masai dada
JF-Expert Member
- Dec 29, 2013
- 16,823
- 16,895
Mungu asipolinda nyumba walindao wakesha bure. Lakini pia kwa wakristo Mungu mwenyewe kwenye biblia amekataza haya masanamu..
hizo roho chafu hupenda kukaa kwenye kitu chochote unachokipenda na kukithamini, zimaweza kukaa hata kwenye mafuta ya kupaka au hata kwenye nywele zako..
Cha muhimu ni kujiweka chini ya ulinzi wa Mungu,hizo roho hazitakusogelea kabisa.
Hata zile katuni wanazoangalia watoto, Boomerang, Disney na zinginezo zimejaa mapepo, kwa macho ya watu Wazima tunaona ni katuni za kawaida, ila watoto wanaona ni vimtu vipo uchi wa mnyama, zjnaharibu sana watoto zile!
Kuna huu mdori umecheza film unaitwa CHUCKY, unaukumbuka?
Sasa kuna mwingine amefahamika anaitwa Black Chucky.... Anabamiza watoto si kawaida.
Sirdirashy midoli mingi ya kariakoo imefanyiwa colabo, mchana ni vinyago usiku ni vinyamkera
Zinaharibu sana future ya watoto wetu, km kuna uwezekano wa kumzuia asiangalie inakuwa vizuri zaidi
Amazing hi ni kweli.Kuna kanisa moja niliwah kusali mchungaj alituagiza waumin wenye midoli na kadi zile za wishes like Xmas cards or birthday cards tuzipeleke kanisani na zilichomwa zote ,pastor alisema tunahifadh roho wachafu nyumban wanaokaa kwenye midol na hizo cards
Kweli kazi ipo😉😉
Hornet,njoo ulale nyumbani,hahahahahaaha,Mshana jiheshimu..nimepoteza usingzi wangu wote ....duuuh uwe unaangaliaga na picha za kuleta basi mweh mweh
Hornet,njoo ulale nyumbani,hahahahahaaha,
Sio peke yako,najua humu Mshana amesababisha maafa ya Midoli.
Ukipita mitaani utakuta Members wa JF wameitupa yoote
Ujumbe kwa Mshana,Kwa taarifa nimezopata ni kwamba,Hasira za Midoli wote w JF zinakufuata wewe.
Lakini tuache utani kuna jamaa nimewaambia wasome humu JF hii mada,kila mmoja amesema aisee kweli,kuna siku naona kama home panazingua...hahaha,mmoja yeye kampigia sim House Girl wake aichukue Midoli yoote aweke kwenye Mfuko anaenda na Gari kuichukua,maana ana mtoto mchanga,sasa huwa kinaumwa mara kwa mara.
Hahahahaha,Mshana majangaaaaa
Mkuu naunga mkono hoja.Huwa tunafuga majini vinyamkera madogoli na rohochafu majumbani kwetu bila kujua, tunanunua vinyago na midoli ya gharama kwa ajili ya kupendezesha sebule zetu na wakati mwingine kama kampani vitandani mwetu...hatutishani lakini ni hatari vina roho hivi vitu
Wengi wetu tumeshawahi kuona zana za waganga wa kienyeji na wachawi,hawakosi vinyago na midoli, pia tumeshawahi kuona wale wenzetu waabuduo miungu wana masanamu mengi sana...!yale yote yamebeba roho na ndio hizo wanazoziabudu
Kuna roho zinatangatanga duniani hazina makazi baada ya majumba (miili)yao kuharibika(kufa)hivyo huwayawaya huku na kule zikitafuta makazi kwakuwa roho haiwi na nguvu mpaka ipate pa kukaa.Sasa ndugu yangu unajaza midoli nyumbani au kwenye gari au ofisini unavutia na kukaribisha mapepo
Zipo shuhuda mbalimbali za watu waliofanyiwa mambo au kuona mambo ya ajabu kutoka kwenye midoli na vinyago....punguza kuhifadhi hivi vitu vyaweza kuwa na roho zenye madhara makubwa
Mi niliambiwa midoli vinyago si mizuri kuweka ndani nikawaga siamini mana nilikua naipenda kuiweka sebuleni. Sasa siku moja nikiwa nimelala nimeiweka pembeni nikaona mdoli una nyanyuka na kunirukia nilipiga makelele ya hatari na kutetemeka juu. Tangia siku hyo nimekoma hata kuibeba. Kweli vinyango ni ma spirits machafu kabisa na inaweza ikawa inaleta mikosi.
duu
mtoto wetu wa 5yrs yupo addicted na hizo jamani
eti mshanajr vipi kuhusu mashuka yenye katoon na picha za midoli ???
Hornet,njoo ulale nyumbani,hahahahahaaha,
Sio peke yako,najua humu Mshana amesababisha maafa ya Midoli.
Ukipita mitaani utakuta Members wa JF wameitupa yoote
Ujumbe kwa Mshana,Kwa taarifa nimezopata ni kwamba,Hasira za Midoli wote w JF zinakufuata wewe.
Lakini tuache utani kuna jamaa nimewaambia wasome humu JF hii mada,kila mmoja amesema aisee kweli,kuna siku naona kama home panazingua...hahaha,mmoja yeye kampigia sim House Girl wake aichukue Midoli yoote aweke kwenye Mfuko anaenda na Gari kuichukua,maana ana mtoto mchanga,sasa huwa kinaumwa mara kwa mara.
Hahahahaha,Mshana majangaaaaa
Na ameua biashara ya midori. Mshana watani zako wachaga wanakutafuta. Ole wako