Viongozi mnaotokea mkoa wa Morogoro mnatuangusha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi mnaotokea mkoa wa Morogoro mnatuangusha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkeshaji, Feb 13, 2012.

 1. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Najaribu kutafakari mwenendo mzima wa viongozi wetu kiuongozi na kiutendaji, napata maswali kadhaa bila majibu.
  Jicho langu leo linawachungulia wale wanaotokea mkoa wa Morogoro (si lazima wawe na asili ya huko kimakabila).

  1. Celina Ompeshi Kombani:

  Licha ya kuwa ni mbunge wa Ulanga Mashariki, pia ni Waziri wa Sheria na Katiba. Mojawapo ya mambo ambayo tunamkumbuka huyu mama ni wakati wa vuguvugu la kudai katiba mpya, ambapo bila aibu alijitokeza hadharani na kusema kuwa hatuna haja ya katiba mpya kwani iliyopo bado ni nzuri sana. Alikuja kuaibika siku chache baadaye wakati Rais alipotangaza nia ya kuanza mchakato wa katiba mpya.

  Inasemekana jimboni kwake hajaonekana tangu alipopata ubunge na wananchi wake wako katika hali mbaya sana kwa kukosa huduma muhimu, ambazo yeye aliwaahidi kuwatumikia pindi wangemchagua.

  Anatuhumuwa kushirikiana na Abdul Mteketa kuchakachua kura katika jimbo la Kilombero zilizomwezesha ndg. Mteketa kutangazwa mshindi wa jimbo hilo na kumpoka mgombea wa chadema ambaye ndiye alikuwa chaguo la wananchi.

  2. Hadji Hussein Mponda

  Huyu ni mbunge wa Ulanga Magharibi na vilevile ni Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii.
  Kama alivyo Kombani (jirani yake), naye pia ameshindwa kuongoza jimbo lake na kutatua kero/matatizo ya wapiga kura wake.

  Anaonekana kuwa ni waziri asiye na "sauti" wala maamuzi hasa pale anapotakiwa kutoa maamuzi sahihi na ya haraka.

  Ameshindwa kutatua mgogoro wa hivi karibuni wa madaktari ambao chanzo chake ni uozo uliopo katika wizara ambayo yeye anaiongoza, na matokeo yake kusababisha adha kubwa kwa wananchi vikiwemo vifo ambavyo vingeweza kuepukika.

  Katika kipindi chote cha mgogoro wa madaktari, hakuwahi kutoa japo kauli yenye kuonesha nia yake ya kutatua mgogoro huo na badala yake alikaa kimya hadi pale walio chini yake walipotoa maamuzi yaliyochochea mgogoro huo na kufanya hali kuwa mbaya zaidi.


  3. Mustafa Haidi Makunganya Mkulo:

  Ni mbunge wa Kilosa na Waziri wa Fedha na Uchumi.

  Licha ya kuwa na uzoefu mkubwa wa mambo ya fedha na uchumi lakini aemshindwa kabisa kutumia uzoefu wake huo katika nafasi aliyopo kulisaidia taifa.

  Taifa limekumbwa na mfumuko mkubwa wa bei na hali ngumu ya maisha ambayo haijawahi kutokea kwa miaka mingi mno.

  Anaonekana kupwaya sana katika nafasi hiyo na hajui nini cha kufanya ili kulikwamua taifa kutoka katika hali ngumu.
  Kwa mara ya kwanza tunasikia nchi haina fedha kwenye akiba yake, yeye akiwa ndio mwenye dhamana ya hayo mambo.

  Ameshindwa kusaidia wapiga kura wake hasa pale walipopata na maafa makubwa ya mafuriko. Alisubiri muda wa kupokea misaada tu ili "auze sura".

  4. Lucy Sawere Nkya:

  Ni mbunge wa Morogoro Kusini-Mashariki na ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.

  Kama mwenziye Mponda, huyu alishindwa kabisa kutatua mgogoro wa wizara ya Afya na badala yake inasemekana alichangia kwa kiasi kikubwa kukuza mgogoro huo katika hatua ambayo ulifikia akishirikiana na katibu mkuu wa wizara hiyi bi. Blandina Nyoni.

  Hana uwezo wa kutafuta suluhu ya matatizo pindi anapotakiwa kufanya hivyo.
  Anonekana ana element ya ubinafsi.

  Ameshindwa kuwatumikia wapiga kura wa jimbo lake.

  5. Abdul Rajab Mteketa:

  Ni mbunge wa Kilombero.
  Ana elimu ya cheti tu.

  Inasemekana hajawahi kutembelea jimbo lake hadi wakati wa msiba wa marehemu Regia.
  Ameshindwa kabisa kuwatumikia wananchi wake.

  Alishirikiana na akina Kombani na Mponda kuchakachua kura za mgombea wa chadema katika jimbo la Kilombero.

  Hatakiwi kabisa na wananchi wa Kilombero.

  6. Benno Ndulu:

  Ni gavana wa Benki kuu.

  Ni mwenyeji wa Ulanga.

  Kama Mkulo, ameshindwa kutumia nafasi yake ya ugavana na uzoefu wake wa mambo ya fedha na uchumi katika kushughulikia suala la mfumuko wa bei.
  Hali ngumu waliyonayo watanzania inatokana na mfumuko wa bei ambao yeye ni mdau mkuu wa kushughulikia tatizo hilo.

  Aliwahi kutuhumiwa kufanya ukarabati wa nyumba ya gavana na naibu wake kwa mabilioni ya shilingi (ufisadi?).


  Ukiangalia kwa makini ni kuwa nafasi nyingi nyeti serikalini zinashikiliwa na watu ambao wengi wao ama wana asili ya mkoa wa Morogoro au ni wakazi wa muda mrefu wa maeneo ya mkoa huo.
  Bado napata shida kama kuna uhusiano wowote kati ya mkoa huo na kuboronga kwa viongozi ambao wanatokea huko.

  Kuna matatizo gani Morogoro?

  Hapo sijawataja akina Liyumba, Ngasongwa.......na wengineo....

  Nita-update kwa kadri nitakapopata muda.
  Ni hayo tu kwa sasa.
   
 2. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  hao uliowataja wana matatizo yao binafsi tu.mbona the late regia alikuwa smart.
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Duh jamaa kachambua. Inawezekana ni matatizo ya watu binafsi lakini kuwapa watu wa sehemu moja majukumu ya uchumi si vyema sana. Watu wa sehemu moja majukumu ya afya pia si vema. Majukumu ya vyombo vya ulinzi kwa watu wa sehemu moja pia si muafaka. Hayo tu.
   
 4. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu nafikiri tatizo si kutokea mkoa wa morogoro,bali tatizo ni kua ktk chama kilichoshika dola na hakipo makini!mbona regia alikua smart?nicas mahinda na prof shivji je?hata liyumba si mbovu kiutendaji na hata upstairs pia
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Feb 13, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Duh kumbe Liyumba naye anatoka fasi ya Morogoro! Wanakula magimbi hawa.
   
 6. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Watch out Untitled.jpg
   
 7. NYENJENKURU

  NYENJENKURU JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mbona umesahau Dr.Ngasongwa,Jaji Mwaisumo na Lumbanga?Wamefanya nini kwa mkoa wa Morogoro?
   
 8. D

  DATOGA Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Je Prof. Lipumba ni wa wapi? nahisi itakuwa hukohuko
   
 9. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sijawasahau. Niliamua kuwa-spea tu kwa sababu hawako kwenye uongozi kwa sasa....lakini ni wale wale tu.
   
 10. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tena ukiangalia kwa unfani, wengi wao wanatokea maeneo ya Morogoro Kusini....sasa sijui ni nini..!
   
 11. senior citizen

  senior citizen Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Omary Mahita (RTD) IGP...?????Celine Kombani atakumbukwa na wakurugenzi aliyewapromote alipokuwa TAMISEMI ikiwa ni pamoja na maofisa wa kawaida kuwa maofisa mipango ambao wengi wao wAmeshindwa majukumu yao mfano mzuri ni DED wA SAME maamuz yote yanatoka kwa DC..
   
 12. M

  Mpenda Posho Senior Member

  #12
  Mar 8, 2013
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huko huko maeneo ya Matombo karibu ya Mtombozi
   
 13. S

  Sangomwile JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2013
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 3,091
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Ngoja tujipange tuje na majibu,lakini ni mkoa gani viongozi wake wako smart?
   
 14. K

  Kolero JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2013
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 493
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kilimanjaro na Mbeya!
   
 15. m

  malaka JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2013
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Lipumba wa Tabora. Tena kule nako kuna SITA, Kapuya na Al-shabab. Kule ndio kumeoza bora hata morogoro kidogo Abood anajitahidi ingawa bado..
   
 16. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2013
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Anatoa basi kuukuu kwa ajili ya mazishi. Waruguru wanafurahi kweli!
   
 17. M

  Mndamba Member

  #17
  Mar 12, 2013
  Joined: Jun 22, 2007
  Messages: 50
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Lumbanga ndio kiboko yao. Huyu ni mwenyeji wa Mngeta/Mchombe. Yeye alikuwa anatumia Helikopta kuja Kijijini akitokea Dar kuangalia wazazi wake wakati alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kuhimiza utengenezaji wa barabara kutoka Ifakara-Mlimba kwa kiwango cha Lami. Hapo Kijijini hakuna umeme japo Umeme kutoka Kihansi wapita hapo hapo. Aaaargh sijui bwana nafikiri kuna tatizo.
   
 18. m

  malaka JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2013
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ebwana wee usipime. Tena kwa hilo kawaweza kweli wenzetu. Huku sasa maji ya bomba yanatoka yananuka vibaya ila life goes on du!!!.
   
 19. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2015
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Guys, Kama mwana CCM najitokeza kuwatetea viongozi wa Kisiasa na Dola wanaotokea MOROGORO.
  1: Hulka yetu ni Utumishi uliotukuka na USIA na upendeleo.
  2:Katika moundo mbinu MOROGORO ilikuwa tayari imepitiwa na barabara kuu za kuunganisha Mkoa na mkoa kwa asilimia 80 tangu awamu ya kwanza ya utawala , tulikuwa na viporo vichache Moro-Tanga,Moro-Ruvuma na Moro - Njombe, Miradi hi tayari sasa imeridhiwa na kidogo awamu hii imeanzaaa and definately Magufuli ataikamilisha.
  3. Kwenye elimu tang awamu ya Julius tupo vema sasa awamu ya none Kanisa Catholic wamepeleka St. Augustine University college St. Francis..
  4.Afya tangu uhuru tuna huduma bora toka Ushirika wa serikalii na makanisa....
  5. Utawala Wilaya ya Ulanga imezaa KILOMBERO 1975, sasa Malinyi 2015 na Halmashauri ya Mji Ifakara 2015

  ujio wa Wilaya ya Malinyi umechangiwa na Dkt. Ngasongwa,Dkt MPONDA,Celina Kombani na wadau wa maendeleo walio Kote nchini Kama kinda Prof. Ndullu ,MDC na RAIS Kikwete aliyetembelea eneo hili zaidi ya Mara tatu na Kuwait RAIS pekee anayelijua eneo hili in n out.
  Barabara ya Songea ni jitihada za makusudi za Dkt Ngasongwa na ridhaa ya RAIS Mkapa juu ya mradi, Jakaya akaipandisha daraja 2009 na Kuwa ya Tanroads ,ktk ile plan yake kuunganisha mikoa kwa lami.

  Daraja la mto KILOMBERO...Dkt Ngasongwa 2003 ndie aliyewaomba BADEA kutufadhiri kk mradi huu ktk feasibility study na kuendelea....Infact daraja hili lapaswa kubeba jina la NGASONGWA (atakayehitaji ufafanuzi why Ngasongwa ni inbox)

  All in all viongozi wetu wengi hawabebwibebwi tu, wako vena upstairs na ethically.....I defend them , I can defend CCM AND OUR BROTHERS N SISTERS WHO ARE CURRENTLY SERVING THIS COUNTRY DELIGENTLY.
   
 20. ILAN RAMON

  ILAN RAMON JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2015
  Joined: Sep 10, 2013
  Messages: 6,578
  Likes Received: 1,526
  Trophy Points: 280
  regia ni mchaga
   
Loading...