Vita dhidi ya ufisadi na maovu mengine katika jamii tutashinda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita dhidi ya ufisadi na maovu mengine katika jamii tutashinda?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tikerra, Feb 21, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hii hoja labda itawashtua na kudhani kwamba labda nina kata tamaa.Lahasha,niko ngangari,na wala sitapumzika mpaka nihakikishe kwamba ufisadi na maovu mengine katika jamii yetu yamefikia managable levels.Tukubaliane kwamba hatuwezi kuyamaliza,ila tunaweza kuyapunguza.

  Sasa kwa nini nina wasiwasi na ushindi wetu katika vita hii?Ni kwa sababu wengi tunapigana vita hii bila silaha za kutosha.Niwakumbushe tu kwamba vita hii ni vita ya kiroho zaidi kuliko hata kimwili,ingawa ina elements fulani za kimwili..Sasa kwa bahati mbaya wengi hatulitambui hili,na sidhani kama tunaweza hata kuli appreciate.Kwa kurahisisha mambo ni kwamba ni vita ya good against evil,that is God against Satan.

  Wengi hatujui kwamba watumishi wa shetani wapo miongoni mwetu,na their zeal to destroy is unprecedented.Watu hawa wanafanya kazi kama mchwa katika harakati zao za kuwapotosha wanadamu na wamewezeshwa kwa kiwango cha kutisha sana katika kila hali,kifedha nk.nk.Kwa bahati mbaya sana wengi wetu ni maskini, kwa maana kwamba ukilinganisha na watumishi wa shetani, we are nothing! Kwa hiyo vita hii ni kama vita ya Daudi ambaye baadaye alikuwa mfame wa Waisraeli, dhidi ya Goliati!Ni vita kali sana.
  Kwa bahati mbaya wengi hatujui hata silaha anazotumia adui,kwa hiyo ni rahisi sana kutushinda.Kila mtu anakumbuka kwamba Daudi alishinda vita ile kwa vile alimtegemea Mungu.Na sisi ni lazima tumtegemee Mungu kuliko akili zetu,vinginevyo hakuna ushindi.

  Wote tunaona jinsi nchi yetu inavyo zidi kuchafuka,kila kukicha kuna kashfa mpya.Wote tulio wategemea sasa wako kwenye payroll ya shetani,wametugeuka kabisa.Tusijidanganye,kwa jinsi hali ilivyo,msaada wetu uko kwa Mungu peke yake,na kama hatuku mgeukia kwa msaada, tutaharibiwa na kuangamizwa kabisa.Dalili zote zinaonyesha mwisho huo mbaya.Sasa ni wakati wa kuamua kama tunakaa upande wa Mungu au wa Shetani,there is no midpoint.
   
 2. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Tikerra,
  Ukifikiria serikali ilivyotumia kodi zetu kuwatengenezea majambazi makao Keko yanayofanana na majumbani kwao, ukajumlisha na sababu zinazoifanya serikali kushindwa kuwakamata kagoda na kina Maregesi hadi leo, hutakuwa na shaka tena kuwa serikali haina dhamira ya kupambana na ufisadi na zaidi utapata picha kwamba serikali yenyewe inahusika na ufisadi.

  Lakini nikikumbuka Mramba na Yona walivyo koswakoswa kwa kuokolewa na polisi pale Kisutu baada ya wananchi wenye hasira kutaka kuwafaniya kweli, napata faraja. Serikali inafanya masihara bila kujua kuwa wananchi wa leo si wale wa jana, kama alivyosema Mwakyembe. Ni vema serikali ikajua kuwa kamwe haiwezi kuishinda nguvu ya umma na tutashinda kwani kama ulivyoandika hapo juu, Shetani hawezi kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu!
   
Loading...