Vipimo vya kuwalinganisha Rais Mstaafu Kikwete na Rais Magufuli

darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
8,881
17,486
Huwa nachukizwa na watu wanaolinganisha marais wetu wapendwa bila kuzingatia vigezo au kutumia kigezo kimoja na kisha kutoa maamuzi ya ubora.Ninachotaka kusema ni kwamba ni mapema mno kulinganisha watu hawa kwani ndio kwanza JPM hajafikisha hata mwaka mmoja.Hapa nimeorodhesha baadhi ya vitu vinavyoweza kuwalinganisha watu hawa hapo baadaye.

1.ELIMU
Idadi ya vyuo vikuu vilivyojengwa na idadi ya wahitimu wanaomaliza vyuo
Uhakika wa kupata elimu bora kwa mtoto wa maskini.
idadi ya maabara mpya mashuleni
uwepo wa mazingira mazuri wa ujifunzaji na ufundishaji
Idadi ya kutosha ya walimu
Ubora wa elimu


2.AJIRA
Idadi ya ajira mpya zilizotolewa serikalini
Idadi za ajira mpya zilizotolewa sekta binafsi
Fursa na ustawi wa mtumishi wa umma
Malipo na stahiki zilizolipwa za mtumishi wa umma
Motisha na morali ya ufanyakazi kwa mtumishi wa umma
Ajira katika ujasiriamali
Maadili ya mtumishi wa umma

3.AFYA
Upatikanaji rahisi wa huduma za afya Mf idadi za zahanati vijiji,mijini nk
uwepo a miundombinu na vifaa vya tiba
wahudumu wa kutosha
Tiba bora

4.UCHUMI
Tofauti ya ukusanyaji mapato ya serikali katika miaka yote waliyoongoza kutoka kwa warithi wao.
Ukuaji wa kipato cha mtu binafsi
Mazingira mazuri ya ujasiriamali
unafuu au ukubwa wa kodi
Nafasi ya taifa katika viwango vya kimataifa vya umaskini na utajiri mfano toka ya 3 mwaka 2004 mpaka 47 mwaka 2015

5.NISHATI NA MADINI
Asilimia za upatikanaji wa umeme mijini na vijijini.(zimeongezeka au la)
Idadi na matokeo ya tafiti za madini
Sheria za madini
Pato la taifa kutoka sekta ya madini
Idadi za megawati za umeme zinazozalishwa
Uwekezaji mkubwa katika miundo mbinu ya umeme kv usafirishaji
Upatikanaji rahisi na nafuu wa nishati kwa mtumiaji.

6.MAHUSIANO
Mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi yetu na nchi za nje.
Heshima ya kiongozi/viongozi wetu katika medani ya kimataifa
Heshima na nafasi ya nchi yetu kimataifa
Uhusiano chanya wa serikali na wananchi wake

7.DEMOKRASIA/SIASA
Chaguzi huru na zenye haki
Mipaka ya viongozi wa serikali dhidi ya sheria na katiba
Uhuru,usawa wa kila raia bila kujali kanda, kabila,jinsia,jinsi au dini
Uhuru wa binafsi kutoa maoni
Uhuru wa kukutana na kujadili mambo yanayohusu jamii mf mikutano ya kisiasa
uhuru wa vyombo vya habari

8.MIUNDOMBINU/MAWASILIANO/
Idadi ya kilometer za reli zilizojengwa.
Idadi ya kilometer za barabara zilizojengwa katika kiwango cha lami
Uboreshaji wa mawasiliano mf ongezeko la watumiaji wa simu ua kupungua
Gharama au unafuu wa upatikanaji wa taarifa toka radio,tv,magazeti
Uwekezaji mkubwa katika mawasiliano kuhakikisha huduma za mitandao zinapatikana.mfano Mkonga wa Taifa,halotel nk
Unafuu katika gharama za usafirishaji mizigo na abiria
Ubora wa vyombo vya usafirishaji
Kupungua au kuongezeka kwa idadi ya wamiliki vyombo vya usafiri binafsi mfano pikipiki,magari,baskeli
Upunguaji wa foleni, BRT au Metro train
Uboreshaji wa huduma za ndege nchini na unafuu wake

9.TEJNOLOJIA/
Uingizaji na matumizi ya teknlojia mpya katika nyanja mbali mbali

10.USALAMA
Usalama wa raia na mali zao
Usalama wa mali za umma
Usalama wa nchi na mipaka yake
Haki za raia

11.BUSARA/HEKIMA/AKILI
Maamuzi yenye busara katika masuala ya kitaifa na kimataifa



mengineyo wadau mtaongezea
 
Bora jk,huyo p,maneno mengi matendo zero,busara ya kuzaliwa nayo hana,na s kimbilio la wanyonge hata.
 
Back
Top Bottom