Vipi kwa upande wa Daraja la Kigamboni?

Vipi kwa upande wa Daraja la Kigamboni?

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Posts
19,042
Reaction score
22,592
MAGOGONI.JPG
 
Kigamboni kuna watu zaidi ya milioni moja. Daraja peke yake na vivuko peke yake havitoshi... Lazima vishirikiane...
 
Shida iliyopo ni kwamba tumejenga daraja ila kwa lengo la biashara na sio kuwa saidia wana nchi leo hii pamoja na kujenga daraja kuna daladala za kariakoo tu kwanini amna za kwenda sehemu nyingine?ushawahi kujiuliza na daladala zinazo fanya kazi kule kwasasa niza mtu mmoja na ni mbunge,daladala moja inalipa 5000 kila ikipita licha ya kwamba zinasaiidia jamii wanashindwa kutoa fever basi,ila wanajua kwamba wakiruhusu daladala kwa wingi kivuko kitapoteza mapato!!!,lakini pia kipande kilicho baki ambacho ndo kina jengwa kwa sasa kinafanya watu wengi wa magari waone bora kupita fel kuliko darajani
Pia uwa sichoki kuwaomba viongozi wawa kemee walinzi wao wa darajani pale wanapageuza mtaji wanalipisha watu kupiga picha hata kwa simu huu ni upuuzi
 
Shida no umbali. Unataka kwenda wapi? Wewe unataka kwenda bank kuu. Na ukipanda ferri ni karibu kuliko darajani. Unakwenda hazina. Unakwenda Post nk. Na wewe una gari. Darajani unakwenda Airport. Kariakoo. Mpirani. Ilala. Mambo ni mazuri sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magazeti yanapenda habari mbaya ambazo Watanzania wengi wanapenda kusikia. Sasa hivi kuna pantoni tatu, msongamano umepungua kiasi kwamba watu hawana hata ulazima wa kupita darajani, mimi mmoja wao. Muulize mtu anaekata tiketi darajani atakwambia jinsi magari yalivyopungua darajani.

Ukiwa mkazi wa kigamboni na mchunguzi utajua tabia za wapanda pantoni. Wengi wanapenda kusimama pale mbele ili wawe wa kwanza kuondoka, au wakati pantoni inakaribia utaona watu wote wanajazana mbele kabla haijasimama, pantoni inajaa kwasababu haiwezi kwenda tupu ni hasara. Ila kwasasa hivi shida ya usafiri imepungua. Mkazi wa Kigamboni ataelewa ila mnaosoma tu magazeti bila kuchanganya na zenu hamuwezi kuelewa.
 
Back
Top Bottom