Viongozi wetu jihadharini...Waingereza ni wasengenyaji!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
18,173
13,776
Kusengenya mtu, kwa mila za kiafrika si tabia nzuri.
Usengenyaji ni dharau ya hali ya juu.

Wiki hii tumeshuhudia usengenyaji uliofanyikabkitsifa kwa viongozi ambao si tu wanajulikana sana, lakini taifa lao ni mkubwa, Uingereza.

Waziri Mkuu wa Uingereza ,David Cameron, alisikika akiwasengenya Nigeria na Afghanistan, kuwa ni nchi za wala rushwa wa kutupwa duniani.
Huku alikuwa amewaalika kuongelea masuala ya rushwa siku ya pili yake.
Cameron alikuwa akimpasha Malkia wake Elizabeti!

Malkia Elizabeti naye alisikika akiwananga Wachina kuwa hawakuwa wastaarabu walipomtembelea!
Hii ilikuwa wakati wa ziara ya kiongozi wa China Uingereza, Xi Ping mwaka jana.
Malkia alikuwa akiteta na kapolisi ka kike kenye cheo cha chini sana kiwadhifa.
Haya yote yamezua maswali.
Hawa waingereza, watu wa visiwani hawa, ni watetaji na wasengenyaji wakubwa, viongozi wetu walielwe hilo.
 
Ile ni aibu ya mwaka na inavyoonekana Malkia hafuatilii siasa za kimataifa na Cameruni ameshajua udhaifu wa malkia katika siasa za kimataifa ndio maana anatoa taarifa za uongo kwa Malkia. Ila Buhari keshasema yeye hataki majibizano anadai pesa zake zilizofichwa kwenye mabenki UK.
 
Hivi mtu akisema Tanzania ni nchi corrupted atakuwa anakusengenya? Kama Buhari anapambana na rushwa maana yake kunatatizo la rushwa. Kama JPM anapambana na mafisadi halafu kuna rais wa nchi nyingine anasema Tanzania inatatizo la rushwa! kwan atakuwa amekusengenya? Mtu huyo huyo akisema Tanzania imepata mpambanaji wa rushwa ambae ni JPM mtasifia usiku na mchana ila wakikosoa inakuwa tatizo. Ndio maana karne ya leo bado tunahangaika na sukari!
 
Sasa mtu kusema nchi flani Ni corrupt Ni usengenyaji? Wakati kwa uchunguzi wake amegundua Hilo...jambo likisemwa uliyekosea yakupasa kubadilika iwapo siozuri.
Tatizo kunawatu hupenda kusifiwa tuuu!! Anyways kama kunavitu vya kutahadharisha viongozi wetu this is the last and least
 
Yan ukiskia watu wabaya ni hawa jamaa tena Mara Mia ya makabulu hawa jamaa ni wabaya sana zaid wao kwao hta hawapendan,yan wana majungu ya kmiakmia ni balaa.ukiwa nao wanajifanya kukuchekea na kukusifia ukiwapa mgongo wanaanza kukutete yan ni shida.
 
Waingireza ni wastaarabu sana, ni wakweli lakini hawana jeuri ya kukuambia usoni watakusema pembeni. Buhari mwenyewe amakubali Nigeria ni very corrupt country. Kwa rais wa nigeria kukubali tatizo ni mwanzo mnzuri kwani anajua tatizo liko wapi.
Sio wastaarabu... sio wakweli na ni wanafiki wakuu

Kuhusu suala la corruption, Buhari said it even before he became a president, na ameendelea kusema hayo... that is nothing new! Wazungu, na hasa waingereza ni corrupt mno, masuala ya rada, ESCROW and many deals wao wamo kwenye uhusika, but they always shift blame to others... Wazungu wanahonga sana wanasiasa na watendaji wetu ili wapate favors kwenye many business deals (and they try to clean their deed na maneno matamu)...

many russians and arabs wamewekeza UK na hao hao huonekana kama wakiukaji wa haki za binadamu na corrupt (in case wanawekeza Africa)

I like Buhari alivyowajibu kwamba ni kweli kuna corruption na hajawaomba wamwombe msamaha, lakini warudishe pesa zinazofichwa mchini kwao

Time to call a spade, a spade; na nimefurahi Magu kaishia Uganda, badala ya kwenda kwenye kikao cha kinafiq
 
Hivi mtu akisema Tanzania ni nchi corrupted atakuwa anakusengenya? Kama Buhari anapambana na rushwa maana yake kunatatizo la rushwa. Kama JPM anapambana na mafisadi halafu kuna rais wa nchi nyingine anasema Tanzania inatatizo la rushwa! kwan atakuwa amekusengenya? Mtu huyo huyo akisema Tanzania imepata mpambanaji wa rushwa ambae ni JPM mtasifia usiku na mchana ila wakikosoa inakuwa tatizo. Ndio maana karne ya leo bado tunahangaika na sukari!
Kwa mifano miwili iliyoyolewa, inaonekana kabisa Waingereza hawana ustaarabu wa kukuambia kitu usoni, ila wanakusema mgongoni.
Hata waandishi wa BBC waliorekodi usengenyaji wa Cameron na Malkia hawakupenda tabia hiyo.

Ukiona kitu kibaya unampa mtu ukweli wake usoni, si maneno maneno ya pembeni.
Tabia za uswahili swahili wa kiingereza.
 
Kusengenya mtu, kwa mila za kiafrika si tabia nzuri.
Usengenyaji ni dharau ya hali ya juu..

Sio hivyo tu, ni wazindiki, ndumilakuwili, kujifanya wao wanapenda haki, kumbe, haki zao ni kama manukato tu, viongozi wakiiba wanapeleka mahela kule, waingereza wanajuwa kabisa ila wataanza kujishaua hiki na kile sijui haki za binadamu sijui nini ali mradi tu zile hela zibaki kule, kama wangekuwa na moyo wa kibinadamu hawa kweli wangekuja kututawala na kutunyonya miaka yote ile?! Shukurani ziwaendee watemi wetu na mababu kwa kuwakatalia na kuwaondoa nchini, hawa jamaa wanajidai wanatuletea misaada ya kufa mtu wakati kiukweli hela wanayochota hapa ni zaidi ya makumi kuliko wanayoleta kama misaada, TUZINDUKE NA HAWA KUPE..
 
Ningependa wajuzi watujuze hawa jamaa toka walivyotuvamia na kuanza kutunyonya walifaidika kwa kiasi gani mpaka sasa, nasikia makumbusho zao zimejaa mali kutoka Asia, Afrika na sehemu kadhaa, kuzirudisha hawataki, leo hiii wanajidai wao wasafi?! NDOROBO WAKUBWA..
 
Tujenge utamaduni wa kujadili HOJA na sio MTOA HOJA.Buhari ameonesha ukomavu katika kudadavua hoja yenyewe,hakutaka malumbano na mtoa hoja.
 
Ningependa wajuzi watujuze hawa jamaa toka walivyotuvamia na kuanza kutunyonya walifaidika kwa kiasi gani mpaka sasa, nasikia makumbusho zao zimejaa mali kutoka Asia, Afrika na sehemu kadhaa, kuzirudisha hawataki, leo hiii wanajidai wao wasafi?! NDOROBO WAKUBWA..
Mnafiki anajulikana kwa vitendo vyake.
Ameambiwa na Buhari-rudisha hela yetu sasa, mnafiki kimya!
 
Kwa mifano miwili iliyoyolewa, inaonekana kabisa Waingereza hawana ustaarabu wa kukuambia kitu usoni, ila wanakusema mgongoni.
Hata waandishi wa BBC waliorekodi usengenyaji wa Cameron na Malkia hawakupenda tabia hiyo.
Vyombo vyao vya habari ndo vinanipa rah
Ukiona kitu kibaya unampa mtu ukweli wake usoni, si maneno maneno ya pembeni.
Tabia za uswahili swahili wa kiingereza.
Haaaa haaa ila kamera huwa inawaumbua kishenzi. Waziri mkuu mstaafu Kabla hajapigwa chini kampeni Za mwisho mwisho alimaliza kukutana na waapiga kura mama mmoja kamlima swali lililomkera wakati anaondoka alisahau kuwa mic iko on kamshushua zinga la tusi akijua anaongea na walio kwenye gari tu huo mtindo wao alimkashifu kishenzi kumbe mic iko live iliwachefua wapiga kura nahsi nayo ilishusha kura zake ila wapiga kura walimmind balaa. Tabia hiyo wanayo na wanaweza wakakusema ukiwa nao especially wakijua kuwa si lugha yako ya kwanza Yaani ni Kama utamaduni kusengenya.
 
Sio hivyo tu, ni wazindiki, ndumilakuwili, kujifanya wao wanapenda haki, kumbe, haki zao ni kama manukato tu, viongozi wakiiba wanapeleka mahela kule, waingereza wanajuwa kabisa ila wataanza kujishaua hiki na kile sijui haki za binadamu sijui nini ali mradi tu zile hela zibaki kule, kama wangekuwa na moyo wa kibinadamu hawa kweli wangekuja kututawala na kutunyonya miaka yote ile?! Shukurani ziwaendee watemi wetu na mababu kwa kuwakatalia na kuwaondoa nchini, hawa jamaa wanajidai wanatuletea misaada ya kufa mtu wakati kiukweli hela wanayochota hapa ni zaidi ya makumi kuliko wanayoleta kama misaada, TUZINDUKE NA HAWA KUPE..

Achana na waingereza, Ghadaffi alipanua London School of Econamy, alikuwa mfadhili mkubwa na mwanae alisoma pale, kilivyonuka walimkanaa! Walisema hawakujua kuwa ilikuwa blood money!
 
Ile ni aibu ya mwaka na inavyoonekana Malkia hafuatilii siasa za kimataifa na Cameruni ameshajua udhaifu wa malkia katika siasa za kimataifa ndio maana anatoa taarifa za uongo kwa Malkia. Ila Buhari keshasema yeye hataki majibizano anadai pesa zake zilizofichwa kwenye mabenki UK.

Sio uongo wana Nigeria ni wala rushwa kwani uwongo? Hakusema buhari mla rushwa
 
Kumbukumbu zinasema Buhari alichaguliwa na jukwaa la kupambana na ufisadi ili kuweza kukomesha hayo matendo na anajitahidi sana. Ila kauli za kinafiki kama zile zinaonyesha kuna wanaobeza na kudharau jitihada zake.
 
Nigeria na Tanzania tunapishana kidogo sana kwa rushwa. Ukisikia Nigeria inatajwa, ujue Tanzania haiko mbali. Tuwage wakweli na kukubali kukosolewa, badala ya kukurupuka kukanusha kila kitu.
 
Kusengenya mtu, kwa mila za kiafrika si tabia nzuri.
Usengenyaji ni dharau ya hali ya juu.

Wiki hii tumeshuhudia usengenyaji uliofanyikabkitsifa kwa viongozi ambao si tu wanajulikana sana, lakini taifa lao ni mkubwa, Uingereza.

Waziri Mkuu wa Uingereza ,David Cameron, alisikika akiwasengenya Nigeria na Afghanistan, kuwa ni nchi za wala rushwa wa kutupwa duniani.
Huku alikuwa amewaalika kuongelea masuala ya rushwa siku ya pili yake.
Cameron alikuwa akimpasha Malkia wake Elizabeti!

Malkia Elizabeti naye alisikika akiwananga Wachina kuwa hawakuwa wastaarabu walipomtembelea!
Hii ilikuwa wakati wa ziara ya kiongozi wa China Uingereza, Xi Ping mwaka jana.
Malkia alikuwa akiteta na kapolisi ka kike kenye cheo cha chini sana kiwadhifa.
Haya yote yamezua maswali.
Hawa waingereza, watu wa visiwani hawa, ni watetaji na wasengenyaji wakubwa, viongozi wetu walielwe hilo.
Heri kuwa visiwani kuliko kuwa bara na shombo ya umasikini, udikteita, ujinga, maradhi and all misfortunes known to human being
 
Haaaa haaa ila kamera huwa inawaumbua kishenzi. Waziri mkuu mstaafu Kabla hajapigwa chini kampeni Za mwisho mwisho alimaliza kukutana na waapiga kura mama mmoja kamlima swali lililomkera wakati anaondoka alisahau kuwa mic iko on kamshushua zinga la tusi akijua anaongea na walio kwenye gari tu huo mtindo wao alimkashifu kishenzi kumbe mic iko live iliwachefua wapiga kura nahsi nayo ilishusha kura zake ila wapiga kura walimmind balaa. Tabia hiyo wanayo na wanaweza wakakusema ukiwa nao especially wakijua kuwa si lugha yako ya kwanza Yaani ni Kama utamaduni kusengenya.

Ile kamera imewaumbua..... kweli? unaumbuka kwa kusema ukweli?
 
Back
Top Bottom