Viongozi 2 wafikishwa mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU mkoa wa MARA,imewakamata na kuwafikisha mahakamani viongozi wawili wa kata ya Suguti katika halmashauri ya Musoma vijijini kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka kwa kujipatia kiasi cha shilingi milioni 50 ambazo zilitolewa na halmashauri hiyo kwa ajili ya ununuzi wa Terekta la kikundi cha vijana wa kata hiyo.

Watuhumiwa ambao wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mfawidhi wa wilaya ya Musoma ni aliyekuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Musoma ambaye pia ni diwani wa kata ya Suguti Bw Denisi Ekwabi na aliyekuwa mtendaji wa kata hiyo Bw Jackson Mgendi Marwa.

Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Bw Erick Kiwia,ameiambia mahakama hiyo mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Bw Karim Mushi,kuwa watushitakiwa hao wote kwa pamoja,machi 9 na mei 24 mwaka 2015 walitumia madaraka yao vibaya kinyume cha kifungu cha 31 cha sheria za kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Amesema mahakamani hapo kuwa june 29 mwaka 2013 halmashauri ya Musoma iliingiza kiasi cha shilingi milioni 50 katika akaunti ya mfuko wa maendeleo wa kata ya Suguti namba 3032301513 na kwamba wakiwa waweka saini Desemba 02 mwaka 2013 walizichukua fedha hizo na kukaa nazo hadi walipoamua kwenda kununua trekta aina ya Masey Ferguson kwa majina yao toka kampuni ya Kilasa kinyume na kanuni 163(1) na 164(1) za manunuzi ya umma za mwaka 2003 kitendo ambacho kilinufaisha kampuni hiyo.

Washitakiwa wote wamekana mashitaka hayo na kwamba mtuhumiwa wa kwanza ametimiza mashirti ya dhamana yaliyotaka kuwa na wadhamini wawili na kutoa kiasi cha shilingi milioni 14,250,000 au mali isiyohamishika huku mshitakiwa wa pili akishindwa kutimisha masharti ya dhamana na kwenda rumande hadi Aprili 25 kesi hiyo itakapo tajwa tena.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom