Habari wakuu,
Kuna kitu nimewaza na haya ni mawazo huru. Maisha kwasasa yamekuwa ghali sana, na piah utandawazi umebadilisha mitazamo mingi sana.
Tujikite hapa, kuhusu mahusiano imekuwa kawaida sana kusikia lawama za mahusiano kwa Sasa na wengi wanaoanzisha nyuzi humu ndani shutuma nyingi wanaziendekeza kwa hao wenzi wao kila anaeleta malalamiko humu ndani yeye ni mambo safi mwenzie ndo ana matatizo.
Kama vijana hasa wa kiume jaribu kuyawaza haya.
1. Maisha yamebadirika hakuna apendae maisha magumu.
Huu ni ukweli uliowazi maisha kwa Sasa ni tofauti na Karne, tujifunze kuishi kulingana na maisha yalivyo. Kiasili mwanaume ameumbwa kutafuta kwa nguvu na mwisho anaekula matunda ni mwanamke (mama au mpenzi).
Unakuta kijana upo Hauna uhakika wa kuishi, kazi ni shida, upatikanaji wa pesa ni WA shida na wakusuasua, kujituma wajituma lakini Bado Hali haijakaa sawa, ukimiliki mwanamke mzuri atahitaji gharama na matunzo azidi kuimarika na uzuri wake usipotee, kumiliki mwanamke mzuri na kuhakikisha anabakia kwenye fomu yake yakuhitaji gharama yanini kumiliki gari ambalo huna uwezo wa kulitunza?! Na ukiwa na mwanamke mbovu ni hasara kwa matamanio yako ya mwili, lakini ukiwa na mwanamke mbovu "kiakili" ni hasara kwa maisha yako yote?
2. Wanaume wengi hatuna hisia na watu wetu sababu kuu ni utafutaji na mazoea. Mtu uko na mwanamke utafutaji wako ni WA patupapatu, muda wote wawaza kazi, hisia na mwenzio hakuna, watoka kazini muda umeenda wataka kumpanda tu na sababu ya uchovu huwezi mudu tendo vizuri, ubora wako unapotea, anabakia na mawazo tu yasio yakujenga akishikwa akili na marafiki plus hiyo namba Moja hapo juu, lazima kichwa kiwake moto.
3. Umalaya.
Hili linaeleweka vyema, wanaume tuliowengi tuna matamanio ya juu sana. Wakuta mwanaume Yuko katika mahusiano heshima kwa mtu wake haipo, mdada wa watu kila mara akuvumilia kwa mengi, apambania penzi lake lisiingie kinyamkera, akikufuma na messages au viashiria na wanawake wengine unatumia uanaume tu "mwanaume akosei", okay plus namba pili plus namba Moja hapo juu?
4. USAFI.
Piga hesabu sisi wanaume tukidate na mwanamke mchafu maneno humu ndani ni mengi sana, kashfa ni nyingi, upande wa pili?!, Mwanaume kazikazi unarudi kwapa Liko hoi unakula wataka ule tena full uchafu kuoga ni kazi, mwili watoa harufu usafi tu waboxer ni kazi, boxer ukiirusha haidondoki inasimama, viatu vinanuka, mdomo, kumuandaa mwenzio ni shida ushamgeuza kuku, ongezea na hayo ya hapo juu?!!
5. Sifa za kipuuzi.
Mwanamke mbinafsi ni hatari kwa ndugu wa mume, lakini ukikutana na mwanamke anaejali na anahako kaubinafsi lazima mfike mbali kimaisha. Wanaume wengi ni wabinafsi, wengi hawahudumii kwa moyo, ugomvi kidogo utasikia "mimi nakulisha nakuvisha nimekununulia simu..." Mzee huo ni wajibu, na kwanini umhesabie wema wako, kwanini usifanye kwa moyo.
Kwani kumhudumia ni tiketi ya kumfanya utakavyo?! Kumsomesha ni tiketi?! Na kwanini umsomeshe wakati hujasoma kufika level hizo?! Na piah kumsomesha kwann iwe ni tiketi ya kuoa?! Bado waeza msomesha na usiwe na malengo yoyote nae (wenye hela ndo wanafanya hivi) wewe huna kitu unahudimia kwa kuhesabu (ubinafsi) mwisho unasahau wajibu plus ya hapo juu
Mwisho.
Mahusiano mengi, causes zinafanywa na wanaume kwa kutokujua kwa sababu ya matumizi mfu ya 'uanaume', na effect zinatolewa na wanawake na mwishoni kuonekana kuwa wanawake wanamatatizo.
Jitahidi kujikubali kama mwanaume kwa kile ulichojaaliwa na jipe muda, epuka kumiliki kitu ambacho huna uwezo wa kukimudu muda mrefu, ingia katika mahusiano ukiwa na utayari. Kuingia kwenye mahusiano muda mfupi unatanga ndoa ni kama kubashiri tu matikiti uloyaona muda mfupi na kuamua kuchukua yaweza tokea bahati ukabahatisha. Jitahidi kuishi mwanaume hakuna aliye mkamilifu.
TUMIA MUDA MWINGI KUTAFUTA MWANAMKE KABLA YA KUINGIA KWENYE MAHUSIANO NA USIDATE NA MALAYA, wanawake wengi ambao hawayaelewi mahusiano yao"wako single"