Viongozi CHADEMA Mungu awatie moyo

Administer

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
930
1,408
Viongozi CHADEMA mmepambana na changamoto kubwa sana kutoka utawala huu wa CCM,endeleeni kufanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya chama.

Sijawahi kuchukizwa kwa maamuzi mbalimbali mliyoyafanya kwa mwanachama aliyeikosea CHADEMA ,mliwaadhibu wakosefu ipasavyo na kwa haki hila kujali nafasi zao.

Kwa sisi wapenda mabadiliko hatupendi kuona upinzani hasa CHADEMA inakufa,najiuliza upinzani ukifa kura yangu nitampigia nani?

Sijawahi kuipigia kura CCM katika chaguzi zote hata kama inashinda kwa hila.Nina hofu CHADEMA ikifa sisi wasakatonge tutadharauliwa sana.

Ogopa kuishi katika nchi ambayo serikali yake inauhakiki wa kushinda uchaguzi kwa njia yoyote wanachi mtaongozwa kama gari bovu.
 
Dah! Ila naamini sasa Habari za Siasa hazitakiwi kuhusishwa na Mungu wa kweli wa isaka na Yakobo.

Najaribu kuachana nazo lkn najikuta naumia tu. Nimejaribu kuhamisha fikra za kutokuwa mpenzi wa siasa za ukweli, niwe mjanja mjanja hivi naona bado. So nipo tu nataraji Haki itokee siku moja Mungu akijalia. Lkn yanayoendelea yanazidi kuwaathiri watu wengi zaidi.

Ukiacha wale wanafiki wachache wanasema hata mfanye nini, hali itakuwa hvhv! Kimsingi hatutengenezi future Nzuri
 
Wewe Jamaa Upo Kama Mimi YAANI NIKIPIGA KURA CHADEMA SIJUI kwanini huwa nasikia TU amani moyoni HATA kama hawatashinda.

UZURI WA CHADEMA haiogopi KUFUKUZA MTU HATA AWE NANI, NAKUMBUKA ZITO KABWE alifukuzwa NA BADO chama kipo imara......hivyo sitoshangaa endapo wakiwatimua viongozi waliokiuka MWENENDO WA CHAMA
 
Kwa kweli Mimi ikipita siku bila ya kuwaombea viongoz wa Chadema. Hiyo siku huwa ninajiona Nina hatia kubwa sana. Mbowe. Lissu . Heche. Mnyika. and all central committee members, don't give up guys . we are with you . we love you. Tunafaham magumu mnayopita . tunafaham mateso mnayoyapata chin ya utawala huu dhalimu. MUNGU AWATANGULIE.
 
Mungu awajaalie viongozi wa Chadema wawe ni mioyo kama waliyonayo sasa.
wavumilivu,wasikivu na waelewa, hasa linapokuja swala la kunusuru taifa letu kwenye kabali za mabeberu wawe wanalegeza kama walivyolegeza sasa
 
Niliwahi sema humu mwaka 2012 na sasa narudia tena, chadema hata igeuke band ya muziki nitakuwemo.

Mie siasa ni imani sio MTU wala maslahi.

Mungu awatie nguvu viongozi wa cdm watz tuko pamoja nanyi.
Uko sawa kabisa, maana hata nzi kwenye usaha humwelezi wala humwambii kitu.
 
Kumbe kuna watu wana misimamo yao kimya kimya ila huwa hawapigi kelele kama wengine, big up.
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom