Viongozi wakuu watakubali kuzikwa DODOMA ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wakuu watakubali kuzikwa DODOMA ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Sep 6, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Viongozi wakuu wa nchi sasa kuzikwa Dodoma *wamo Rais,Makamu, Spika, Waziri Mkuu, Jaji MKuu Na Habel Chidawali, Dodoma

  VIONGOZI wa juu serikali akiwamo Rais, Makamu, waziri mkuu sasa wataanza kuzikwa katika eneo maalum la ekari 100 lililotengwa kwa ajili ya mazishi ya viongozi hao.

  Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkurugenzi Mkuu Ustawishaji Makao Makuu (CDA), Martin Kitila, jana zinaeleza kuwa viongozi wataanza kuzikwa katika eneo hilo baada ya kukamilika kwa maandalizi yake.

  Alisema viongozi wengine ambao watazikwa katika eneo hilo na wakuu wa mihili ya dola ambo ni Spika na bunge na Jaji Mkuu.

  Kitila hakuweza kufafanua mwisho wa mvutano wa Bunge katika pande mbili zinazopingana kuhusu rais wa Zanzibar kuzikwa eneo hilo.

  Mchakato wa kupata eneo hilo ulioanza miaka mingi iliyopita, ulilenga kuwa na eneo la pamoja kwa ajili ya mazishi ya viongozi wakuu wa nchi ili kutunza Kumbukumbu zao kwa ajili ya vizazi vijavyo.

  Kitila alisema CDA imetenga eneo hilo kwa kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu na kwamba kuanzia sasa viongozi hao kiongozi yoyote atakayekufa, atazikwa hapo badala ya sasa ambapo kila kiongozi anazikwa eneo lake.

  Viongozi wa juu wa serikali waliokufa mpaka sasa ambao wanastahili kuzikwa eneo hilo ni pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki Oktoba 14, 1999, na kuzikwa nyumbani kwa Butiama mkoani Mara, Waziri Mkuu Edward Soikoine aliyefariki Aprili 20, 1984 na kuzikwa nyumbani kwake Monduli Juu mkoani Arusha, Jaji Mkuu, Francis Nyalali.

  Wengine ni Spika wa Bunge, Adam Sapi Mkwawa,Makamu wa Rais, Dk Omar Ali Juma ambaye alizikwa nyumbani kwao Pemba.

  Kwa mujibu wa Kitila eneo hilo lililoko Chimwaga karibu na mipaka ya Chuo Kikuu cha Dodoma (DOM),liko chini ya Kitengo cha Maadhimisho kilichopo ofisi ya Waziri Mkuu.

  Alisema kazi iliyopo sasa ni kusafisha eneo hilo na kukamilisha mipaka yake baada ya kumalizika kwa michoro na ramani.

  "Eneo hilo liko tayari, lipo maeneo ya Chimwaga, kazi tuliyonayo sasa ni kulisafisha na kuweka mipaka vizuri kisha litakuwa chini ya ulinzi kwa hiyo sio kificho tena katika suala
  hilo," alisema Kitila.

  Eneo hilo ambalo kwa mujibu wa jiografia ya Mji wa Dodoma litakuwa kwenye
  miinuko ya upande wa Kusini mwa mji, limekuwa na tafsiri tofauti kwa wakazi wa mji huu.

  Baadhi ya wakazi wa mji huo waliozungumza na gazeti hili walihoji mantiki ya serikali kushindwa kuhamishia makao makuu ya Serikali Dodoma badala yake kuweka makao makuu ya makaburi ya viongozi wa serikali.

  Mmoja wa watu wanaopinga wazo la kuweka makaburi ya viongozi Dodoma ni Mbunge wa Kibakwe (CCM), George Simbachawene ambaye alihoji mantiki yake wakati serikali imeshindwa kuhamia Dodoma.

  Simbachawene ambaye ni mbunge kijana kuliko wabunge wote wa Mkoa wa Dodoma, kimsingi hakupinga kutengwa kwa eneo hilo isipokuwa alikosoa utaratibu wa kuharakisha makaburi badala ya kuharakisha makao makuu ya serikali kama ilivyopitishwa 1973.


  Kwa upande wake Balozi Mstaafu Job Lusinde alisema kuwa kutengwa kwa eneo hilo ni hatua moja ya kusonga mbele na kutekelezwa kwa baadhi ya mipango ya serikali katika kuifanya Dodoma kuwa makao makuu.


  Hata hivyo, alisema kuwa hatua hiyo imechelewa na kufanya maziko ya Baba wa Taifa yakafanyika katika kijiji cha Butiama mkoani Mara badala ya Dodoma ambako ndiko alikostahili kuzikwa kiongozi huyo wa kwanza wa Tanzania.

  "Mpango wa kutenga eneo hilo ni wa muda mrefu sana wala haukuanza leo na kama wangetenga mapema ni imani yangu kuwa hata Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere angezikwa hapa Dodoma" alisema Lusinde.

  Lusinde ambaye ni miongoni mwa Mawaziri wa kwanza katika serikali ya Tanganyika, alisema kuwa kutengwa kwa eneo hilo kusionekane kuwa ni jambo jipya kwani lilizungumzwa miaka mingi iliyopita.

  Kulingana na ramani ya CDA ambayo inachukua eneo lote la Manispaa ya Dodoma, eneo hilo kwa siku za usoni litakuwa katikati ya Mji umbali wa hatua chache kutoka zinapotarajiwa kujengwa ofisi mbalimbali Wizara na idara za serikali.
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Swala la sehemu ya kuzikwa mtu ni very personal.Vipi kama familia ina tradition ya kuzika kwao?

  Ni vizuri kuwa na hii sehemu, lakini apart from actually moving the government to Dodoma, itakuwa vizuri zaidi kama uamuzi wa mwisho aachiwe mtu mwenyewe na famila yake.

  Kama mimi tayari familia yetu ina sehemu ambapo wanandugu wote huzikwa, kwa nini niende kuzikwa Dodoma?
   
 3. Brutus

  Brutus Senior Member

  #3
  Sep 6, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wameamua kutengeneza " Arlington Cemetery" ya kibongo?
   
 4. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Tanzania imekuwepo kwa karibu miaka 50 bila makaburi haya. Sasa kuhangahika huku leo hii kwa faida gani? Ni kama kutengeneza ulaji ki namna
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Kunatakiwa kuwe na sehemu ya mashujaa na si viongozi wa siasa tu bali wanajeshi waliopigana kwa nchi yetu. Kuna mawaziri wakuu ambao hawastahili hii heshima kama walikuwa mafisadi.
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ni mambo mema tu yatakayomnusuru mwanadamu na adhabu ya mwenyezimungu. Uzikwe kwenye kaburi la zege, uzikwe kwenye jeneza la dhahabu, uzikwe eneo maalum la viongozi, uliwe na papa baharini au uliwe na simba na mabaki kumaliziwa na vultures, fisi, hii yote haina unafuu au ukali kwa mwanadamu. Unafuu unapatikana pale ulipokuwa hai ulifanya matendo gani ya kumpendeza mwenyezimungu wako?. Je ulitumia vizuri nafasi ya uongozi duniani (kama Khalifa) kwa manufaa ya wale uliokuwa unawaongoza?, je ulikuwa tayari kuua mtu ili ulinde maslahi yako ya utawala?, je ulitumia hila katika kukandamiza haki za watu ulipopewa nafasi ya kutoa haki?. Ulishirikiana na watu katika kukandamiza maisha ya watanzania kwa kujilimbikizia mali huku kina mama wajawazito wakifa kwa kukosa huduma, watoto wakifariki kwa kukosa lishe bora kutokana na hali duni ya maisha ya unaowaongoza huku wewe ukiwakandamiza na kuwahadaa kila wakati wa kupiga kura na ikibidi hata kuwadhulumu maamuzi yao kwa kujitangaza mshindi?, kumtangaza rafiki yako mshindi?

  Kama hayo yote viongozi wetu hawayazingatii, ninaamini hakuna atakayekuwa tayari kuzikwa eneo maalum maana litakuwa na vilio vya adhabu na litakuwa na joto kali kutokana na adhabu za kaburi watakazo kuwa wanazipata viongozi wengi kama si wote waliozikwa eneo hilo.

  "Otherwise huu ni upuuzi mwingine wa kupoteza hela za walipa kodi na ardhi ambayo ingetengwa kwa kilimo ingesaidia wananchi". Kinachowatisha ni nini hasa? Ninakumbuka MAZISHI YA MAKAMU WA RAIS DR OMARI ALI JUMA KULE PEMBA, yaliwatia aibu wakubwa kwa jeneza kufunikwa kwa nguo chakavu, lakini mimi nilifurahi maana huenda huko alipo amekwepa adhabu ya kuwa mnafiki.
   
Loading...