mikedean
JF-Expert Member
- Mar 15, 2018
- 3,255
- 4,599
Ni suala la uzalendo na zuri kutangaza nchi ya Tanzania nje ya Tanzania. Timu ya Simba inapaswa kupewa heko kwa Hilo.
Simba itapata kutembelea nchi za Sudan, Misri na Kongo. Nchi hizi za kiafrika Zina ukaribu mkubwa na Tanzania isipokuwa Sudan. Hivyo wasudan watakumbuka kuwa Kuna nchi inaitwa Tanzania.
Jambo linalonitatiza ni kuingiza dili hilo bure kabisa. Hii sio nzuri, Simba ilipaswa kupata chochote. Angalau kingesaidia kuwapa motisha wachezaji Kama hela isingetumiwa na Simba SC. Kama ni uzalendo basi wangepunguza walau hata mil 200.ili iwasaidie hata kwa kulipia hotel.
Kwa sababu klabu ya Simba ni mali ya Mo Dewji Ndio maana sio ajabu wanafanya haya. Ni kama Man City ya Sheikh Mansoor
Sidhani kama Man City kuingiza dili na Etihad inamaana Mansoor sio mzalendo Bali Ile ni biashara.Tunaposema mpira ni biashara,hii ilikuwa fursa ya kupata kuingiza mapato.
Mwenyekiti wa Simba ajaye anapaswa asiwe mtu wa kuburuzwa. Anapaswa awe ndiye msimamizi wa madili kama haya Ili Simba ya wanachama iwe na chochote.Yamkini Mo akawa Hana shida na hela hizo, ila Simba ya wanachama ambayo inasemekana Ina hisa 51% ambayo kwa Hakika ni asilimia hewa. Hizi Ndio pesa ambazo Simba ilipaswa kuwa nazo.
Leo Barbra ameingia huo mkataba kwa BARAKA za kaimu mwenyekiti au kwa BARAKA za Mwenyekiti wa Bodi? Narudia tena hili dili Halina maslahi kwa Simba. Ilipaswa mwenye hisa 51% Ndio awe na sauti. Sasa swali ni kuwa Barbra yuko kwa maslahi ya Simba ya Mo au Simba SC?
Sijaandika kwa nia mbaya au kuwa Simba wamekosea Ila nahisi serikali ilipaswa ichangie.simba inatumia uwanja wa taifa mechi moja ni Mil.4 na unatoa kabla ya mechi.Basi Simba nao wangepewa kutumia uwanja huu bure kwa mechi za nyumbani za CAF champions ligi Kama fadhila.
Kuchangiwa kwa hoja karibu