuongeza majengo au kuweka ratiba ambayo kwayo asubuhi msingi wanaosoma na mchana sekondari wanasoma papo hapo ili kupunguza hasara inayotokana na vyumba vya madrassa kutumika kwa masaa machache sana.
  . Makampuni ya migodi ilipe bei sawa na wenzetu wa Botswana wanayofaidi ili sehemu kubwa ya mzigo wa huduma za jamii ibebwe na kodi na mapato mengine toka makampuni ya migogi. Waliopo wakikataa tuwauzie Wachina, Warussia au Wakorea.

  . Tuwe na minada ya madini , mazao na vitu vingine papa hapa nchini ili tupunguze kuibiwa na kudhulumiwa kila siku.

  . Air Tanzania iachane na biashara ya abiria sasa kwa kununua ndege kubwa za mizigo kwa mizigo ya Watanzania, Wazambia, Wakongo, Warundi na Wanyarwanda.

  . Twendeni Marekani kusini pia tusiwe vipofu kwa sababu ya taa za New York na kwenda tu USAA!

  Na nina mengi mengine ila nawaachia wasiokuwa na ubunifu wala akili ya kuzua mambo mapya ili Tanzania na Watanzania wawe na hali bora ya maisha kuiba na kufanya haya niliyoandika hapa kwao bila shukrani. Panapo kyama kumbukeni nitawauliza je, mlinipa haki yangu kwa kutumia mawazo yangu??

  Maana jana nimemsikiwa waziri fulani anatepu moja kwa moja bila hata ya kusema jamani haya si yangu niliyadondoa kutokana na mpumbavu mmoja kwenye jamiiforums!

  Hawa wanaofanya hivyo wajue kwamba kuna wizi wa aina mbili kubwa. Wizi wa fedha/vitu na wizi wa mawazo.

  Watanzania na hasa viongozi wamekithiri kwa wizi wa mawazo ya watu wengine kisha kufanya ni mawazo yao orijinoo! Ile amri ya Usiibe- inasimama hapa pia na wote mnaofanya hivi mna dhambi tena pengine kubwa kuliko ile ya mafisadi!

  JUU YA YOTE hili la kutegemea misaada ili TUIKATE na kufadhili chama cha siasa au tumege tujineemeshe sisi wenyewe kwa majengo ya kifahari na magari ya anasa lazima liishe. Madini na mali asili nyingine zetu zina uwezo kabisa wa kutupa patp la kutosha ili mradi tu tusiwe tumepokea teni paseni na kukubali asilimia 3 badala ya 20 ya mrahaba.. Hivi kuna mashine au mitambo ambayo kweli ina thamni kuliko Watananzania na mali asili yao?
   
 2. Yohana Kilimba

  Yohana Kilimba JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2015
  Joined: Dec 25, 2012
  Messages: 8,132
  Likes Received: 5,211
  Trophy Points: 280
  long time,umenena kiongozi
   
Loading...