Wakuu nimeona mantiki ya baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani Zanzibar wakihoji uhalali wa vyama viwili tuu Cuf na ccm kukaa na kujadili masuala yanayowahusu wazanzibar wote ili hali kuna vyama vingine. sijaelewa mpaka leo kwa nini cuf wamejimilikisha uhalali wa kuwa mpinzani pekee , monopolize. ni kwa nini ?? tunadhani mazungumzo yoyote ya mustakabali wa nchi yahusishe vyama vyote , no matter what. vyama amkeni, zindukeni mshirikishwe kwani wao cuf wana uhalali gani wa maamuzi ya nchi peke yao. tafakarini na chukueni hatua