Viongozi acheni ubinafsi, mnamchukiza Mungu

Mugabe Jr

Senior Member
Aug 19, 2020
160
287
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini siwafichi kazi ya kulijenga taifa hili itaendelea kuwa ngumu, ngumu haswa kama viongozi hamtaacha ubinafsi. Nasisitiza tena, taifa hili halitasonga mbele kama viongozi hawataacha ubinafsi. Nchi hii ina utajiri mkubwa sana wa rasilimali kuliko nchi nyingine nyingi barani Afrika na duniani kwa ujumla. Kiukweli Tanzania MUNGU aliibariki, akaipatia kila kitu, akaipatia ardhi ya kutosha tena yenye rutuba, akaipatia maziwa, bahari, madini ya Tanzanite yasiyopatikana sehemu yoyote ile ulimwenguni, mito na rasilimali nyingine nixing kadha wa kadha. Ila licha ya huu utajiri mkubwa wa rasilimali, wananchi katika taifa hili bado wanaendelea kuogelea katika dimbwi kubwa la umasikini wa kutupwa, kwasababu ya ubinafsi wa viongozi.

Kiukweli moyo wangu unavuja damu nikiona wananchi katika taifa hili lenye ukwasi mkubwa bado wengi wao wanaishi maisha ya ufukara. Ingawa ni miaka sitini sasa tangu taifa hili lipate uhuru toka kwa muingereza, ila chakushangaza maeneo mengi katika nchi hii bado kuna upatikanaji duni wa huduma za kijamii kwa ujumla.

Katika huduma za afya hali bado ni mbaya, hospitali na zahanati bado ni chache sana, na hata hospitali zilizopo nyingi yapo majengo tuu na watumishi, ila vifaa hakuna, madawa hakuna. Wananchi wa maeneo mbalimbali katika taifa hili ni mashahidi wazuri wa hiki ninachoeleza, kwani wengi wamekuwa wakilalamika waendapo katika vituo hivi vya afya baada ya kufanyiwa vipimo wamekuwa wakipewa majibu kwamba dawa hakuna, dawa hazipo, dawa zimeisha. Tatizo hili limesabishwa na ubinafsi wa viongozi wetu wanaoweka maslahi yao binafsi mbele. Viongozi hawa wabinafsi wasio na huruma wamekuwa wakitumia fedha za serikali kujinufaisha wenyewe.

Licha ya kutambua uwepo wa huduma duni za afya, kukosena kwa madawa hospitalini. Ila hawa viongozi wabinafsi wameendelea kulipana mishahara minono, posho zisizo na tija, viongozi hawa wabinafsi wamekosa nyuso zimekosa haya bado wamekuwa wakilalamika kuwa mishahara yao haitoshi, hiyo haitoshi bado wanaendelea kutumia pesa ya umma kwa ajili ya kujinunulia magari ya kifahari. na pengine kwa kutojali shida za wananchi wapo viongozi wamekuwa wakishiriki kuiba dawa, pamoja na vifaa tiba vinavyotolewa na wahisani, na kisha kufungua pharmacy zao mitaani na kupiga pesa.

Hali katika vituo vyetu vya afya ni mbaya sana ,hata katika kipindi hiki nchi yetu ikiendelea kupambana na hili janga la Corona tumesikia kwa masikio yetu baadhi ya vituo vyetu vya afya vikikili wazi kuwepo kwa upungufu wa mitungi ya gesi. Viongozi hawa wabinafsi wanalijua suala hili, wanafahamu fikra huduma zilivyokuwa mbovu katika hospitali zetu, na wamegoma kulivalia njuga suala hili na kulipatia ufumbuzi kutokana na ubinafsi kwasababu ukwasi na fedha walizokwisha chuma zinawaruhusu kutibiwa nje ya nchi tena hospitali za kisasa pindi wauguapo.

Ili tutatue tatizo hili viongozi wanapaswa kuachana na ubinafsi, kwa kuacha kutumia fedha za umma kwa maslahi yao binafsi, kuacha kulipana posho zisizo na msingi, na badala yake fedha hizi zielekezwe kuboresha huduma za afya nchini. Viongozi inatakiwa pia waache ubinafsi na kukubali kulipwa mishahara ya kawaida inayoendana na uchumi wa nchi, kuliko kuendelea kulipana mishahara mikubwa na malupulupu huku wananchi wakiendelea kuteseka. Viongozi pia ambao ni wabunge waache ubinafsi na kukubali mishahara yao kukatwa kodi, vilevile kuna nafasi za uongozi zisizo na mantiki yoyote kwa mfano wabunge wa viti maalumu, hizi nafasi za viti maalumu bungeni zingeondolewa ili serikali kujipunguzia mzigo na hizo gharama zitumike katika kuboresha huduma za afya nchini.

Katika upande wa elimu nako hali bado ni mbaya sana. Mitahala inayotumika katika elimu yetu ni ukweli usiopingika kwamba imepitwa na wakati, na haimuandai kijana kuweza kuyatawala mazingira ya ulimwengu wa sasa. Kwa ufupi mambo yamebadirika ila chakushangaza mitahala inayotumika ni ileile iliyokosa ubunifu unaohitajika na dunia ya sasa, na kuendelea kujikita katika nadharia. Matokeo ya mitahala hii isiyoendana na hali ya sasa imekuwa ikizalisha wasomi wengi ambao hawana ujuzi na ubunifu nje na taaluma zao, mitahala hii iliyooza ni dhahiri iliwaandaa vijana hawa wasomi kisaikolojia kwamba hitimisho la elimu zao ni kuajiriwa. Elimu inayotolewa kutokana na mitahala yetu imeshindwa kumuandaa kijana msomi wa taifa hili kufanya shughuli nyingine tofauti na kile alichosomea. Miaka ya hivi karibuni mambo yamebadilika kutokana na ongezeko la wasomi na mikakati mibovu ya hawa viongozi wabinafsi ajira sasa zimekuwa hazipatikani, na hata zikipatikana urasimu umekuwa ni mwingi.

Cha kusikitisha viongozi hawa wabinafsi suala hili mitahala inayotumika imepitwa na wakati wanalifahamu miaka nenda miaka rudi, ila ubinafsi wao wameshindwa kuiboresha hii mitahala ya elimu hapa nchini, na kuamua kuwapeleka na kuwasomesha watoto huko katika nchi za magharibi na nchi nyingine duniani zinazotoa elimu bora kuliko hii itolewayo hapa nchini. Viongozi hawa wabinafsi wameshindwa kufanya mabadiliko katika hii mitahala ya elimu na kuacha watoto wa watanzania wakiendelea kufundishwa elimu ya hovyo, huku wao wakisomesha watoto wao nje ya nchi.

Hakika inatia simanzi hata linapokuja suala la ukosefu wa ajira, viongozi hawa wabinafsi hawaguswi nalo kabisa na hawako tayari kulipatia ufumbuzi. Viongozi hawa wabinafsi wamekuwa wakitoa kauli mbaya kwa hawa vijana wasomi na kuwaambia wajiajiri ilihali wanafahamu kuwa vijana hawa wasomi wengi wao ni watoto wa wananchi masikini, na elimu waliopatiwa kutokana na hii mitahala mibovu haikuwaandaa kuweza kujiajiri. Bado haitoshi viongozi hawa wabinafsi wameendelea kuruhusu mitahala hii iliyopitwa na wakati iendelee kutumika na kuzalisha vijana wasomi maelfu kila mwaka huku ikiwasusa na kuwatelekeza na vyeti vyao mitaani, na kuwataka waende kujiajiri. Viongozi hawa wabinafsi wamewaacha vijana hawa wasomi ambao wengi wao ni watoto wa wananchi masikini na kuwaambia wakajiajiri, huku wao wakiwapatia watoto wao ajira nzuri serikalini na kwenye mashirika ya umma.

Kilio hiki cha vijana hawa wasomi waliokosa ajira, pamoja na wazazi wao ambao ni wananchi masikini, imekuwa kama kelele kwa viongozi hawa wabinafsi hivyo wameamua kuweka pamba masikioni bila kujali hatma ya vijana hawa ambao wengi ni tegemeo katika familia zao. Viongozi hawa wabinafsi wanapoulizwa wana mikakati ipi kuliokoa hili kundi la vijana wasomi waliokosa ajira wamekuwa wakipaniki na kutoa majibu ya dharau na fedhea. Viongozi hawa wabinafsi wamekuwa wakisikika wakiwaambia vijana hawa wasomi katika taaluma mbalimbali kama vile udaktari, uwalimu kuwa “wajiajiri, wauze hata karanga”. Kwakweli Inasikitisha sana, hivi kweli haya ni majibu ya kumpatia kijana huyu msomi aliyebeba matumaini ya familia yake masikini, kijana huyu aliyetumia miaka mingi kupambania ndoto yake ya kuwa daktari au kuwa mwalimu, leo unamwambia akauze karanga, akachome mahindi.

Viongozi badilikeni acheni ubinafsi, tafadhali gusweni na matatizo ya wananchi wenu, na umizeni akili zenu kupata suluhisho la hili tatizo. Acheni ubinafsi wa kukimbilia kusomesha watoto wenu katika shule zilizopo nje ya nchi, badala yake boresheni mitahala ya elimu yetu iendane ubora na elimu itolewayo huko mnapopeleka watoto wenu. Tatizo haliwezi tatuka kwa kulikimbia na mkumbuke nyinyi ni viongozi wa wananchi, siyo viongozi wa familia zenu hivyo acheni ubinafsi matendo yenu inatakiwa yawe ni yakutafuta suluhu ya shida zinazowakumba wananchi badala ya kuzifumbia macho na kuona kama hayawahusu. Viongozi acheni ubinafsi kubalini kukosolewa, kubalini kuelekezwa msiyoyafahamu. Viongozi acheni ubinafsi tuijenge Tanzania yenye haki na usawa

Vilevile tumeona viongozi hawa wabinafsi wakiwa hadaa na kuwataka wananchi kuwa wazalendo na kulipa kodi ili kuijenga nchi, huku wao wakishindwa kuwa mfano mzuri na wakuigwa katika ulipaji wa kodi. Kiukweli suala la kuijenga hii nchi viongozi hawa wabinafsi, wamewaachia wananchi wenyewe. Viongozi wamekuwa wabinafsi na kujali maslahi yao zaidi kuliko kushughulikia kero za wananchi wao. Inasikitisha kuona mpaka leo nchi hii ambayo ilipata uhuru wake miaka sitini iliyopita, iliyobarikiwa maziwa, mito na bahari bado mpaka muda huu kuna maeneo yanashida ya maji ambayo ni hitaji muhimu la binadamu. Halafu upande wa pili tumeshuhudia hivi karibuni mmoja wa kiongozi akilalamika kuwa mishahara yao minono inayoambatana na posho nyingi kuwa bado haitoshi. Kiongozi huyu ni mfano wa viongozi wengi wabinafsi waliopata nyadhifa ya uongozi katika taifa hili. Viongozi hawa wabinafsi wamekuwa wakiwaza tuu kuyashibisha matumbo yao na kujali maslahi yao wenyewe kuliko shida, matatizo na kero zinazowakumba wananchi wao. Viongozi hawa wabinafsi wamekuwa wakifanya maamuzi ya hovyo bila kujali athari za hayo maamuzi kwa wahusika ambao ni wananchi wenyewe. Viongozi hawa wabinafsi wamekuwa wakifanya maamuzi yanayo waumiza wananchi, na wanapoulizwa wamekuwa wakitoa majibu ya jeuri na kujiona miungu watu kwasababu ya ubinafsi wao.

Hivi karibuni tumeona viongozi hawa wabinafsi wakipitisha sheria ya tozo ya miamala, ambayo wananchi wamekuwa wakiipinga vikali na kuilalamikia kwamba siyo rafiki kabisa, ila viongozi hawa wabinafsi wasiojali raia wao wameyaziba masikio yao na kuamua kuwaumiza wananchi. Viongozi hawa wabinafsi wamekuwa wakiwachukia wazi wazi watu wanaowakosoa kitu ambacho siyo sawa. Badala ya kurekebisha pale wanapokosolewa ili wafanye vizuri zaidi, viongozi hawa wabinafsi wamekuwa hawataki kabisa kukosolewa, viongozi hawa wabinafsi wanajiona wako sawa kwenye kila wanachofanya kutokana na ubinafsi wao. Viongozi hawa wabinafsi wamekuwa hawataki kushauriwa, kitu ambacho kinawapelekea kufanya maamuzi ya hovyo.

Viongozi acheni ubinafsi, badilikeni kuweni na mioyo ya utu, kuweni na mioyo ya huruma yenye kuguswa na vilio vya wananchi. Viongozi badilikeni acheni ubinafsi, shida za wananchi zichukueni, zibebeni kama shida zenu ziwanyime usingizi, na muumize akili zenu kuzipatia ufumbuzi. Viongozi acheni ubinafsi, nawaambia tena acheni ubinafsi na kujikweza kiukweli hamtapungukiwa na kitu kwa kusikiliza ushauri mnaopewa na makundi mbalimbali katika jamii, badilikeni acheni ubinafsi heshimuni mawazo ya wengine kwani wote tunaijenga Tanzania moja. Viongozi badilikeni acheni ubinafsi na kuwachukia wanaowakosoa, badala yake jitafakarini matendo yenu na kuboresha pale mnapokosea bila kuona aibu. Viongozi acheni ubinafsi badilikeni ili kila raia wa nchi hii aifurahie keki ya taifa hili, na kila mmoja ajivunie kuwa mtanzania. NAMALIZA KWA KUSEMA “VIONGOZI ACHENI UBINAFSI, MNAMCHUKIZA MUNGU”
 
Sijasoma yote mkuu,nimepata hasira za ghafla Sana ujue upuuzi Kama huo wa Hawa makaburu weusi CCM unanitia hasira Sana nikifikiria,yaani kila nikifikiria kuhusu hii nchi naumia sana sana moyoni Aisee nimezaliwa miaka ya 90's mwishoni Huko ila nikiangalia nchi yangu Ina Lindi kubwa la umaskini Hadi huruma.

Jamani miaka 60 ya uhuru Bado Kodi ya kuingiza gari inazidi Bei ya gari lenyewe aaaaa wewe huu ni ujinga na upumbavu kabisa miaka hii mkulima wa kawaida kununua japo kirikuu ya kubebea mazao Hana hapo bado hujazungumzia suala la pembejeo za kilimo zilivyo ghali kuzidi Bei za mazao na hapo wanasema UTI wa mgongo wa taifa ni kilimo!

Hata japo kupangilia miji tu CCM wameshindwa wataweza nini ndugu!

Aaaaaweeee hebu acheni masikhara wallah tumefeli,tumefeli wadau yaani Leo mbuge mmoja anatembelea gari la million 400 kwenye nchi masikini Kama hii halafu mtarajie siku tutakua nchi za Dunia ya kwanza!

Napinga! Napinga!
Hizo ni ndoto za kiangazi wadau

Nifanyaje Sasa Sina jinsi na kelele za mbwa hazivunji geti!
 
Kuna majamaa walishaliona hilo wakaona waanze kulifanyia kazi kwa kuanza na KATIBA MPYA
lakini hao wabinafsi wakaamua kusema kiongozi wa wanaotaka KATIBA MPYA ni gaidi wamemkamata
Wamesahau athari ya kusema nchi ina GAIDI ni kubwa
Kwa vile hata wageni hawatakuja kwa vile TZ kuna magaidi
Bora Hayati alikuwa anasema ishu zinazo mkumba mtu binafsi kama muhujumi uchumi, mchochezi n.k
Ugaidi siyo swala linalomkumba gaidi pekee bali jamii mpaka dunia
Sasa kwa ishu ya viongozi waache ubinafsi bila maombi ni ngumu maana hawa watu hawataki kujua kuna MTZ anakosa milo mitatu ndio maana wakaweka TOZO
 
Kuna majamaa walishaliona hilo wakaona waanze kulifanyia kazi kwa kuanza na KATIBA MPYA
lakini hao wabinafsi wakaamua kusema kiongozi wa wanaotaka KATIBA MPYA ni gaidi wamemkamata
Wamesahau athari ya kusema nchi ina GAIDI ni kubwa
Kwa vile hata wageni hawatakuja kwa vile TZ kuna magaidi
Bora Hayati alikuwa anasema ishu zinazo mkumba mtu binafsi kama muhujumi uchumi, mchochezi n.k
Ugaidi siyo swala linalomkumba gaidi pekee bali jamii mpaka dunia
Sasa kwa ishu ya viongozi waache ubinafsi bila maombi ni ngumu maana hawa watu hawataki kujua kuna MTZ anakosa milo mitatu ndio maana wakaweka TOZO
Fimbo ya kwanza Mungu ameleta,amezuia mvua tena kwa kufuata mipaka,ukienda malawi inanyesha,Zambia inanyesha,Congo inanyesha, Mozambique inanyesha,hii ni shida kuu katika Taifa hili.
 
Back
Top Bottom