Viongozi wa dini acheni kuilaumu serikali-rc | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini acheni kuilaumu serikali-rc

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by politiki, Jan 2, 2012.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi, amewataka viongozi wa dini nchini kuacha kuilaumu serikali kuhusu ufisadi ambao unafanywa na viongozi, badala yake waiombee serikali isonge mbele.

  Alitoa kauli hiyo jana wakati wa kutoa salamu zake za mwaka mpya kwenye ibada iliyofanyika katika Kanisa la EAGT Siloam Ipagala mjini Dodoma.

  Dk. Rehema alisema viongozi wa dini nchini wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha wanaliombea taifa ili liwe na viongozi waadilifu na si kuendelea kuilaumu.

  Alisema viongozi wa serikali wanamilikiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi wa dini hivyo hakuna sababu yoyote ya kuwafumbia macho watumishi ambao siyo waaminifu na badala yake wanatakiwa kuwakemea.

  Alilitaka kanisa hilo kujenga tabia ya kujitegemea kwa kuwekeza katika kilimo na ufugaji ili kuondokana na tabia ya kuwa tegemezi.

  Naye Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Evance Lucas, aliitaka serikali kukemea baadhi ya viongozi wa siasa wanaohubiri udini na ukabila.

  “Sisi viongozi wa dini, hatutaki kusikia viongozi wa siasa wakihubiri masuala ya udini na ukabila kwa kufanya hivyo ni dalili za kutaka kuwapandikiza Watanzania tabia ambayo haikuwepo tangu kupatikana kwa Uhuru ambao ulitafutwa kwa hekima na busara za waasisi wa nchi,” alisema Mchungaji Evance.

  Alimtaka mkuu huyo wa mkoa kufikisha salamu za kanisa kwa viongozi wa kitaifa kuwa kanisa lina ushirikiano na vyama vyote vya siasa hivyo hakuna sababu yoyote ya kubagua na kuongeza kuwa yapo makanisa ambayo kwa sasa yanahubiri udini na ukabila.

  MCHAKATO WA KATIBA MPYA

  Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini Njombe, Issa Mengele, amewataka Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa Katiba mpya kwa kuyajumuisha makundi maalumu wakiwemo walemavu katika utoaji wa maoni.

  Wito huo ulitolewa jana wakati wa ibada maalum ya mwaka mpya iliyofanyika katika kanisa hilo Usharika wa Songea.

  Askofu Mengele alisema kila Mtanzania anayo haki ya kushiriki na kuijadili Katiba iliyopo ambayo kwa sasa imeonekana kuwa ina mapungufu mengi hivyo kila mwananchi ni vyema ashiriki kuchangia mchakato wa Katiba kwa kuyaainisha mambo muhimu ambayo yanapaswa kuongezwa.

  Alieleza kuwa Watanzania ni lazima wafahamu haki yao ya msingi kwa kuwa wawekezaji wa nje kwa muda mrefu wamekuwa wakijishughulisha na uchimbaji wa madini ambayo ni rasilimali kubwa ya nchi na kwamba iko haja sasa mambo hayo yakawekwa bayana kwenye Katiba mpya kwani katika maeneo mengi ambayo yana madini, wawekezaji wamekuwa wakichimba madini na kuondoka nayo huku wakiwaachia wenyeji mashimo.

  Imeandikwa na Godfrey Mushi, Iringa, Jacquelina Massano, Dodoma na Nathan Mtega, Songea.

  CHANZO: NIPASHE

  my take kwa mkuu wa mkoa.
  wananchi wakiwemo viongozi wa dini wanayo haki ya kikatiba ya kuikosoa serikali kutokana na record mbaya ktk swala zima la ufisadi unataka waendelee kuwaombea watu waovu bila kuwakemea hao waovu endelea na kazi yako ya kimla ya ukuu wa mkoa waache viongozi wa dini waendelee na kazi yao ya kukemea maovu.
   
Loading...