Viongozi wa ccm na wizi wa ardhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa ccm na wizi wa ardhi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by UPORAJI ARDHI, Sep 5, 2010.

 1. U

  UPORAJI ARDHI New Member

  #1
  Sep 5, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]MAALUM KWA WAKAZI WOTE WENYE KUMILIKI ARDHI NA NYUMBA PEMBEZONI MWA JIJI LA DAR ES SALAM NA MJIJI YOTE MIKUBWA. [/FONT]

  [FONT=&quot]Eneo lote la mkoa wa Dar es Salaam zamani lilikuwa na Vijiji vya Ujamaa 52, ambapo wananchiwalimiliki ardhi kimila. Katika miaka ya 1980 eneo lote la Jiji la dare s Salaam kama inavyoendelea kufanyika pia katika miji mingine mikubwa lilitangazwa kuwa chini ya mipango ya kuendelezwa. Chini ya mpango huu wananchi wakapoteza umiliki wa ardhi wa kimila na uwezowa kuitumia ardhi hiyo kwa uhuru kwa ajili ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kujiondolea umaskini.[/FONT]

  [FONT=&quot]Kutokana na kukithiri kwa ufisadi, mpango wa uendelezaji maeneo yaliyoko pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam na miji mingine ukawapatia madaraka makubwa sana Maafisa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi na Manispaa za Jiji hilo za Kinondoni, Temeke na Ilala; na hlamashauri za miji na wilaya. Hivyo wakaanza kuwanyanyasa wananchi na kuwapora ardhi waliyokuwa wakiimiliki. [/FONT]

  [FONT=&quot]Sambamaba na mipango yabuendelezaji wa miji, miradi ya uwekezaji kamam vile ya uchimbaji madini, kilimo, ujenzi n.k nayo ikatumika kuwanyanganya wananchi ardhi yao pasipo kuzingatia Sheria za Ardhi namba 4 na 5 za mwaka 1999, hususan haki ya wananchi wanyonge kulipwa fidia kwa bei ya soko. Watendajiwa Wizara ya Ardhi na hlamashaurui za miji na wilaya kwa kushirikina na wakuu wa mikoa, wilaya na watendaji mbali mbali wakashirikikatika ufujaji wa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ulipwaji wa fidia kwa wananchi. Hii ilipelekea kila palipo kuwa na miradi wa kuhamisha watu, wananchi kugeuka maskini zaidi kuliko walivyokuwa kabla na hivyo kuwepo migogoro mikubwa ya ardhi katika kila kona ya nchi hii. [/FONT]

  [FONT=&quot]Tegemeo kubwa la wananchi wanyonge dhidi ya njama hizi zakuwapokonya ardhi yao kwa kukiuka Katiba na Sheria za nchi lilikuwa katika viongozi mbali mbali wa kuchaguliwa k.m wabunge, madiwani, wenye viti wa mitaa n.k. Lakini kwa uchungu mkubwasana wananchi wengiwalipoteza ardhi, nyumba na makazi na mali zingine nyingi kutokana kusahmiri kwa Ufisadi miongioni mwa viongozi wa ngazi mbali mbali CCM. Tofauti na ilivyokuwa zamani si wabunge, madiwani, wala wenye viti wa mitaa waliotoa kero hizi za wananchi katika mikutano bunge, mabaraza ya madiwani au katika mikutano ya serikali za vijiji na mitaa.
  [/FONT]


  [FONT=&quot]Matokeo yake ni wananchi kunyang’anywa ardhi yao, kuvunjiwa nyumba za na kuharibiwa mali zao bila matukio hayo kuwasilishwa katika viakao vyopvyote licha ya vyombo vya habari kuripoti sana ukiukwaji huo wa Katiba, sheria na unyama wa kutisha. Kibaya ziadi vitendo hivi vilikiuka kabisa maudhui yaliyoma katika Ilani ya CCM ya 2005 na Sera mbali mbali za CCM za kuwawezesha wananchi kiuchumi. [/FONT]

  [FONT=&quot] Kufumba na kufumbua ardhi iliyokuwa ikimilikiwa na wananchi wanyonge na maskini katika maeneo yanayozunguka Jiji la Dar es Salaam na miji yote mikubwa ikaangukia mikononi mwa viongiozi wa Serikali CCM, watumishi wa Wizara ya Ardhi, Manispaa na Halmashauri za Miji na wilaya katika mtindo wakujilimbikizia idiadi kubwa ya viwanja qwalivyovipata kwabei chee kwakutumia nyadhifa zao. Baada ya kuhodhi viwanja hivi huviuza kwa bei za juu mno hivyo kuwanyonya wananchi wanaotaka kujenga nyumba. Mtindo mwingine uliotumiwa na viongiozi wa kupora ardhi za wananchi ni kumiliki hisa katika makampuni ya uwekezajiyaliyopatiwa ardhi iliyokuwaikimilkiwana wananchi.[/FONT]

  [FONT=&quot] Hivyo kwa kutumia nyadhifa zao viongozi wa CCM kwa kushirikiana na na watendaji wa serikali ya CCM wakafanikiwa kujipatia manufaa ya kiuchumi yanayotokana na kupanda kwa thamani kwa ardhi waliyowanyang’anya wananchi kwa hila, ujanja, vitisho, mabavu kwakutumia mitutu ya polisi n.k.[/FONT]

  [FONT=&quot]Kati ya 2006 hadi 2009 migogoro ya ardhi ilizizima nchi nzima wananchiwaklinyang’anywa ardhi yao kwa kuwa hiki kilikuwa kipindi cha uhamishaji wa ardhi kutoka kwa wananchi wanyonge kwenda kwa viongozi wa CCM na wanyonyaji wenzao kutoka nje ya nchi. Kutokea mwaka 2009 suala hilo limesitishwa ili kuwafanya wananchi wasahau machungu hayo kwa ajili ya uchaguzi wa 2010. Uporaji na wizi wa ardhi ya wananchi wanyonge vitarejewa tena mara tu baada ya uchaguzi kukamilisha miradi iliyosalia na viongozi wapya wa CCM waliochaguliwa pamoja na wanyonyaji wao wapya kupatiwa ardhi. [/FONT]

  [FONT=&quot]Hebu tupitie ahadi za CCM katika Ilani ya Uchaguzi ya 2005, Seraza CCM kuhusu Ardhi na Sheria za Ardhi namba 4 na 5 za mwaka 1999 vilivyopaswa kuzingatiwakwa makini na Serikali ya awamu ya nne ya Mhe Jakaya Kikwete iliyoongoza kati ya 2005hadi 2010. [/FONT]

  [FONT=&quot]iIani ya CCM ya mwaka 2005 ibara ya 8 inayatamka kuwa “……Jukumu la pili ni kuwashirikisha wananchi wote kwa njia ya uwezeshaji katika ujenzi wa uchumi na kuutokomeza umaskini”. Aidha ukurasa wa 61 na 62 pamoja na mambo mengine inatamka wazi wazi “……utekelezaji wa sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi itaepusha balaa la kuwa na jamii ambayo ina matajiri wachache walionacho na wananchi walio wengi wasio nacho”[/FONT]

  [FONT=&quot]Sera ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi iliyokuwa ikatamkwa katika Ilani ya CCM ya mwaka 2005 ni ile iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Mwaka 2004 nakuitwa “Sera ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi ya 2004” . Ambapo katika suala la Ardhi ibara 4.9.2-Tamko la Sera “Serikali itatumia ardhi kama njia ya kuwawezesha wananchi wake kushiriki kikamilifu kiuchumi. Lengo ni kusaidia wananchi watumie ardhi waliyo nayo ama kwa kujipatia hisa katika shughuli za uwekezaji huo au pato lenye kuwanufaisha kushiriki kikamilifu katika shughuli zingine za kiuchumi”. [/FONT]

  [FONT=&quot]Ibara ya 4.9.3.(ii) Mkakati wa utekelezaji wa tamko hilo, “Kutoa ardhi kwa wawekezaji wakubwa kwa shughuli mbali mbali za kiuchumi. Pale ambapo itabidi Wananchi wahamishwe ili kuwapisha wawekezaji wakubwa. Serikali itawasidia utaalamu wa kuingia katika makubaliano muafaka na wawekezaji kwa nia ya kuwanufaisha”. [/FONT]

  [FONT=&quot]SEHEMU YA PILI KIFUNGU CHA 3 (1) CHA SHERIA YA ARDHI NA 4 NA 5 ZA MWAKA 1999, kifungu hiki kinwataka wote wanaotekeleza madaraka, kutumia au kutafsiri sheria hii kuzingatia pamoja na mambo mengine kuwa:-[/FONT]

  [FONT=&quot]f) kwamba maslahi yoyote ya wananchi katika ardhi yana thamani, na kwamba thamani hiyo inazingatiwa wakati wote katika mapatano yoyote yanayoathiri maslahi ya wananchi katika ardhi.[/FONT]

  [FONT=&quot]g) kulipa fidia kamili, ya haki na kwa wakati kwa mtu yoyote anayepoteza maslahi yoyote katika ardhi.[/FONT]

  [FONT=&quot]Sheria ya Ardhi Namaba 4 ya 1999, Kifungu cha 179, Tangazo la Serikali Namba 78 la tarehe 4 Mei 2001 linatamka bayana katika ibara ya 3 kuwa fidia za ardhi na maendelezo yoyote vitazingatia bei ya soko. [/FONT]
  [FONT=&quot]Ibara ya 4 inaelekeza utaratibu wa kufikia “bei ya soko” kuwa ni kwa kuzingatia mauzo ya hivi karibuni ya ardhi au majengo katika eneo husika. Ibara ya 7 inatamka, kama ardhi au nyumba husika inatumika kwa shughuli za kujipatia kipato basi mhusika atalipwa fidia ya posho ya upotevu wa faida kwa kukokotoa faida ya mwezi kwa kipindi cha miezi 36.[/FONT]

  [FONT=&quot]Watanzania tusidanganyike bila ya kuwa na ardhi inayomilkiwa na wananchi wenyewe kihalali, maendeleo mengine yote yanayoahidiwa na CCM na mgombea wake Jakaya Kikwete kama vile Barabara, Meli, Viwanja vya ndege, Madaraja, Maji Safi n.k ni kazi bure. Maendeleo hayo yatawanufaisha wageni hususan kutoka nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki ikiwemo Kenye,Uganda, Rwanda Burundi n.k ambao viongozi wa CCM wanawauziwa viwanja na ardhi waliyowanyanganya wananchi kwa kasi ya kutisha.[/FONT]

  [FONT=&quot]Maswali ya kujiuliza:- [/FONT]

  [FONT=&quot](1) Kwa Ufisadi ulionyeshwa na viongozi wa kuchaguliwa wa CCM wakiwemo wabunge, madiwani n.k kushirikiana na watendaji wa Serikali kuwanyang’anya wananchi wanyonge ardhi yao,kuwabomolea nyumba na kuharibu malui zao bila ya huruma na untyama mwingimne wa kutisha; na kisha wakashirikia katika kujilimbikizia aradhi hiyo kwa mfumo wa kumilikim idadi kubwa ya viwanja. Je wananchi wakiwachagua tena kwa kishindo kama walivyofanya 2005 watakuwa salama kweli? [/FONT]

  [FONT=&quot](2) Kutokana na udhaifu mkubwa sana ulionyeshwa na viongozi wa kuchaguliwa CCM yaani wabunge, madiwani, wenye viti wa mitaa n.k kwa kushindwa kuzuia na kudhibiti uporwaji wa ardhi ya wananchi kwa fidia hafifu sana zisizozingatia Ilani ya CCM ya 2005, Sera za Ardhi za CCM na Sheria za Ardhi. Wananchi hawaoni kuwa ni hatari kubwa sana kuwajaza wabunge, madiwani na wenye viti wa mitaa kutoka CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010 na zingine zinazokuja. Kwakuwa inafahamika kuwa wagombe wengi wa CCM wamejitokeza kutokana na kuvutiwa na fursa za kujinufasisha zilizopo ndania ya CCM kwa kuwafanyia wananchi Ufisadi na ukweli kwamba viongoizi hawa wapya wametumia viwango vikubwa vya fedha ili kuprta uongozi na watahaitaji kurejesha fedha zao na kujilimbikizia mali hususan ardhi na viwanja kutoka kwa wananchi kaama walivyofanya wenzao waliopita? [/FONT]


  [FONT=&quot]SULUHISHO:-[/FONT]

  [FONT=&quot]Kwa kuwa wabunge, madiwani na wenye viti wa mitaa wa CCM walishindwa kuwasaidia wananchi wasinyanganywe ardhi yao; na pia walishindwa kusimamia utekelezwaj iwa Sheria za Ardhi, hususana za Sheria za kuwalipa wananchi fidia. Hakuna haja ya wananchi kuchagua tena wabunge, madiwani na wenyeviti wa mitaa kutoka CCM na badala yake wawachague kutoka vyama vya upinzani kwa nia ya kulinda umiliki wao ardhi na ustawi wa kiuchumi, kijamii na kujiondolea umaskini kwa kuwa tatizo la CCM sio sera wala Ilani ni kushindwa kuvisimamia ili wananchiwapate manufaa kama tulivyoona sera za Sheria za ardhi zilizopo.[/FONT]

  [FONT=&quot]Baada ya wabunge , madiwani na wenye viti wa mitaa kuingia madarakani kwa wingi wataleta chachu ya kusimamia vizuri ukusanyaji wa kodi, fedha a na mali za umma na rasli mali za taifa na maendeleo yanayoahidiwa na Jakaya Kikwete kwa kutumia fedha za Serikali yatapatikana maradufu. Ikiwa wananchi watashimndwa kutumia nafasi hii kuweka upinzani wakweli bungeni, katika mabaraza ya madiwani na katika vijiji na mitaa yetu watakuwa wamepoteza fursa muhimu ya kulinda haki yao ya kumiliki ardhi waliyo nayo na kupata maendeelo endelevu. [/FONT]
   
 2. U

  UPORAJI ARDHI New Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 3. U

  UPORAJI ARDHI New Member

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 4. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Kwa hakika ndugu umenena mamabo ya ukweli kabisa, tena aliyekuwa kinara wa wizi wa ardhi za wananchi Bibi Salome Sijaon aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi; mara tu baada ya kusataafu JK alimzawadia kuwa balozi wetu nchini Japan. Inadaiwa mama huyu aliwaagiza maafisa wa wizara hiyo kupima maeneo ya wananchi waliyoishi muda mrefu zaidi ya miaka 20 (Ishirini) maeneo ya Kigamboni na kuikabidhi NSSF kujenga housing project.

  Pia mwaka 2004 alivunja Sheria za Ardhi kwa kupima maeneo ya wananchi wanaoishi maeneo ya Mloganzila huko Kwembe na kuyakabidhi kwa Chuo Kishiriki cha Muhimbili pasipo wananchi hao kuwa wamearfifiwa wala kulipwa fidia yoyote. Baada ya kukipatia Chuo kumilikishwa ardhi hiyo kwa kupatiwa Hati miliki, ndipo mwaka 2010 Serikali ikawalipa fidia ndogo sana eti kwa madai ya walivamia ardhi ya Serikali; wakati ambapo ni Serikali hiyo hiyo iliyowahamishia eneo hilo mwaka 1979 wakati wa Operesheni Gezaulole.
   
Loading...