Viongozi wa dini msikubali kunyamazia uonevu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini msikubali kunyamazia uonevu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtaka Haki, Feb 7, 2011.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa kisiasa wamejaribu kila wawezalo kuwanyamazisha viongozi wa dini hasa pale wanapokemea au kukosoa vitendo vya kidhalimu. Mara wamesemakana kuanzisha udini na kadhalika. Mara nyingi wameshauriwa kutokuonyesha kuegemea upande wowote. Lakini wakati kuna uonevu wa lolote au kuna lolote lisilo haki kwamba linatendwa na viongozi wa serikali au vyama vya siasa basi ni wajibu wa viongozi wa dini kusimamia misingi ya haki bila kujali mkosaji ni nani?

  Dr. Desmond Tutu aliwahi kusema hivi.

  "If you are neutral in situations of injustice, you have chosen the side of the oppressor. If an elephant has its foot on the tail of a mouse and you say that you are neutral, the mouse will not appreciate your neutrality."

  Archbishop Desmond Tutu.
  TAFSIRI ISIYO RASMI:
  Kama ukisema huna upande katika uonevu, basi umechagua upande wa muoneaji. Kama tembo ataweka mguu wake juu ya mkia wa panya halafu wewe ukasema hauna upande , basi panya hatafurahia kutokuwa kwako na upande.

  Nawasilisha kwenu viongozi wa dini na wale wote mnaowalaumu kwa kukemee uonevu.
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kuwa CCM imewanunua baadhi ya viungozi wa dini moja , hivyo wakisimama viungozi wa dini ya kikristo kukemea maovu ya watawala, haraka haraka watajibiwa na BAADHI ya viongozi wa kiislamu, viongozi hawa wamejipa kazi ya kuwa wasemaji wa CCM na serikali yake. Na sababu wanayotoa ni kuwa viongozi wa kikristo wanaiandama serikali kwa sababun rais ni muislamu.Mtego huu uliotegwa na MAFISADI umewanasa baadhi ya viongozi wa kiislamu hivyo kufanya kazi ya ukombozi wa taifa letu toka kwa wakoloni weusi kuwa ngumu.Na huu ni ubunifu wa JK WAGAWE UWATAWALE MILELE.
   
 3. A

  Adaha Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtume Mohamedi wakati akieneza ujumbe wa MUNGU kwa watu waliokusudiwa alipata wafuasi wengi.Viongozi wa serikali na wanasiasa hawakufurahishwa na hili na wakapanga kumuua. Mungu alimwezesha kukimbia kifo.

  Yesu Kristo hali kadhalika hakupendwa na viongozi wa kiserikali na walimuua.

  Viongozi wa kiserikali hasa waarabu waliona ni rahisi kuitumia duni kama sehemu ya serikali ili kuwapumbaza watu. Dini ya kiislamu ni kitu adimu na haiwezi kuwa sehemu tu ndogo katika serikali. ukitaka inchi iongozwe kidini basi SHEIKH mkuu ndiye atakaye kuwa na mamlaka makubwa kuliko mtu yeyote na maamuzi haya yatafanywa toka msikiti mkuu na si ikulu. Angalia Vatican inavyotawaliwa. Mwenye mamla ya mwisho ni Baba mtakatifu. Kule mambo ni shwari.

  Sasa sehemu nyingi zinazotawaliwa kiislamu kwa kuufanya uislamu kama sehemu ndogo ya serikali wameshituka na wanataka demokrasi. Ukitaka demokrasi maanake unataka kutenganisha dini na Serikali.

  Hayati baba wa taifa alisema "Serikali ya Tanzania haina dini ila watu wake wana dini"

  Haya maneno aliyatoa katika vitabu vitakatifu. Yesu alisema yaliyo ya Mungu mpe Mungu na yaliyo ya Kaisari mpe Kaisari. Pia alisema ufalme wake siyo wa DUNIA hii.
   
 4. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naamini katika kila dini kuna watu wafuasi wa kweli wa Mungu ambao kwao uonevu haupiti bila hukemewa.
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo unakubaliana na "matamko ya viongozi wa Kiislam na Kikristo"

  If that is the case then good move.
   
 6. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nina maana kuwa kati ya makundi yote ya dini sio wote wanaoweza kununuliwa. Penye ukweli uongo hujitenga.
   
 7. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unaweza kuona tena TEMBO AMEWEKA MGUU WAKE JUU YA MKIA WA PANYA. Kanuni zinageuzwa ili kuthibiti wanaotaka kuithibiti serikali. Bado viongozi wa wanaharakati na wadau wengine mnanyamaza?
   
 8. P

  Paul S.S Verified User

  #8
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kila nchi inaustaarabu na tamaduni zake, leo hii usa kwenyewe kuwa muislam ni issue kuwa rais, england kanisa ni sehemu ya uongozi.
  Maana yangu ni kuwa kwakuwa tutu katamka ya kisiasa nchini kwake hayo ni mazingira ya kwao kama ilivyokuwa ngumu kuingiza utawaa na kanisa hapa bongo kama uk, au tuwe kama usa au iran nk
  Ni wajibu wa watu kujua mazingira na misingi iliyotumika kutufikisha, hapa tulipo.
  Leo hii hatuwezi kuruhusu viongozi wa dini kuwa mahakimu wetu wa kuanza na kugeuka kuwa kama masignatory wanao endorse huyu si meya halali hatumtambui kesho watesema huyu si mbunge halali hatumtambui, wao ni kina nani?
  Kwani dini ni nini, ni wangapi wanaamini hayo mapokeo ya dini na kudhani ndio sahihi kwa kuokoa jamii, kama dini zenyewe ndio hizi za kukatana mikono na kuua wanaokuwa against na wewe hata kwa kuchinja, kama dini zenyewe ndio hizi za kuwalawiti watoto wadogo na kuleta mafunfisho ya wizi wizi na kutapeli watu kwa majina matamu ya nabii,mtume,askofu nk, basi nasema wewe umepotoka
  Viongozi wa dini wanajukwaa lao la kusafisha waumini wao madhabahuni kama wameshindwa huko wasikimbilie ktk siasa.
  Leo hii kanisa rwanda ni sehemu kubwa wa yaliyotokea na kisingizio ilikua ni kujifanya dini haiwezi kukaa kimya katika mambo ya siasa.
  Tafakari kwa kina utapatamajibu
   
 9. P

  Paul S.S Verified User

  #9
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu mimi ni mkristo, lakini hapo umeuliza swali lenye manti nzito sana kwa mtu muelewa, je tukubaliane na matamko ya dini na madhehebu yote? maana isie onakana matamko fulani tu ndio sahihi, mind that kunamadhebu kama ya akina kibwetere nao ni dini.
  I real hate this shit kuchanganya siasa na dini
   
 10. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Suala hapa sio kuhubiri dini au siasa. Suala alilosema Tutu halihitajii kuwa katika eneo fulani la kijiografia ili uone ukweli huo. Huwa hakuna ukweli wa eneo fulani na eneo jingine. Hapa anachosema ni kuwa ukiona uonevu kisha ukaunyamazia basi unakubaliana na huo uonevu na pia ukiona mtu anaonewa na husemi chochote, basi yule anayeonewa hawezi kufurahia kuwepo kwako au kushuhudia kwako. Kuhusu viongozi wa dini kutokuzungumzia maslahi ya nchi yao kwa kisingizio cha kuwa wahubiri wa dini liliwahi kujibiwa.
  Jibu lilikuwa " Endapo wote tunasafiri katika boti na mara mmoja wetu akaaza kutoboa boti, kisha msafiri mmoja ambaye sio nahodha akapiga kelele, Acha Acha, kisha anayetoboa anasema It's none of your business, ( Haikuhusu nyamaza).
  Je utanyamaza kwa kuwa anakuambia nyamaza? Yaliyotokea Rwanda yalisababishwa na viongozi wa dini waliounga mkono matendo ya uonevu na yasiyo ya haki kama ambavyo hapa Tanzania wako wanaounga mkono viongozi wa kisiasa kwa kila wanachofanya hata pale ambapo ni UONEVU WA WAZI. Uonevu huchochea kuondoka kwa amani. Amani huzaliwa kwa matendo ya haki. Haki ikiondolewa
  AMANI INAKUWA IKICHEZEWA.
   
 11. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mnatoka nje na mada. Suala kuu hapa ni kupiga kelele pale ambapo tunaona uonevu. Viongozi wa dini ni mfano unaotumika kwa watu wa nje na siasa lakini walio viongozi kuwatia moyo kupiga kelele kwa uonevu. Haijalishi kelele inapigwa na nani. Kama ni kelele ya haki kila mtu ataiunga mkono. Hapa tuna maana kuwa hata kama ni mashirika yasiyo ya serikali au wanaharakati wanapaswa wapige kelele.
  Iko kama Tropical na Paulss ni ndugu waliokuwa pamoja au ni yuleyule?
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Hivi dini ni nini? ndio njia sahihi kwa kuishi?.
  Hivi kati ya tamko la maaskofu wa arusha na tamko la waislamu dar tufuate lipi? hivi inahitaji akili kiasi gani kujua jinsi hawa viongozi wa dini wanavyo tukanganya?
   
 13. P

  Paul S.S Verified User

  #13
  Feb 9, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu sawa unaposema kupiga kelele viongozi wa dini je tufate kelele za maaskofu wa arusha au tufuata za waislamu wa karmjee?.
  Huitaji akili ya ziada kujua hatari iliopo kuruhusu malumbano kama haya unayoyaita kelele za haki
   
 14. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huwezi kusema tufuate lipi. Haki hujitenga na uonevu. Kweli hujitenga na uongo.
  Tutafuata anayesema kweli bila kujali dini yake hata kama ni mwanaharakati. Ujumbe hapa ni kuwa Tembo kila mtu anajua ukubwa wake sasa wenye macho wakiona anamkanyaga panya halafu wanamsifia tembo kwa uhodari wake au wanawakemee wanaosema wewe tembo sio haki kukanyaga mkia wa panya, basi ujue kuna upungufu wa watu wanaoona haja ya kuhimiza haki katika JAMII.
  Kama tatizo ni kusema viongozi wa dini basi niseme jamii ya watanzania katika nyanja mbalimbali TUSINYAMAZIE UONEVU WA WAZI TUNAOSHUHUDIA KATIKA NCHI YETU.
  HAKI IKIENDELEA KUONDOLEWA NA UONEVU KUDUMISHWA AMANI ITATOWEKA. Watu hujichukulia sheria mikononi pale wanapokuwa na mashaka na utawala wa haki na sheria.
  TUHIMIZE HAKI
   
 15. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Viongozi wa dini kutoka madhebu tofauti nchini, wameshauriwa kuacha kuchanganya siasa na dini ili kuepusha uvunjifu wa amani katika makanisa na jamii wanayoihudumia.
  Wito huo ulitolewa jana na NABII wa kituo cha Sauti ya Uponyaji, Joshua Aram wakati wa maadhimisho ya miaka miwili ya kituo hicho kilichopo Kihonda Manispaa ya Morogoro. Arama alisema viongozi wengi wa dini hivi sasa wamekuwa wakitumia makanisa kuzungumzia masuala ya siasa na kusababisha mfarakano katika makanisa na jamii kwa ujumla.
  Pia aliwataka waumini wa makanisa hayo kutokubali kushirikishwa kwenye ugomvi wa kisiasa badala yake wawe na msimamo wa kiimani bila kushurutishwa na mtu yoyote.
  Mwananchi machi 18, 2011
   
 16. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  kama nchi inapelekwa kusiko viongozi wa dini hawana budi kukemea... na wala sio siasa kukemea viongozi waovu
   
Loading...