Viongozi wasiojua wajibu wao ni Jipu

Mpenda Siasa

Member
Feb 9, 2011
8
2
Habari Wanajamii Forums,
Katika kumbukumbu zangu Enzi za tawala ya JKN halmashauri zote zilikuwa na taratibu za kutoa huduma kwa jamii husika kama vile ukusanyaji wa taka na nyinginezo kwa kutumia kodi na makusanyo mengine kam ushuru na mazingira kwa ujumla yalikuwa yanaridhisha.
Hivi sasa utasikia viongozi na hasa wa hizo halmashauri wakipanga mikakati hewa kwa wananchi ambayo wanashindwa kuhisimamia ipasavyo kama suala la taka.

wananchi wengi wapo tayari wengine hata kuchangia gharama za uzoaji wa taka hizo lakini viongozi hao wa mitaa au kata ndio kwanza wanashindwa kutekeleza.
Na hili nalo linaitaji Presda au PM au Waziri wa mazingira ?
Nafikiri viongozi inabidi muwe Creative na hasa kwenye masuala yahusuyo field yako.
Sio kila kitu hadi viongozi wajuu waje wawapangie mipango kwenye maofisi yenu.
 
Wengi ya viongozi wetu wamekariri hawanaga mapya.
ukiangalia wanaokimbiliaga udiwani hawajui nini wawafanyie wananchi wao zaidi ya siasa.
Wananchi hawataki siasa sasa wanataka matendo kwahiyo nakuunga mkono mtoa mada viongozi wengi wanatakiwa wabadilike.Ni wakati wa Action kwenda mbele.
Kuweka mikakati ya kuimarisha ulinzi kwenye Makata maana siku hizi kuna Polisi kata.
kufanya shughuli zote za kujenga nchi viongozi wa chini ndio kila kitu ......uraiani ndio kuna wauza unga,wezi nk kwahiyo uwajibikaji ukianzia chini kila kitu kitaenda sawa.
Sidhani kama waziri wa mambo ya ndani atapata habari za wahamiaji haramu,na wafanya biashara haramu bila msaada wa wananchi kupitia ngazi za chini kama watendaji wa vitongoji ambao ni waajiliwa wa halmashauri zetu.
Kwahiyo viongozi wetu waende na kasi za kina Makonda wawe wabunifu kwa kweli
 
Back
Top Bottom