Omulangi
JF-Expert Member
- Feb 12, 2008
- 1,036
- 267
Naona kwa hali zinazoendelea nchini, ingekuwa vema viongozi wa dini kwa ajili ya amani ya taifa watengeneze jukwaa la kutetea haki. Kwa mwendelezo misuguano ya kisiasa uliopo na matumizi ya vyombo vya dola; ikiwa viongozi wa dini hawatoi sauti ya kinabii dhidi ya lolote lililo kinyume na haki amani inaweza kutoweka. Nashauri viongozi wa dini waje pamoja na kuangalia kwa haki michakato mbali mbali inayoendelea kama uchaguzi wa Zanzibar, umeya katika majiji, manispaa na halmashauri zinazobishaniwa sana na kisha wazungumze na viongozi wa kisiasa na wa kiserkali juu ya njia sahihi za kumaliza shida hizi.
Ikiwa hatua kama hizi hazichukuliwi mapema na bila upendeleo au woga yafuatayo yanaweza kutokea:-
1. Viongozi hawa watakuwa wamesaliti wito wao wa kuisaidia jamii kuishi kwa amani na katika haki.
2. Mambo yakiharibika watakuwa hawana tena uhalali wa kujaribu kuongea au kusuluhisha au kushauri.
3. Siku moja watatoa hesabu mbele za Mungu asiyekuwa na chama, wala upendeleo jinsi walivyo compromise (walivyojichanganya) katika wajibu wao.
4. Viongozi wetu wa kisiasa na kiserkali ambao ni waumini wao, watakuwa si wakulaumiwa kwa vile hawakupewa mwongozo sahihi wakati walipokuwa wanauhitaji sana.
Mambo huharibika pale wale waliopewa jukumu na Mungu kutunza ustawi wa jamii husika wanapoacha kufanya wajibu wao.