Viongozi waliopora nchi zao mamilioni ya pesa wakiwa madarakani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_93772678_mediaitem93772677.jpg
Zaidi ya dola milioni 11 zinaripotiwa kutoweka kutoka kwa hazina ya taifa nchini Gambia, kufuatia kuondoka kwa kiongozi wa muda mrefu Yahya Jammeh.

Jammeh alikwamia madaraka kwa karibu miezi miwili licha ya kushindwa kwenye uchaguzi wa urais mwezi Disemba.

Bwana Jammeh ambaye kwa sasa yuko nchini Equatorial Guinea, si kiongozi wa kwanza anayelaumiwa kwa kupora pesa za umma. Kuna wale walipora nyingi zaidi na hawa ni baadhi yao.

Sani Abacha, Nigeria

_93772357_mediaitem93772356.jpg
Sani Abacha, kiongozi wa Nigeria kutoka mwaka 1993 hadi 1998, aliripotiwa kupora kati ya dola bilioni moja na bilioni 5 kutoka kwa hazina ya taifa. Mwaka 2014 idara ya haki nchini Marekani ilisema kuwa ilitwaa mali ya Abacha yaliyokuwa yameibwa ya thamani ya dola milioni 450.

Suharto, Indonesia

_93772288_mediaitem93772287.jpg
Suharto, rais wa Indonesia kutoka mwaka 1967 hadi mwaka 1998, anadaiwa kuisafisha hazina ya taifa ya nchi kwa hadi dola bilioni 35. Mwaka 2000 aliwekwa chini ya kuzuizi cha nyumbani na kushtakiwa kwa kuiba dola milioni 570. Lakini madaktari waligundu kuwa alikuwa mgonja sana kuweza kufika mahakamani . Aliaga dunia mwaka 2000 .

Mobutu Sese Seko, Zaire

_93772353_mediaitem93772292.jpg
Kiongozi wa Zaire ambayo sasa ni Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kutoka mwaka 1965 hadi mwaka 1997, Mobutu aliongoza utawala dhalimu ambao ulikandamiza upinzani. Pia aliishi maisha ya anasa na kujirundikia mali nyingi ikiwemo nyuma ya viumba 30 huko Lausanne ya thamani ya dola milioni 5.5. Anakisiwa kuiba dola bilioni 5.

Ferdinand Marcos, Ufilipino

_93772563_gettyimages-56905178.jpg
Mke wa Marcos, Imelda alikuwa na viatu 3000. Marcos anaaminiwa kuiba dola bilioni 10 akiwa madarakani kati ya mwaka 1965 na 1986. Baada ya kifo chake kesi kadha ziliilazimisha Uswizi ambapo alificha pesa hizo kurudisha karibu dola milioni 7000 kwa utawala wa Ufilipino.

Ali Abdullah Saleh, Yemen

_93772567_mediaitem93772566.jpg
Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh anakisiwa kupora karibu dola milioni 60 wakati akiwa ofisini. Aliondolewa madarakani mwaka 2012 wakati wa mapinduzi ya nchi za kiarabu lakini sasa anashirikiana na waasi wa Houthi katika nchi hiyo iliyokumbwa na mapigano.

Slobodan Milosevic, Serbia

_93772572_gettyimages-57057219-1.jpg
Slobodan Milosevic, Ni kiongozi dhalimu ambaye aliitawala Serbia kati ya mwaka 1989 na 1997. Alishtakiwa kwanza kwa kuendesha mauaji ya halaiki. Lakini pia alishtakiwa kwa kupora pesa za umma. Kiwango alichopora hakijulikani lakini anakisiwa kuiba kati ya dola bilioni 1 na bilioni 4. Aliaga dunia mwaka 2006 akiwa kwenye mahakama ya Hague.

Hosni Mubarak, Misri

_93772675_gettyimages-180523531.jpg
Alipinduliwa mwaka 2011. Hosni mubarak alishtakiwa kwa kuiba pesa zilizonuiwa kukarabati ikulu za rais na kuzitumia kujenga miradi yake binafsi. Mubarak na wanawe wa kiume walipatikana na hatia ya kuiba zaidi ya milioni dola 17 kati kipindi cha miaka minane. Alihukumiwa kifungi cha miaka mitatu jela huku wanawe wakihukumiwa kifungo cha miaka minne kila mmoja.

Ben Ali, Tunisia

_93773113_499d8038-2616-4f04-b44b-91ce3531cc2a.jpg
Mwaka 2011 wakati wa kupinduliwa kwa Ben Ali, yalianza mapinduzi ya nchi za kiarabu. Ali na mkewe walikimbia kwenda Saudi Arabia lakini mahakama ya Tunisia iliwahukumu bila ya wao kuwepo kifungo cha miaka 35 jela kwa kupora pesa za umma. Wakati wa kesi yao mwendesha mashataka alisema kuwa vito vya thamani ya dola milioni 27 na pesa vilipatikana ndani ya moja ya nyumba zake.

Kwa msaada wa BBC/Swahili
 
Usd mil.11 kwa rais ni wizi mdogo mno kwa kweli.Cheki Abacha hela aliyopiga
 
Back
Top Bottom