Viongozi wa Afrika na roho ngumu

Major

JF-Expert Member
Dec 20, 2007
1,865
2,453
Kwa wenzetu wazungu mtu akitajwa tu na Kashfa kidogo, anajuzulu, wako Very Clean.
Africa ni tofauti kabisa, that means, Viongozi wengi wa Africa wapo madarakani ili tu watafune kodi za Wananchi. Ndiyo maana ni vinganganizi haswa, wako tayari kuziingiza Nchi zao machafukoni ili mradi wahakikishe wanatafuna kodi zao milele

Nasikia hakuna kitu kitamu ktk nchi Kama kodi za Wananchi, wengine wako tayari hata kubadili katiba ya nchi kibabe ili mradi waendelee kutafuna kodi zao, Mfano wa Tanzania ni Bunge la katiba,yaani baada ya uchaguzi kuisha basi, Pesa zoote zilizotumika ktk bunge hili ni kodi za Wananchi lakini matokeo yote ya maamuzi ya Bunge hili kwa sasa ni kama yametupwa ktk dust bin

Ni Africa peke yake ambapo Kodi za wananchi hazitumiki kuwahuduma Wanachi Bali kuhudumia Viongozi, utakuta kiongozi tena wakawaida anatumia gari ya Mil 300. Unakuta karani tu wa ofisi ya Serikali anatumia gari ya mil 250.

Sijui ni Ushamba au ni kulewa kodi za wananchi, utakuta katikati ya mji Kama Dar tena mjini kiongozi anatumia gari kuubwa 4 wheel, utafikiri labda anaogopa kukwama ktk lami, wakati Waziri wa Nchi Tajiri Kama Japan anatumia baiskeli ktk mizunguko yake ya kawaida

Gari moja tu la kiongozi linaweza kununua tractor 10 kubwa mpya, Wagonjwa hawana vitanda Wajawazito wanajifungulia Sakafuni Wananchi hawana hata maji safi ya kunywa, walitegemea kodi wanayolipa ingerudi kuwahudumia kumbe kodi zao Viongozi wanatanua nazo. HILI HALIKUBALIKI.

Ndiyo maana kiongozi safi akituhumiwa tu, basi inatakiwa ajiuzulu. Kiongozi mtafuna kodi hata umtuhumu na Kesi ya mauaji hawezi kujiuzulu kamwe.. Inanisukuma kuamini Kuwa, Mungu alishaondoka Africa
 
Back
Top Bottom