Nimepata bahati ya kuona ile DVD ya 'The Fake Pastors'. Pamoja na kwamba hadithi yake ina mawaidha mazuri tu, ule uigizaji wa hawa jamaa bado, tena bado sana unahitaji kuongezwa. Wanasema hizo scripts kama wamekariri vile, sio kama watu wanavyoongea katika hali ya kawaida ya kila siku. Kujiita Denzel wa Tanzania, nadhani ni kujikweza kabla hajafikia kiwango cha utaalam wa kuigiza. Nawashauri waongeze kiwango cha kuigiza, kabla ya kutengeneza filamu nyingine.