viongozi hawa wanahataisha amani ya taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

viongozi hawa wanahataisha amani ya taifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kalunguine, Oct 31, 2012.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  jumapili iliyopita nilikuwa kanisani katika wilaya ya manyoni katika kata ya mitundu,wakati ibada inaendelea inaendelea mara ikaja land cruiser iliyobeba wachungaji wa 3 wa makanisa ya TAG-MANYONI,AIC MANYONI NA KKKT.WAKAJINADI YA KUWA WAMETUMWA NA MAKANISA YA MANYONI eti kuwahadharisha wakristo kuhusu upendeleo wanaopewa waislamu katika katiba mpya,kwamba wakristo wasipochukua hatua za haraka mahkama ya kadhi itaingizwa katika katiba,oic,adhabu ya kifo,mgawanyo sawa wa madaraka na eti wakristo tudai katiba itambue kuwa tunaweza kuchinja wanyama wetu badala ya kuchinjiwa na waislamu.

  yote yanaweza kuwa sawa lakini kilichonitisha ni video ya kizushi na kichochezi iliyokuwa inaonyeshwa pale ili kuwafanya wakristo waichukie mahkama ya kadhi,walionyesha video ya maharamia wa kisomali wakimchinja mwenzao kwa madai ya kuwasaliti katika harakati zao lakini wachungaji hawa wakatudanganya wakristo eti huyo mchinjaji ni kadhi!

  zaidi ya hayo,wakauliza dini za viongozi wa kuchaguliwa kuanzia mwenyekiti wa kijiji,diwani na hata mbunge,walipojibiwa kuwa ni wakristo wakaitika haleluyaa! wakatuhimiza 2015 tuchague wakristo tu! baadhi yetu kanisani wakasema lakini hawa waliochaguliwa hawatusaidii lakini jamaa wakasema hata kama hawasaidii chagueni wakristo kumpendeza mungu.

  hawa jamaa wanazunguka na lan cruiser kanakouzaga biblia na vitabu vya kikristo no zake ni T 264 BJJ.vyombo vya usalama chukueni hatua kwani hii ni hatari kwa usalama wa taifa na mshikamano uliopo.
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  J.k ndio nyangumi,hao wengine dagaa wa kigoma
   
 3. Nokla

  Nokla JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 2,121
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Wenzio tunafanya siri wewe umeyaleta hapa lengo lako nini?
   
Loading...