Viongozi wakerwa na mwenendo wa Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wakerwa na mwenendo wa Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Aug 1, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,434
  Likes Received: 19,764
  Trophy Points: 280
  Mzindakaya: Bunge losing direction

  Sunday, 31 July 2011

  [​IMG]
  The Citizen Reporter

  MPs should strive to strengthen national unity irrespectuve of political leanings, longtime CCM member Chrisant Mzindakaya said yesterday.

  In so doing, the National Assembly will remain focused, he said, warning that Parliament had lost its authority.
  Mr Mzindakaya also urged CCM MPs to stop confrontational politics with opposition parties and instead concentrate on implementing their party's election manifesto.

  Mr Mzindakaya, who served as a Kwela MP for decades, told a news conference that failure to implement the CCM Election Manifesto could make the MPs lose their seats in the 2015 polls.Apart from politics, Mr Mzindakaya also served as a minister and regional commissioner.

  "Tanzania is now a leading country in the world when it comes to noisy politics while its economy is reeling," noted Mr Mzindakaya, who is also the National Development Corporation (NDC) board chairman."It's a shame and annoying to see such antics taking place in the august House," he said.

  Recently, four Chadema MPs were thrown out of the House for allegedly violating Parliamentary Standing Orders. Booing, heckling and talking back to the Speaker or session chairs have become commonplace in the House.

  "The integrity of a person is not about academic qualifications but his or her acts. We have many educated MPs now than ever before, but their conduct raises more questions than answers…Let our MPs act courteously and not thuggishly," he cautioned. He called on poorly performing ministers to step down because they are accountable for their mistakes of those committed by their subordinates.

  He also said CCM members who were habouring the ambition to succeed President Jakaya Kikwete in the 2015 General Election should hold their horses and concentrate on implementing their party's manifesto first. He asked the government to heed advice of former leaders.

  "It's shocking to see a ward or district leader is opposing a statement by a former president or a prime minister. This is indiscipline."He proposed that a body be set up to enable retired leaders to have a forum of advising the government.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Idd Simba aitabiria kifo CCM

  • Akerwa na malumbano ndani ya Bunge

  na Waandishi wetu


  MWANASIASA mkongwe nchini, Idd Simba, amekitabiria kifo Chama cha Mapinduzi (CCM) endapo hakitachukua hatua za haraka kudhibiti makundi yaliyo ndani yake ambayo mengi yanatokana na baadhi wanachama kuanza mapema mbio za kukimbilia Ikulu wakitaka urais.

  Idd Simba, mwenyekiti wa baraza la wazee wa mkoa wa Dar es Salaam alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kufungua semina ya maimamu na wanazuoni wa Kiislamu, iliyofanyika katika hoteli ya Starlight, Dar es Salaam.

  Alisema makundi yaliyojengeka ndani ya CCM yamesababisha chama hicho kupoteza kuaminika na wananchi hali ambayo inahatarisha amani nchini.

  Alisema kutokana na hali hiyo moja ya mkakati wa kwanza wa baraza la wazee wa mkoa wa Dar es Salaam ni kuhakikisha linadhibiti hali hiyo ili kuweka mazingira mazuri ndani ya CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.


  Pamoja na mambo mengine, aliwaonya wanachama wanaojiundia makundi ya mtandao kwa kuelekeza nguvu zao za kuelekea Ikulu badala ya kukisaidia chama kuwa imara mbele ya wananchi.


  "Kupoteza mwelekeo kwa chama chetu kunatokana na makundi ya watu ambao wana nia ya kukimbilia Ikulu na hali hii sisi wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na wenzetu nchi nzima tumejipanga kuthibiti hali hii.


  "Kila anayesema hivi sasa anamtolea mfano Mwalimu Nyerere, sasa hayupo nani anayeendeleza na kukienzi chama kama ilivyokuwa wakati wake? Ili kuondokana na tabaka hili sisi wazee tunajipanga kukishauri chama kama kunatokea matatizo kama ilivyo sasa wazee tuweze kushauri kwa maslahi ya chama na wanachama kwa ujumla pamoja na kujenga misingi imara ya uzalendo na siasa zilizotukuka ndani na nje ya CCM," alisema Simba ambaye amepata kuwa waziri katika serikali ya awamu ya tatu.


  Alisema ili kujenga misingi imara lazima siasa ndani ya CCM, zijengwe na watu hasa kwa kuongozwa na itikadi kama aliivyokuwa ikisimamiwa na Mwalimu Nyerere na wasaidizi wake.

  "Sisi wazee na wanachama wote wa CCM tusiposimama imara kuna hatari ya chama kupoteza mwekelekeo; sasa juhudi zinazofanywa za kurudisha misingi ya chama na mwenyekiti wa taifa, Rais Jakaya Kikwete, na sekretarieti tunahitaji kusimamia na kukomesha makundi yanayokitafuna chama ndani," alisema Simba.


  Hali ya kisiasa nchini


  Akizungumzia mwenendo wa kisiasa alisema hivi sasa amani imekuwa ikivurugwa na vyama vya siasa kutokana na kila chama kutanguliza utashi na maslahi ya chma husika kuliko wananchi na taifa kwa ujumla.

  Alisema malumbano yanayotokea mara kwa mara bungeni, siku moja yanaweza kuwaingiza wananchi barabarani kwa kuhisi wawakilishi waliowachagua hawana tija kwao.


  "Haya yanayoendelea hivi sasa bungeni ni ya kusikitisha sana kwani hivi sasa muhimili muhimu wa Bunge unayumba na hata kukosa mwelekeo kutokana na baadhi ya wabunge kuona pale ni jukwaa la kisiasa.

  "Huwezi ukawa na wabunge wenye kuonyesha ufundi wa kuzungumza na kila mara mwongozo wa Spika au taarifa wakati hivi sasa Watanzania wanahitaji kutatuliwa matatizo yao na watunga sheria hao," alisema mwenyekiti huyo wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.


  Amani ya nchi


  Kuhusu suala hilo, Simba ambaye alikuwa waziri katika utawala wa awamu ya tatu kisha baadaye kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Taifa, alisema hivi sasa amani ya nchi iko shakani kutokana na kauli za viongozi wa vyama vya siasa wanazozitoa katika Bunge na mikutano yao ya kisiasa.

  "Kila mbunge au kiongozi ametanguliza maslahi yake binafsi kwa kugombea vyeo vya uwakilishi na kulumbana kupitia Bunge kuliko watu waliomchagua huku akisahau lilolompeleka pale, kwa hatua hii kuna kila dalili za kuchafua amani yetu," alisema Simba.  CCK yasikitishwa na Bunge

  Katika hatua nyingine, Chama cha Kijamii (CCK), kimesema Bunge limepoteza heshima kutokana na wabunge kusimama kutetea maslahi ya vyama vyao na kusahau wananchi ambao walichagua serikali yao kukaa madarakani.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi, alisema kuwa kupoteza heshima kwa Bunge kumetokana na wabunge kuwakilisha vyama na kuacha wananchi wakiwa hawana imani na serikali yao katika kupata maisha bora.

  Alilaani wabunge kutohudhuria kwa wingi bungeni hali inayosababisha wabunge wanaopitisha bajeti kuwa wachache hivyo kuwafanya wananchi wengi kukosa kuwakilishwa ipasavyo.


  Dowuta yatoa tamko


  Wakati huo huo, Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA) kimesema Buge la sasa limekosa dira na kutokana na hali hiyo kuna haja ya kuwepo kwa chuo kinachofundisha uongozi kabla ya watu hao kuteuliwa katika nafasi za uongozi.

  Akizungumza na Tanzania Daima, ofisini kwake mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu wa Dowuta, Abdallah Kibunda, alisema Bunge la sasa linatia aibu machoni mwa jamii hivyo kulifanya kukosa dira.


  "Bunge la sasa ni la ghasia tu, wabunge wamejisahau kwani badala ya kujadili masuala ya maendeleo wanalumbana bila mpango wakati malumbano yalishaisha wakati wa kampeni.

  "Hao ni wawakilishi wa wananchi hivyo hawana budi kujirekebisha. Hata hivyo suala la uongozi linahitaji taaluma na kungekuwa na chuo ambacho moja ya sifa ni viongozi wakiwemo mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa na wengine kupitia huko kabla hawajateuliwa ingekuwa vizuri," alisema Kibunda.


  Alisema malumbano hayo hayawanufaishi wapigakura kwani asilimia kubwa ya wapigakura si wanachama wa CCM, CHADEMA, CUF wala TLP bali waliwapigia kura wabunge hao kutokana na kunadi sera zao kwao wakitegemea watapata maendeleo lakini kinyume chake wabunge hao wamekuwa wakilumbana siku hadi siku badala ya kupaza sauti zao bungeni kusaidia kuondoa kero za wananchi.


  Alisema kwa hali hiyo wabunge hawana budi kurekebisha mara moja tabia hiyo kabla haijaleta athari zaidi.


  Kwa mujibu wa katibu huyo, mkutano huo wa Bunge ni muhimu kwa sababu unajadili maendeleo ya taifa yakiwemo ya wafanyakazi katika kukuza uchumi wa taifa ili kukuza uchumi.


  Alisema badala ya wabunge hao kujadili matatizo ya wafanyakazi kama vile mazingira mabovu ya kazi waliyonayo, kukatwa kodi na mengine badala yake kila mtu anafanya jambo analojisikia.

  Alitoa rai kwa wabunge kufanya kazi kwa hekima, umakini na busara wawapo bungeni kwa maslai ya taifa.
   
 3. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Hawa wote ni wanafiki tu wanalizunguka tatizo wanagenelorize lawama badala ya kusema ukweli kwamba hakuna usawa wa maamuzi,na hii inafanywa na maspika wote kuipendelea CCM wazi wazi wakati hili ni bunge la vyama vingi.
   
 4. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ah! kumbe ni yale matapishi ya jana na juzi, to hell.
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,052
  Likes Received: 3,082
  Trophy Points: 280
  sasa mbona hawamshauri raisi kupitia chama chao wamrudishe mzee wa standard na speed ama bado hawajauona uchi uliwazi kabisa wa kiti kuwa wazi...anyway twende hvyohvyo ili CCM ife kama 'kinyonga'
   
 6. m

  manengero Member

  #6
  Aug 1, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MWANASIASA mkongwe nchini, Idd Simba, amekitabiria kifo Chama cha Mapinduzi (CCM) endapo hakitachukua hatua za haraka kudhibiti makundi yaliyo ndani yake ambayo mengi yanatokana na baadhi wanachama kuanza mapema mbio za kukimbilia Ikulu wakitaka urais.
  Idd Simba, mwenyekiti wa baraza la wazee wa mkoa wa Dar es Salaam alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kufungua semina ya maimamu na wanazuoni wa Kiislamu, iliyofanyika katika hoteli ya Starlight, Dar es Salaam.
  Alisema makundi yaliyojengeka ndani ya CCM yamesababisha chama hicho kupoteza kuaminika na wananchi hali ambayo inahatarisha amani nchini.
  Alisema kutokana na hali hiyo moja ya mkakati wa kwanza wa baraza la wazee wa mkoa wa Dar es Salaam ni kuhakikisha linadhibiti hali hiyo ili kuweka mazingira mazuri ndani ya CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
  Pamoja na mambo mengine, aliwaonya wanachama wanaojiundia makundi ya mtandao kwa kuelekeza nguvu zao za kuelekea Ikulu badala ya kukisaidia chama kuwa imara mbele ya wananchi.
  “Kupoteza mwelekeo kwa chama chetu kunatokana na makundi ya watu ambao wana nia ya kukimbilia Ikulu na hali hii sisi wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na wenzetu nchi nzima tumejipanga kuthibiti hali hii.
  “Kila anayesema hivi sasa anamtolea mfano Mwalimu Nyerere, sasa hayupo nani anayeendeleza na kukienzi chama kama ilivyokuwa wakati wake? Ili kuondokana na tabaka hili sisi wazee tunajipanga kukishauri chama kama kunatokea matatizo kama ilivyo sasa wazee tuweze kushauri kwa maslahi ya chama na wanachama kwa ujumla pamoja na kujenga misingi imara ya uzalendo na siasa zilizotukuka ndani na nje ya CCM,” alisema Simba ambaye amepata kuwa waziri katika serikali ya awamu ya tatu.
  Alisema ili kujenga misingi imara lazima siasa ndani ya CCM, zijengwe na watu hasa kwa kuongozwa na itikadi kama aliivyokuwa ikisimamiwa na Mwalimu Nyerere na wasaidizi wake.
  “Sisi wazee na wanachama wote wa CCM tusiposimama imara kuna hatari ya chama kupoteza mwekelekeo; sasa juhudi zinazofanywa za kurudisha misingi ya chama na mwenyekiti wa taifa, Rais Jakaya Kikwete, na sekretarieti tunahitaji kusimamia na kukomesha makundi yanayokitafuna chama ndani,” alisema Simba.
  Hali ya kisiasa nchini
  Akizungumzia mwenendo wa kisiasa alisema hivi sasa amani imekuwa ikivurugwa na vyama vya siasa kutokana na kila chama kutanguliza utashi na maslahi ya chma husika kuliko wananchi na taifa kwa ujumla.
  Alisema malumbano yanayotokea mara kwa mara bungeni, siku moja yanaweza kuwaingiza wananchi barabarani kwa kuhisi wawakilishi waliowachagua hawana tija kwao.
  “Haya yanayoendelea hivi sasa bungeni ni ya kusikitisha sana kwani hivi sasa muhimili muhimu wa Bunge unayumba na hata kukosa mwelekeo kutokana na baadhi ya wabunge kuona pale ni jukwaa la kisiasa.
  “Huwezi ukawa na wabunge wenye kuonyesha ufundi wa kuzungumza na kila mara mwongozo wa Spika au taarifa wakati hivi sasa Watanzania wanahitaji kutatuliwa matatizo yao na watunga sheria hao,” alisema mwenyekiti huyo wa wazee wa mkoa wa Dar es Salaam.
  Amani ya nchi
  Kuhusu suala hilo, Simba ambaye alikuwa waziri katika utawala wa awamu ya tatu kisha baadaye kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Taifa, alisema hivi sasa amani ya nchi iko shakani kutokana na kauli za viongozi wa vyama vya siasa wanazozitoa katika Bunge na mikutano yao ya kisiasa.
  “Kila mbunge au kiongozi ametanguliza maslahi yake binafsi kwa kugombea vyeo vya uwakilishi na kulumbana kupitia Bunge kuliko watu waliomchagua huku akisahau lilolompeleka pale, kwa hatua hii kuna kila dalili za kuchafua amani yetu,” alisema Simba.

  Source : Tanzania daima
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  washapitwa na wakati hao. wakati wapo bungeni walifanya nini cha maana?
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  The two guys have things in common Simba is the guy behind the American company grabbing thousands of acres in Mpanda. On the other hand Mzindakaya has accumulated thousands of acres in Sumbawanga.

  Sasa kwa vile wako secure hawapendi kusikia kelele za wazalendo kudai haki zao, kwani zikisika watakosa ulaji
   
 9. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wakawaulize wanchi walio piga kura Bunge hili ndilo linalo faaaa au hapana maana mtu anaambiwa ukweli wake sasa unataka ustaarabu wa wapi kama wewe kiongozi wa serikali hutekelezi uricho kihaidi unategemea nini ustaarabu kwanza uanze serikalini kwa kutekeleza mambo yote kwenye ilani zenu kwani hamkujua hili ndilo au silo
   
 10. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mheshimiwa spika naunga mkono hoja 100%, ila jimboni kwangu hali ni mbaya..kidumu chama
   
 11. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Wale wote wanaosema bunge la sasa limekosa ustaarabu wanapendelea mabunge ya kizamani ya ndio mzee yaliyoingiza hii nchi katika tope la umaskini wa kutupwa. Sasa wameingia vijana wasiopenda upuuzi wa kuunga mkono hoja asilimia mia na wanaexpose madudu yanayaofanywa na serilkali, wakikosa hoja za kujibu wanasingizia ustaarabu. Ustaarabu gani wanahitaji wakati nchi imechoka hivi......
   
Loading...