Nichumu Nibebike
JF-Expert Member
- Aug 28, 2016
- 8,658
- 15,814
Tangu nimekuwa mdogo, tukienda dukani tuasema, nipimie mafuta kibaba kimoja.
Leo nina hamu ya kujua hichi kipimo cha kibaba kilitoka wapi na ili upate lita moja, unahitaji kuwa na vibaba vingapi?
Nadhani waliowahi kuuza duka watakuwa na majibu zaidi juu ya hili...
Tangu nimekuwa mdogo, tukienda dukani tuasema, nipimie mafuta kibaba kimoja.
Leo nina hamu ya kujua hichi kipimo cha kibaba kilitoka wapi na ili upate lita moja, unahitaji kuwa na vibaba vingapi?
Nadhani waliowahi kuuza duka watakuwa na majibu zaidi juu ya hili...
Hapana Mkuu,Kibaba kilitumika kupimia Mafuta ya kula na mafuta ya taa enzi hizo,Kibaba hakikutumika kupima vitu kama mafuta ya taa au ya kupikia. Kipimo ninachokumbuka mimi ni kikoroboi (kule kijijini kwetu). Naweza kuwa nimesahahu jina lake.
Kibaba kilikuwa kinatumika kupimia vitu kama mchele, maharage, ufuta, n.k. Vibaba vinne ni pishi moja. Kwa wakti ule pishi kama 30 hivi zilikuwa zinajaza gunia moja (gunia la jute).
Mambo hayo ya Vipimo vipimo cha vibaba, Mizani, na yale makopo yenye vipimo yana asili ya India, Wahindi ndio khasa waanzilishi na kisha vikaingia Uarabuni na kisha kuingia huku kwetu
Sina uhakika kama kile kinachopimia mafuta ya kula ni Kibaba, bali kibaba ni kopo kubwa zaidi
Asili yake siyo India. Hizo ni "Imperial measurements" zilitokea Uingereza. Mpaka leo Canada bado wanatumia kwenye uuzaji wa nafaka.
Kwa hapo juu kibaba ni hicho cha pili kwa ukubwa. Cha tatu kwa ukubwa ni pishi ambayo inachukua vibaba vinne. Kikubwa zaidi nadhani havikutumika Tanzania kinaitwa bushel kwa kizungu. Mpaka leo Canada wakitangaza bei za nafaka wanasema bushel moja ni dola ngapi.
Hapana Mkuu,Kibaba kilitumika kupimia Mafuta ya kula na mafuta ya taa enzi hizo,
Hiki Kibaba kilikua ni kifaa kilichotengenezwa kwa material ya "steel" kilikua na mkono mrefu wa kushikia,
Kilitengenezwa kua na mkono mrefu wa kushikia kwa makusudi kabisa ili kiwe na uwezo wa kuchota mafuta hata kama yapo chini kabisa ya Debe, Kibaba kimoja kwa mtazamo wangu kinaweza kufikia Appx 35-40 Ml
Pia kuna Kibaba ambacho kilitumika kupimia vitu kama Mchele na unga,kwa kawaida kibaba hiki kilikua ni kopo fulani hivi lenye ujazo wa Appx 400-500 gram, nakumbuka baadhi ya wafanyabiashara walikua wakiyaponda haya makopo/vibaba kwa chini ili yabonyee na kupunguza kipimo cha mchele/unga n.k
Kwa nini unasema havina asili ya India?, yaani haiwezekani wahindi kuwa ndio waanzilishi na vilifika Uingereza vikitokea India?