Vipande hatari vya barabara nchini

Ungekutana na za Iyovi - Mikumi na hizo gari - ndege za chini ungesemaje?

izo za iyovi driver anaendesha huku anavuta sigara?
akizizoea za iyovi mwambie aende za lukumburu, njombe-songea, asisahau mifuko ya kutapikia
 
Barabara ya Mto wa mbu kwenda Karatu noma. Ukiachilia sehemu ya daraja na kipande cha barabara kuharibiwa vibaya na mawe pamoja na magogo yaliyoletwa na maji, uwekekano wa lami kumeguliwa na maji yanayopita pembezoni mwa barabara (along the road especially from up to downhills) ni mkubwa iwapo Tanroads hawatachangamka mapema kutengeneza mitaro mikubwa pembezoni mwa barabara. Ukiwa unapandisha kutoka Mto wa mbu kwenda Manyara then Karatu utaona jinsi maji yalivyokula pembezoni mwa barabara.
 
Barabara ya kutoka Minjingu hadi Arusha noma mzee. Ina mashimo mashimo ya hapa na pale na mawimbi ya kutosha. Kama ni mgeni wa njia usithubutu kwenda mwendokasi wa 100 - 140 KPH nenda tu mdogomdogo ufike salama.
 

Kwa sisi tiliosafiri katika barabara ya Songea - N jombe tangu mwanzoni mwa miaka ya sabini tunafahamu vyema hali ilivyokuwa husisan ktk milima ya Lukumburu.Tulikuwa tunatumia siku mbili kupita kipande hicho lakini kwa sasa ni nusu saa tu. Hata hivyo, barabara hiyo kweli ni nyembamba sana na ina kona nyingi na kwa hiyo inatakiwa kuwa re-designed.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…