Vipaumbele vitatu vya Serikali ya Magufuli

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Serikali ya Magufuli ina vipaumbele vitatu kwa mtazamo wangu. Na naipongeza kwa uchaguzi makini wa vipaumbele hivi. Navyo ni kama ifuatavyo
1.Mapato
2.Mapato
3.Mapato
Ningependa ukwepaji kodi hata kama ni kidogo liwe ni kosa la kuhujumu uchumi na wakwepa kodi wapewe adhabu kubwa sana ikiwa ni pamoja na kucharazwa viboko.
 
Wewe unahitaji
1.Elimu
2.Elimu
3.Elimu
Mapato hata kama yatakuwa kwa asilimia 900% kama hakuna uzalishaji wa ndani,uuzaji bidhaa nje na matumizi mazuri ya mapato hayo ni kazi bure.
 
Kama kweli hivi ndio vipaumbele vya Magufuli basi kuna tatizo kwa watunga sera na wapanga mipango waliopo serikalini....kwa hiyo ule mpango wa kuifanya nchi kuwa ya uchumi wa kati kupitia mapinduzi ya viwanda ndio basi tena...??
 
SUBIRINI Tu Akusanye Matrion Kwanza!!! Alafu Aanze Kutekeleza Ahadi Zake Alizohidi Watanzania Wkt Akiomba Ridhaa Yao, Maana Ziko Lukuki!!! MF.Kila Kijiji Million 50, Kata 150, Kila Kijiji Zahanati, Kata Kituo Cha Afya, Wilaya Hospital Yenye Hadhi Hiyo Na Kila Mkoa Hospital Ya Rufaa!! TENA Zikiwa Na Waganga, Wauuguzi, Vifaa Tiba Na Dawa Za Kutosha!! KILA Mkoa VIWANDA Vidogo, Vya Kati Na Vikubwa! MAJI Safi Na Salama, ELIMU Bure, Vivuko Na MELI Za Abiria Na Mizigo N.k!! SASA Bila KUKUSANYA Hayo Matrion, Ataweza KUTEKELEZA Hizo Ahadi Zake /Zao!!!!!?? TEHE! Tehe! Tehe!!!
 
Kama kweli hivi ndio vipaumbele vya Magufuli basi kuna tatizo kwa watunga sera na wapanga mipango waliopo serikalini....kwa hiyo ule mpango wa kuifanya nchi kuwa ya uchumi wa kati kupitia mapinduzi ya viwanda ndio basi tena...??
Nyie mnafikiri kuwa na viwanda wakati kodi makusanyi.
 
Wewe unahitaji
1.Elimu
2.Elimu
3.Elimu
Mapato hata kama yatakuwa kwa asilimia 900% kama hakuna uzalishaji wa ndani,uuzaji bidhaa nje na matumizi mazuri ya mapato hayo ni kazi bure.
Hivyo viwanda mtajenga kwa mawe? Kusanya kodi kwanza.. ukiwa na fedha hata akili inakaa vizuri
 
Hivyo viwanda mtajenga kwa mawe? Kusanya kodi kwanza.. ukiwa na fedha hata akili inakaa vizuri
Ukiwa na fedha akili inakaa vizuri ??? Hivi kwenye mapato yako unapanga mipango kisha kutafuta fedha au unapata hela kisha unapanga ??? Kama unapata halafu ndo unapanga naomba uniambie na ni kwa asilimia gani umeweza kutekeleza mipango yako ??? Tusije tukawa tunaongelea serikali kumbe we mwenyewe hujielewii.
 
Wewe unahitaji
1.Elimu
2.Elimu
3.Elimu
Mapato hata kama yatakuwa kwa asilimia 900% kama hakuna uzalishaji wa ndani,uuzaji bidhaa nje na matumizi mazuri ya mapato hayo ni kazi bure.
enzi tuliyopo ni ya huduma hivyo viwanda vinakuwa chaguo la pili na kilimo la kumi huko!
 
Ukiwa na fedha akili inakaa vizuri ??? Hivi kwenye mapato yako unapanga mipango kisha kutafuta fedha au unapata hela kisha unapanga ??? Kama unapata halafu ndo unapanga naomba uniambie na ni kwa asilimia gani umeweza kutekeleza mipango yako ??? Tusije tukawa tunaongelea serikali kumbe we mwenyewe hujielewii.
Serikali yoyote ambayo haikusanyi mapato haifai ndugu yangu.. Mipango ipo tena mizuri.. ila fedha tunaachia wahuni .. Mipango sio tatizo lannchi hii. ipo nanitakuwepo.. shida ni fedha.
 
Hakuna serikali inayong'ang'ania viwanda huku haikusanyi kodi. Kwavyovyote mapato lazima yadhibitiwe ndipo tupate elimu bora, nishati ya kuchochea uwekezaji wa viwanda,huduma bora za afya nk.
Sasa unazurura ulaya kutafuta wawekezaji kwenye viwanda wakati husomeshi wataalamu,umeme mgogoro,uchukuzi (treni,ndege) hakuna,uzalishaji malighafi (kilimo/mifugo) duni nk. Huo ni uchizi Kama uchiz mwingine
 
Serikali ya Magufuli ina vipaumbele vitatu kwa mtazamo wangu. Na naipongeza kwa uchaguzi makini wa vipaumbele hivi. Navyo ni kama ifuatavyo
1.Mapato
2.Mapato
3.Mapato
Ningependa ukwepaji kodi hata kama ni kidogo liwe ni kosa la kuhujumu uchumi na wakwepa kodi wapewe adhabu kubwa sana ikiwa ni pamoja na kucharazwa viboko.

Ukiwa na hela yote yanawezekana
 
KWA UPANDE WANGU KUNA VITU AMBAVYO WATANZANIA WALITAKA KUONA. KWA ZILE SIKU 100 AMBAZO ALISEMA ANGETATUA.
1. STRATEGIES ZA ELIMU BURE, SIO UNA EMPLEMENT BILA KUWA NA MIPANGO MIKAKATI YA KUENDELEZA JAMBO HILI
2. STRATEGIES ZA KUWAINUA WASANII, WA TANZANIA KUANZIA BONGO FLAVOUR MPAKA BONGO MOVIES, WAKATI ILIKUWA MOJA YA SERA ZAKE MATOKEO YAKE AKAZUNGUKA NAO NCHI NZIMA KISHA KAWATELEKEZA . JAPO KWA KUWATUNGIA SHERIA ZAO, (WAZIRI HUSIKA ALICHUKUA HILI KAMA CHANGAMOTO)
3. STRATEGIES ZA KUONGEZA NAFASI ZA AJIRA, (KUTATUA CHANGAMOTO ZA MISHAHARA KWA PRIVATE SECTORS) EITHER KWA KUTAFUTA WAWEKEZAJI ZAIDI, AU KWA KUHAKIKISHA KUNA MIKAKATI MADHUBUTI INAYOONEKANA KURUDISHA VIWANDA VYA SELEKALI KATIKA KAZI ILI NAFASI ZA AJIRA ZIONGEZEKE. (SIO KUJIFUNGIA TU NDANI UNADHANI WATAKULETEA VIWANDA HUMU, UNAPASWA KUWAELEZA JINSI GANI NCHI YAKO IKO PROFICIENT KWA KUWEINCEST.
4. STRATEGIES ZA KUPAMBANA NA KULIMIT RUSHWA TANZANIA. KWA HII FUKUZA FUKUZA, RUSHWA HAIJAKOMA BALI IMEZIDI KUSHIKA KASI NA ZINAZOONGOZA KWA RUSHWA NI GOVEMENTAL INSTTUTIONS, AMBAZO YEYE NDIYO RAISI WA GOVERNMENT HII.
5. MUNGILIANO WA MAJUKUMU KWA MAWAZIRI KIASI KWAMBA WANASHINDWA KUFANYA KAZI ZAO KIUKAMILIFU AKIFIKIRIA KUWA SIO MAJUKUMU YAKE BALI NI YA TU MWINGINE HIVYO JAMBO HUSIKA KUACHWA SOLEMBA NA WATANZANIA WAKIBAKIA DILEMA.
6. KUKOSA MBINU THABITI ZA KUINUA UCHUMI WA NCHI, PIA KUIMARISHA THAMANI YA SHILINGI YETU.
HAYO HAPO JUU NI MAJIPU MAKUBWA AMBAYO BABA MZEE POMBE MAGUFULI HAWEZI NA HAJATHUBUTU KUYAGUSA,
 
Siku 100......
Awali, hicho ni kipindi kifupi kurealise mabadiliko makubwa kama ya ongezeko la ajira au uzalishaji kupitia uwekezaji kama vile wa viwanda. Hiki ndio kipindi cha kuchambua na kutafakari namna ya kujenga upya misingi imara zaidi, baada ya kutambua mapungufu yako wapi kupitia tathmini za uhakika.
Kitendo cha kutuonyesha udhaifu uliopo kwenye udhibiti wa mapato ni fanikio mojawapo la kupongeza.
Systems zetu zipo kwa muda mrefu na zimejijengea maadili tofauti na matarajio.....kumbukeni hao hao wanaomsaidia leo ndio waliokuwepo jana wakiendesha mambo na huyo aliyemkabidhi hicho kijiti.
 
Back
Top Bottom