Virusi za kompyuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Virusi za kompyuta

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MziziMkavu, Nov 23, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Virusi za Kompyuta ni programu haramu yenye uwezo wa kujisambaa ndani ya kompyuta na kujiingiza ndani ya programu halali zinazotakiwa kufanya kazi mle. Ikisambaa inaathiri programu halali na kusababisha hasara. Virusi

  zinasambaa kwa njia ya intaneti lakini pia kwa njia ya sidii au diski yoyote ya kubebea data kati ya kompyuta. Virusi vinaweza kuharibu mafaili na kupunguza uwezo wa ufanyaji kazi wa kompyuta yako.

  Historia Programu za virusi zilianzishwa tangu vyanzo vya kompyuta vyenyewe. Wanahisabati maarufu kama John von Neumann walikadiria nadharia ya programu zenye uwezo wa kujiendeleza na hata kujisambaa peke zao tangi miaka ya 1950. Tangu kupatikana kwa kompyuta ndogo za nyumbani imeonekana ya kwamba programu za aina

  hii zinaweza kuleta hasara mbalimbali. Mara nyingi programu (c)Brain hutajwa kama virusi ya kwanza iliyosambaa kwenye kompyuta ndogo tangu mwaka 1986. Usambazaji wake ulikuwa kosa la watungaji wake waliotaka kukinga diski za programu halali waliyouza dhidi ya kopi haramu; waliandika namba ya simu yao ndani ya virus.

  Tangu kupatikana kwa intaneti kuna watu maelfu ambao wametunga programu za virusi kwa kusudi mbalimbali; mara nyingi ni vijana wanaotaka kujaribu uwezo wao wa kuandika programu za aina hii. Wengine wanakusudia mzaha tu wakitaka kuona mafanikio yao kwenye kompyuta za dunia yote. Kuna wengine wenye hasira dhidi ya

  kampuni kubwa kamaMicrosoft, dhidi ya benki, dhidi ya serikali au dhidi ya binadamu kwa jumla. Hao ni hatari zaidi wakijitahidi kusababisha hasara kubwa. Wengine hufuata kusudi za kisiasa wakilenga kwa kompyuta za lugha au

  nchi fulani hasa. Virusi nyingi zina malengo ya kijinai kwa sababu watungaji wao wanajaribu kupata faida ya kifedha kwa njia ya utapeli wakijaribu kuiba maneno ya siri kutoka kompyuta ya watu yanayomruhusu mtumiaji kuwasiliana na benki na kutuma fedha kwa akaunti yningine.


  Hatari za kutumia makompyuta mengi-mengi Mtandao wa intaneti unaruhusu mamilioni ya watumiaji wa kompyuta duniani kuungana pamoja kibiashara na hata kwa kujifurahisha. Watu wengi tofauti hutumia intaneti. Yeyote anayetumia Intaneti anaweza kupata habari nyingi kuhusu mada tofauti, tena kwa lugha tofauti, yaani, katika kipindi kidogo sana.

  Intaneti inawezesha mtu mmoja kuharibu au kupunguza uwezo wa mamilioni ya kompyuta ambazo zimeunganishwa nazo. Wanaweza kufanya hivi kwa kuandika program za kompyuta. Au, wanaweza kuzifanya kompyuta zijiweke taarifa za kipuuzi ambazo zinasabisha kompyuta iache kufanya kazi. Iwapo sio mwangalifu, basi unaweza kusababisha kompyuta iache kufanya kazi.

  Hasara kubwa zilizosababishwa na "worm"Mnamo tar. 24 Januari, 2003, aina ya kirusi cha kompyuta kiitwacho "worm" kilitolewa ili kuathiri Intaneti. Worm ni mfululizo wa maelekezo ya kompyuta ambayo yanajiweka nakala nyingi-nyingi yenyewe na kuzituma kwa kompyuta nyingine.

  Huyu worm ametuma nakala kibao zake mwenyewe kwenye kompyuta nyingine kupitia Intaneti. Huyo worm ameharibu mamilioni kadhaa ya kompyuta duniani. Imepunguza uwezo wa makompyuta kibao kupitia mitandao ya kompyuta.

  Kampuni za kupiga vita virusi Sophos P-L-C ni kampuni ya kompyuta ya huko Britania ambayo inatengeneza program za kuilinda kompyuta dhidi ya virusi. Hii ni kampuni ya nne kwa ukubwa ya kutengeneza program za kuzuia virusi.

  Hivi karibuni, kampuni ya Sophos imetangaza onyo rasmi watumiaji wa kimpyuta kujikinga dhidi virusi vipya vingi na worms. Tangaza lilitoa maelezo juu ya baadhi ya watu wanaofanya kazi kwa juhudi kutengeneza bidhaa pepe haramu za kompyuta. Kampuni ya Sophos ilisema ya kwamba hizi ni ripoti kutoka katika gazeti lililochapishwa

  nchini Singapore mnamo tar. 14 Januari, siku tu kable ya shambulio la worm lililofanywa katika Slammer.
  Graham Cluley ni mtalaamu wa kompyuta katika kampuni ya Sophos. Alisema kwamba kampuni za utengenezaji wa programu za kulinda kmpyuta zinategemea virusi vingi kwa mwaka huu. Alisema watunzi wa virusi wanataka

  kubuni virusi vingine vyenye nguvu kupita hata hivi vya worm. Hii itaweza kusambazwa kupitia ujumbe elektronikia au njia ya mawasiliano ya kompyuta iitwayo Instant Messaging (Ujumbe wa Haraka kama vile Yahoo Messenger, Google Talk, Windows Live Messenger, na kadhalika). Bwana Cluley aliendelea kusema kwamba aina hii ya virusi husababisha matatizo makubwa sana.

  Wataalamu wa kompyuta wa Kampuni ya Sophos walisema kuna virusi vya kompyuta takriban 40,000 ambavyo kwa sasa vinafahamika kama vipo. Wataalamu hao waliendelea kusema kwamba takriban virusi vipya 200

  hutolewa kila mwezi kupitia Internet.
  Bwana Cluley alisema miaka kumi au tisa iliyopita kompyuta nyingi zilizoharibiwa na virusi ni zile ambazo zinatumia Microsoft Windows kama ndiyo mfumo wake wa uendeshaji, yaani, operating system.

  [​IMG]
   
 2. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  sasa itakuwaje mkuu?
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Tujikinge na hizo virus za Computer kwa kutumia Antivirus zilizo nzuri .
   
 4. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu umeniogopesha kwa hili somo lako murua. Swala la kujikinga ni gumu sana, maana antivirus siku hizi ni nyingi sana,
  hata kutambua ipi ni bora zaidi inakuwa shida. Kikubwa zaidi ni huo mzigo wa 200 monthly! Hapa kiukweli kazi ipo.
   
 5. m

  mzee wandimu JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 441
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  mkuu mzizimkavu(kamasijalikosea jina) asante kwa mada nzuri! nadhani virus kuisha itakuwa ngumu make imekaa kibiashara zaidi kwawanao tengeneza hao virus na wanaotengeneza ant virus!

  off topiki!
  hivi mkuu kuna programmers wowote wa tanzania walioweza kutengeneza program hizi?
   
 6. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,273
  Trophy Points: 280
  Hapo ni kati ya mchawi na mganga!!Na mara nyingi wanaotengeneza Virus ni hayo makampuni yanayotengeneza anti virus!1kwakuwa kwa wenzetu sheria imeshika atamu watengenezaji wa virus wanatengeneza kwa uficho mkubwa hivyo ikigundulika nikampuni fulani hiyo fain yake nikubwa na kampuni kufirisika hivyo mara nyingi wao ndo wazalishaji!1Na pili hata serikali za wenzetu matharani USA wao kwa vitengo vya intelejensi utumia virus vingini kwa ajili ya kupata data kwenye komputa za watu walio wakusudia mfano shirika fulani linatumia net yao hivyo wanaweza kusambaza virus ikakolekiti data wakapata walichokuwa wakikitaka!!
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hii ndio maana hua sifungui link zisizoeleweka hata kama zimetumwa kwa email nnayoifahamu.
  Miaka kadhaa nyuma nilifungua link kwenye MSN Messenger laptop yangu ikachukua likizo ya ugonjwa kwa miezi.

  Kama kitu hukielewi elewi usifungue.
  Asante MM kwa kutukumbusha.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Kanuni bora za usalama wa kompyuta

  [HR][/HR]

  [​IMG]Ingawa mara nyingi tumekuwa tukisikia hakuna usalama wa asilimia miamoja kwenye ulimwengu wa kompyuta,ila kinga ni bora kuliko tiba.
  Hebu angalia,wengi wetu tumeweka nondo za kutosha majumbani mwetu huku tukiwa na lundo la mbwa wakali. Ingawa vyote hivi sio kama vitawazuia majambazi kukuingilia,ila inaweza kusaidia kuzuia vibaka wadogowadogo.
  Kwa mantiki hayo,leo hii tutaangalia njia bora za kujikinga na kujiweka katika mazingira ya usalama.Binafsi nimeshasahau mara ya mwisho ni lini kuvamiwa na virusi au minyoo,sio kwakuwa natumia programu za ulinzi zenye nguuvu saaana au ni bingwa sana kwenye masuala ya kompyuta hadi virusi vinaniogopa,bali ninafuata kanuni bora za usalama wa kompyuta ambazo leo hii nitagawana nanyi. Hivyo bila kupoteza muda hebu tuziangalie kwa mapana yake.
  I.Tumia programu unazozihitaji

  Wengi tumekuwa wahanga wa matatizo ya kompyuta kwa kujisababishia wenyewe,inawezekana kwa kujua au bila kufahamu.
  Kompyuta nyingi zimekuwa zikiathiria na masuala ya kiusalama sio kutoka nje bali ndani ya kompyuta husika. Matatizo haya mengi husababishwa na programu ambazo hazijaandikwa kiusahihi.Chukulia mfano jinsi ukuta wa nyumba unavyoweza kukuangukia na kuvunja vifaa vyako vya ndani au bati ambalo halijagongelewa ipasavyo na kuacha tundu kwenye njia ya msumari na kupitisha maji pindi mvua inaponyesha. Hii ni sawa na hizi programu,kama programu haijaandikwa ipasavyo inaweza kukusababishia matatizo mengi.Sio tu kuhitilafiana na mtambo endeshi(OS) wa kompyuta yako na wewe kuona kama kirusi bali pia inaweza kuacha mianya ambayo wavamizi wanaweza kutumia kuingia kwenye kompyuta yako.
  Mazingatio.
  • 1.Ondoa programu ambazo hauzitumii ili kupunguza uwezekano wa matatizo,wengi wetu tumekuwa na mazoea ya kusimika programu nyingi wakati nyingi kati ya hizo huwa hatuzitumii kabisa,hizi programu hujaza nasafi,kuweka uchafu na hatimaye kutuweka hatiani.
  • 2.Hakikisha unatumia programu zilizo kwenye wakati,simika maboresho(update) pindi yanapotokea.Nimeshuhudia watu wengi wamekuwa wagumu kusimika haya matoleo mapya kutokana na hofu mbalimbali.Achana na hofu.Maboresho yanakuja kwa ajili ya mambo mema na si kukudhuru.
  II.Tumia programu za uhakika

  [​IMG]Je umewahi kujiuliza kwanini natumia programu hii badala ya ile? Ukuaji wa teknolojia umesababisha kila mtu kuja na programu yake,kuna zile za bire,za kugawana na hata zile za bei chee.Sasa sitaki kusema kuwa programu za bei ya juu ndio bora au zile za bei ya chini ni za kukimbiwa kama ukoma,ila wewe kama mtumiaji unatakiwa kufanya kautafiti kadogo kabla ya kuamua kutumia programu fulani. Siku hizi kuna google ambayo inaweza kukusaidia kwa kiasi kikubwa kufanya utafiti na kuangalia maoni ya watumiaji juu ya programu husika.
  Kwa kufanya hivi itakusaidia unapata programu ambayo inakidhi mahitaji yako huku ukiwa salama.Mfano mzuri binafsi sijawahi kutumia Windows Vista,kwani kipindi natumia Windows XP na kutaka kuhamia kwenye mtambo mwingine nilifanya tafiti na kuona watumiaji wengi wakilalamikia windows Vista hivyo niliamua kuachana nayo,habari njema ikaja na Microsoft wakaamua kuiondoa sokoni na ku;eta Windows 7 ambayo ni kipenzi cha wengi.Hivyo TAFITI TAFITI TAFITI.
  III.Hakikisha unajua nini unachokifanya

  Wengi wetu tumekuwa wahanga kutokana na kukubali kiholela au kufanya mambo tusiyoyajua.Labda nikupe mfano mmoja wa mtu wangu wa karibu ambaye aliwahi kuvamiwa na na hizi programu za matangazo(Adware).Yeye alikuwa alifungua tovuti moja mara akaona ujumbe unasema kompyuta yako ipo hatarini hivyo bonyeza hapa ili kutatua.Bila kujua anachokifanya akabofya na kujikuta ameshaingiza madudu kibao.
  Hivyo kuwa makini kila unapokubali ujumbe wowote.Hakikisha unajua unachokifanya.
  Hayo ni mabo machache ambayo unatakiwa kuzingatia ili kuhakikisha unakuwa katika mazingira salama na yenye kinga bora.
  Source: Kanuni bora za usalama wa kompyuta – AfroIT Blog-Wazee wa mididi!
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Jihadhari na Programu hizi FEKI za kuzuia Virusi vya Kompyuta
  [​IMG]  Ili kuzilinda kompyuta zetu na virusi, wengi wetu huwa tunakimbilia programu za bure ambazo zinapatikana kirahisi kwenye internet. Kitu ambacho Nifahamishe tungependa ufahamu ni kwamba kuna programu FEKI za antivirus ambazo zitaharibu kompyuta yako iwapo utaziinstal. Kwanza kabla hatujaanza kuzungumzia programu hizo ni bora kwanza tukajua virusi ni nini kwa faida ya wale ambao neno hili huwa linawakanganya.

  Virusi ni programu ambazo watu wenye nia mbaya huzitengeneza kwa nia ya kuharibu kompyuta za watu wengine.

  Kompyuta yenye virusi huwa inachelewa kuwaka, inapowaka huwa inafanya kazi taratibu sana na mara nyingine hujizima na kujiwasha yenyewe bila wewe kufanya chochote.

  Kompyuta yenye virusi pia huwa mara nyingine inajizima kabisa na hata ukibonyeza kitufe cha kuwashia huwa haiwaki tena.

  Mara nyingine kompyuta yenye virusi huwa inatengeneza mafaili ya ajabu ajabu bila wewe kujua. Na mafaili hayo huifanya kompyuta yako ionekane kama vile hard disk yake imejaa wakati hujaweka chochote cha maana.

  Wakati kompyuta zetu tunapozihisi zina virusi kwa kuonyesha dalili kama hizo tulizozitaja hapo juu, wengi wetu tuna tabia ya kusachi kwenye google au yahoo na kutafuta programu ya antivirus ili kuziokoa kompyuta zetu.

  Kitendo hicho ni cha hatari kwakuwa bila kujua tunaweza tukadownload programu ambazo sisi tutadhani kuwa ni za kuondoa na kuzuia virusi kumbe hali halisi ni kinyume chake.

  Baadhi ya programu hizo ambazo ni feki badala ya kuzuia virusi hutuingizia virusi kwenye kompyuta zetu na hivyo kuziweka kompyuta zetu kwenye hatari.

  Baadhi ya programu hizo feki ambazo zinajulikana sana kuwa ni feki lakini mamilioni ya watu duniani wamekuwa wakiendelea kuzidownload ni hizi:

  PersonalAntiSpy, VirusGuardPlus, VirtualPCGuard, AntiMalware 2009, AntivirusProtection, Security Scanner 2008, VirusResponse Lab 2009, Antivirus Lab 2009, Antivirus Security, Micro Antivirus 2009, AntiSpyware Pro XP na XP Protector 2009.

  Zingine ni VirusHeat,VirusIsolator, Virus Locker, VirusProtectPro, VirusRemover2008, VirusRemover2009, VirusMelt, VirusRanger, Virus Response Lab 2009, VirusTrigger, Vista Antivirus 2008.

  Kama unatumia mojawapo ya programu hizo basi ujue badala ya kuzuia virusi visiingie kwenye kompyuta yako, programu hizo zitakuwa zinavialika kwa wingi virusi ili viharibu kompyuta yako.

  Ufumbuzi wa tatizo hilo ni kwa wewe kuinstall programu zinazojulikana ambazo zitasafisha na kuzuia virusi vyote ambavyo vingeharibu kompyuta yako.

  Zifuatazo ni programu za uhakika ambazo unaweza ukainstall mojawapo na zitaifanya kompyuta yako iwe salama ziku zote.

  Kaspersky -- Trial Versions

  Trend Micro -- Antivirus | Anti-Spam | Anti-Spyware: Product Overview - Trend Micro Europe, Middle East and Africa

  Symantec -- Download Norton Internet Security, AntiVirus, or Norton 360

  Panda -- Download Antivirus Panda Security for free | Try Antivirus - Panda Security

  Avast -- avast! Free Antivirus - Download Software for Virus Protection

  Antivir -- Avira Free Antivirus - Download Best Antivirus Software
   
 10. IHOLOMELA

  IHOLOMELA JF-Expert Member

  #10
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 837
  Likes Received: 366
  Trophy Points: 80
  asanteni kwa kututoa tongotongo. Mie hupata email za ajabu ajabu toka kwa watu ninao email nao nikichek naona kuna link flan but huwa na ignore tu..nikimuuliza mtumaji ni kitu gan ktk hyo link jamaa anasema hajatuma wala hajui chochote kuhusiana na email hyo. Je nayo ni virus?
   
Loading...