Viongozi CHADEMA: Mkakati sasa Kulinda Kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi CHADEMA: Mkakati sasa Kulinda Kura

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mozze, Sep 9, 2010.

 1. m

  mozze Senior Member

  #1
  Sep 9, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi hali ya upepo inavyoelekea kuna dalili CCM maji yako kidevuni sasa! Chadama na mgombea wake Dr. Slaa wanaonyesha wamekubalika kwa kiasi kikubwa. Hadi sasa inaonyesha kuna mtaji wa kutosha, japo utaongezeka katika kipindi kilichobaki hadi kufikia 31 Oct.

  Na kwa vile CCM wanaelekea kuishiwa na mbinu, siasa za "maji ya mtaro" zinapoteza nguvu sasa, wataelekeza nguvu kwenye Hujuma wakati wa kupiga na kuhesabu Kura na kutangaza matokeo.

  Sasa basi nadhani ni wakati muafa sasa kuacha kupoteza nguvu kwenye malumbano na kuanza kuweka mikakati madhubuti ya KULINDA KURA! Sisemi kuwa kutangaza sera kusimamishwe, ila tuanze kuwa makini sasa kufichua mbinu zote ambazo CCM wanaweza kutumia ili kukinyima Chama Ushindi. I have some suggestions:

  1. Chama kianzishe njia ya kupokea taarifa za watu wanaorubuni wanachi ili wazinunue Shahada zao.
  2. Chama kiajiri watu walio makini, na wenye uchungu na nchi yao kuwa mawakala. Hii ni Muhimu sana, Chama kiwe makini na mawakala feki mana CCM inaweza kupenyeza watu wao, au wakapenya watu wabinafsi wakanunuliwa na CCM kukihujumu chama kama wale watu waliojitoa Ubunge. Zoezi hili lifanyike kwa makini sana.
  3. Hakuna haja ya kugharamika kwa mabango na t-shirts kama CCM bali hizo hela zitumike kuwawezesha Mawakala kufanya kazi zao vizuri. Chama kitangaze nafasi za watu kujitolea kwa hili zoezi na kuwalipa gharama mbalimbali.
  4. Ikiwezekana Vituo vilindwe na watu kutoka sehemu nyingine, mfano; mawakala kutoka Dar waende Mtwara na wale wa Mtwara waje Dar na kama hivyo ili CCM isiweze kuwalaghai kirahisi.

  Huu ni mchango wangu, Wapenda mabadiliko ya kimaendeleo wengine wachangie mbinu nzuri zaidi.
   
Loading...