Viongozi hawa vipi!!!!

Viongozi hawa vipi!!!!

Kibagata

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
773
Reaction score
135
Wakati wa sakata la kuandikwa kwa katiba mpya, viongozi wandamizi wakubwa kabisa serikalini walipinga sana wakisema hakuna haja ya kuandika katiba mpya hii ya sasa inakidhi au inatosha. Hawa ilikuwa mwanasheria Mkuu wa serikali ndugu WEREMA na waziri wa sheria na katiba Serina KOMBANI.

Lakini baada ya jamii kupiga sana kelele mkuu wa nchi akaona kuna hoja hapa akakubali katiba mpya iandikwe.

Majuzi kati hapa swala la Gas, waziri wa nishati na mkuu wa mkoa wakasema hoja za kisiasa hizo mara wananchi hawa ni wachoyo, wahuni, wahaini, lakini mwisho wa siku serikali kuu baada ya kuona hali inakuwa tete, mali na majengo kuteketezwa na matamko mengi ya wapenda haki na Maendeleo Waziri mkuu na timu yake wameenda kule wamewasikiliza watu wa kusini, wameona kuna logic behind wametoa tamko lenye kuleta matumain kwa wana kusini kuhusu gas.

Hoja hapa kwa nn president usiwafukuze watu hawa ambao hawafikrii kwa mapana kabla ya kutoa matamko yao kwa niaba ya serikali.

WANASABABISHA MATATIZO NA VIFO NA KUACHA YATIMA NA WATEGEMEZI WENGI AMBAO NI MZIGO KWA SERIKALI NA WALALA HOI WANAOWATUNZA.
 
Ukiwauliza watakuambia yalikua ni maoni binafsi na sio matamko ya serikali......
 
Baba akiwa dhaifu watoto watakua dhaifu
 
Back
Top Bottom