Ujasiri aliopata Mkapa ni siku ile kwenye sherehe ya kuwekwa wakfu na kutawaza Askofu wa Mbinga ambapo Kikwete katika hotuba yake kwa kuwanyooshea kidole viongozi wa dini wakati kosa labda ni mtu fulani mmoa au wawili wasio na umaarufu katika mashirika ya dini wakati Mkapa akishuhudia imeonyesha dhahiri udhaifu mkubwa alio nao Kikwete na ukosefu wa busara kutoangalia watu, nafasi, tukio na mazingira anapotoa tamko .
Kwa mtazamo wangu Marais wote waliomtangulia Kikwete, kuanzia Nyerere, Mwinyi na Mkapa wasingeota tamshi kama lile kwa watu wale, mazingira yale, nafasi ile na tukio lile na nina hakika kati ya wahudhuriaji viongozi wa dini pale hakuna hata mmoja ambaye anahusika na biashara ya madawa ya kulevya.
Mkapa ujasiri huo aliopata ni kutokana na aibu aliyoipata kama kiongozi mwandamizi mstaafu kushuhudia kiongozi aliopo madarakani kutoa matamshi kama yale kwa watu ambao hakutegemea kwa nafasi na heshima yao kwa jamii. Kuna ya kuvumilika kisiasa lakini inapofikia kuwavunjia heshima watu wenye nyadhifa kama za maaskofu wale katika jamii mtu mwenye dhamira ya kujali nafasi zao anapata uchungu na ujasiri wa kufumba macho na kuongelea ukweli wa hali halisi ilivyo.