JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Salamu wanabodi!
Awali ya yote ningependa nijiweke wazi kiimani, mimi ni mkristo lakini kuna jambo moja huwa linanikwaza sana na huwa nakwazika zaidi linapo tamkwa na kiongozi ambaye zamani nilikuwa namuamini kama ni role model wangu kiimani.
Alipo chaguliwa Jakaya Mrisho Kikwete kuna kiongozi mmoja alitamka hadharani kuwa alikuwa CHAGUO LA MUNGU.Binafsi nilitafakari sana na kuona pengine ilikuwa ni mapema mno kusema hivyo, binadamu hawakawii kubadilka kama popo!
Tena baada ya John Joseph Pombe Magufuli kuchaguliwa tena wengine wakajitokeza na kusema wameona utukufu wa Mungu hakika yeye ni CHAGUO LA MUNGU.Mwanzoni na mimi niliamini nikasema Mungu huyu kwanini katuficha vile? Kaacha watu tumedeki barabara, tumekesha uwanja wa ndege kumsubiri Lowassa, kumbe yeye alkuwa na chaguo lake na kamwe hakutufunulia! Alipo ingia madarakani nikasema naam, yawezekana kweli Mungu katusikia!
Lakini mkiezi sita baadae, tena nimeshikwa na mashaka tena kuliko wakati mwingine wowote.polisi wamenyakua madaraka wao ndio kila kitu! mikutano ya kisiasa wamebinafsisha imekuwa ni haki ya chama kimoja.wanafunzi wanafukuzwa chuo kama wameingia kiujanja kumbe ni wao serikali waliwashawishi kuwa waende wakasome special program, wakihitimu wanaajiriwa moja kwa moja, lengo likiwa ni kupunguza uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi.Wamefukuzwa na kuitwa vilaza.wamewapotezea vijana muda wao!
Wafanyakazi wa serikali wanafukuzwa kama paka shume tena hadharani.Sheria,taratibu na kanuni zote zimewekwa kando.Siku hizi ukisikia kiongozi mkubwa anakuja eneo lako la kazi ni lazima ukae karibu na Daktari bingwa maana muda wowote unatumbuliwa bila kujali umewahi kuifanyia srikali mambo mema. Hakuna mwenye hamu na hao viongozi! hata wakiwa na shida namna gani hawathubutu kuwaalika, labda waje wenyewe.
Kizungumkuti kikubwa ni huko kwa watunga sheria. Aliye pewa rungu utadhani kaambiwa na nguvu yenye mamlaka ya ki Mungu kuwa akikosea mtu wa upinzani japo kidogo, toa adhabu kali sana, na kwa kweli anatekeleza kwa nguvu zake zote
Ninacho jiuliza mimi ni kwamba,Je Mungu huyu wa Ibrahimu, wa Yakoba , huyu mwenye huruma na upendo wa ajabu, anaweza kuleta CHAGUO LAKE halafu mtu huyo asiwe na huruma? Kwanini upige watu mabomo wakati wanafanya mikutano ya ndani?Kwanini kuwajaza watu hofu?
Viongozi wa dini mtuongoze vizuri na msikimbilie kusema fulani ni chaguo la Mungu.Walio wake Mungu utawajua tu na kamwe hawafanani na hawa tunao waona.