Vipi kuhusu fedha za kwenye simu za marehemu?

Balungi

JF-Expert Member
May 25, 2011
234
162
Najiuliza kila siku ila sipati majibu.
Hivi inakuwaje kuhusu hizi fedha tunazozihifadhi kwenye mitandao ya simu, warithi wa marehemu wanapata stahili zao mara mtu anapofariki? Hii ni kwa sababu watu wengi hawajui kuhusu kiasi cha fedha marehemu alichokihifadhi na wengi wetu hatuweki wazi kwa wake/ watoto wetu au ndo faida za makampuni ya simu na wafanyakazi wao?
Mwenye ufahamu kuhusu hili.
 
Hiyo hua inapotelea huko huko inabidi sasa tuwaambie wabunge wetu hili jambo lifike bungeni itafutwe namna ya kuchukua hizo hela baada ya mwenye number husika kufariki kama ana hela kwenye mitandao hiyo
 
Hiyo hela ndo hiyo wanayosaidia watoto yatima na watu wenye kuhitaji misaada, utasikia tigo au voda tumetoa msaada kuchangia maendeleo eneo fulani au shule ndo hiyo hela ya marehemu japo kuna muda mfanyakazi mwenye uwezo wa kuichota huwa wanafanya hivyo ila ukigundulika kazi huna
 
Na wakati mwengine namba ya siri anaijua mwenyewe marehemu haswa ukizingatia siku hizi unaweza kumjulisha mwenzako namba ya siri akakumbea visenti vyote.
 
Najiuliza kila siku ila sipati majibu.
Hivi inakuwaje kuhusu hizi fedha tunazozihifadhi kwenye mitandao ya simu, warithi wa marehemu wanapata stahili zao mara mtu anapofariki? Hii ni kwa sababu watu wengi hawajui kuhusu kiasi cha fedha marehemu alichokihifadhi na wengi wetu hatuweki wazi kwa wake/ watoto wetu au ndo faida za makampuni ya simu na wafanyakazi wao?
Mwenye ufahamu kuhusu hili.

Kweli maisha magumu yaani tushafikia huku kupigia hesabu pesa za marehemu.
 
Mie nijuavyo ni kwamba huwa kuna wasimamizi wa mirathi ambao wanachaguliwa kwenye kikao cha wanandugu na baadae mchakato unakwenda hadi Mahakamani, sasa ni jukumu la hao wasimamizi kuwasiliana na mtandao husika ili waone alikuwa na shilingi ngapi na zitolewe kwa utaratibu kama ambavyo wanavyochukua pesa za marehemu kwenye akaunti zake benki
 
Familia inamchagua msimamizi wa mirathi, kisha atakwenda mahakamani kwaajili ya kuthibitisha undugu wake na marehemu , mahakama itatoa barua ya kumtambulisha msimamizi wa mirathi kwenye mtandao husika na kama benki vivyohivyo. Ndipo watampatia fedha.
Ila nimeshuhdia pesa za marehemu zinapotea kwa kukosa msimamizi.
 
Hapa ndipo penye utata, hao watu wa mitandao wanatoa ushirikiano kweli?
 
Back
Top Bottom