DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Viongozi wa dini wametakiwa kuendelea kuelimisha na kusisitiza umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii hasa kwa vijana ili kuhakikisha inatumiwa katika maslahi ya maendeleo ya Taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa jeshi la Polisi David Misime wakati wa Mkutano Mkuu wa 54 wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania uliofanyika Kitonga jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kukiwa na matumizi mazuri ya mitandao kutaboresha familia na kuondoa athari za mmomonyoko wa maadili unaosababishwa na baadhi ya watu kutumia mitandao vibaya.
Aidha Misime amesema viongozi hao wanapaswa pia kuendelea kuhubiri Amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Pia Soma: GE2025 - Vijana JKT wahimizwa kutoa elimu ya Matumizi bora ya Mitandao ya kijamii wakati wa uchaguzi