Kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu wa 2015 ni fursa muafaka kutafakari mustakbala wa nchi yetu katika nyanja mbalimbali. Nami nawasilisha Jukwani vipaumbele nionavyo vinafaa kujadiliwa/kutekelezwa katika nyanja za siasa/utawala bora kwa maslahi mapana ya Taifa letu:
1. Vyombo vya Habari vipewe uhuru na uwezo wa kutosha kufanya kazi zake kwa kujituma na kuwajibika kama Mhimili mmojawepo wa Demokrasia (fourth - -estate), sambamba na Serikali, Bunge na Mahakama. - -
2. Viwekwe vigezo mathubuti vya kutumika wakati wa kuamua kuongeza idadi ya mikoa, wilaya, kata na majimbo ya uchaguzi. Dhana ya "kusogeza huduma kwa wananchi" isitumike vibaya kama haina tija kichumi au ulazima kwani mara nyingine huwa ni kisingizio cha kuongeza nafasi za ubunge/udiwani kwa manufaa ya wanasiasa, na huleta mivutano ya -kikabila, kiitikadi au kimaeneo. -
3. Idadi ya Wizara iwe ndogo na ya kudumu na iwekwe kwenye Katiba ya Nchi kwa kuzingatia-mielekeo wa sekta; tuachane na dhana potofu kwamba ili sekta ifanikiwe ni lazima iwe na wizara "yake" yenyewe. - -
4. Pato la Taifa lisiwe shamba la bibi kwa vyama vya siasa vyenye wabunge. Ruzuku kwa vyama vya siasa ipunguzwe sana na iwe kwa matumizi maalumu tu (mfano gharama za ofisi, mawasiliano, n.k.), na ilingane kwa vyama vyote. Vyama vya siasa vijitegemee katika mahitaji mengine, kama ilivyo kwa vyama vingine vinavyofanya shuguli muhimu za kijamii, madhehebu, vyama vya wafanyakazi-n.k.
-
5. Mishahara na marupurupu ya Wabunge ipangwe na Tume huru siyo wao -wenyewe kupendekezeana na kupitishiana kwa kushirikana na Mawaziri ambao nao ni Wabunge, na kwa vyyovyote vile viwango visizidi vile vya ngazi za juu za watumishi wa Serikali. - -
6. Ipo haja ya kurudisha heshima ya nyadhifa za ubunge au udiwani kuwa ni nafasi za kutumikia wananchi kwa moyo wa kujitolea na kujinyima - kwa ajili ya wenye wito huo.- Tuondoe dhana kwamba ubunge au udiwani ni ajira, kwa mfano kusema "Mbunge ni Mwajiriwa wa Bunge". Kwa sasa, baadhi ya wanaojitosa kugombea nafasi hizo wanavutiwa tu na mishahara minono, marupurupu na mianya ya kujinufaisha kibiashara, na hawana wito -au uwezo wa uongozi. - -
7. Mfumo wa Kukatua Madaraka Wilayani uimairishwe - Halmashauri ziongezewe uwezo - -wa kupanga, kujadili na kusimamia maendeleo katika maeneo yao kwa kuongezewa mgao wao wa moja kwa moja wa Bajeti ya Taifa, kuzidi jumla ya mgao unaotengwa kwa ajili ya Serikali Kuu/Wizara. - -
8. Bunge liwe jukwaa takatifu la kujadili kwa kina masuala yanayohusu mwelekeo wa Taifa ikiwemo Katiba, Sera, Sheria, Mikataba ya kimataifa na masuala - -mengine ya kitaifa. Makundi mbalimbali ya wananchi yahusishwe kikamilifu katika mashauriano kabla ya maamuzi kufikiwa. Bunge pasiwe mahala pa - -kuvutana kuhusu Mbunge gani katengewa nini kwa wapiga kura wake. - -
9. Maamuzi muhimu ya maendeleo yasifanywe kisiasa zaidi. Tuondoe hali ya Mawaziri, Wabunge- na Madiwani kuchukuliwa kama miunguwatu au masultani wasiopaswa kupingwa au kukosolewa na wataalamu wa sekta wakati -wa kufanya maamuzi yanayohusu maendeleo ya nchi. -
-10. Mipango na miradi ya maendeleo ya nchi ipangwe kisayansi na Wizara au - -Halmashauri husika kwa kuzingatia rasilimali na vipaumbele vilivyopo, - -siyo kutekeleza ahadi za wagombea. Tuachane na dhana kwamba Wabunge au - -Madiwani ndiyo wenye jukumu la kuleta maendeleo kwenye maeneo yao au kuwa - -kama wafadhili. Dhana hii huleteleza wao kudai mishahara na marupurupu - -minono isiyoendana na hali halisi ya mapato ya Serikali au malipo - -wanayopata watumishi wengine wa umma.
Nawasilisha na kukaribisha mjadala. Asanteni.