ving'amuzi vya TING;Viogopeni havifai.

ving'amuzi vya TING;Viogopeni havifai.

ferre.g

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2013
Posts
2,215
Reaction score
329
Ndugu watanzania napenda kuwatahadhalisha wote mlokuwa na mpango wa kununua kifaa hiki hakifai hata kuigiliza.

Nina siku saba sasa nakitumia lakini toka juzi yaani siku 4 sasa hakioneshi channel hata moja.

Nimefika ofisini kwao leo mara baada ya kupiga simu yao bila mafanikio nkaambiwa eti mafuta yalikwisha ktk mnara na si punde wametuma mtu kuweka.... sambamba na hilo pia wakadai eti umeme nao unit zilikwisha.

Nawajuza hili hasa wana Mbeya kuweni makini mimi nimeingia MKENGE MWENZENU KITU NI MAGUMASHI HALISHILIKE.

Uliza bei yake sasa nimenunua 110,000yaani laki moja na elfu kumi shilingi.

Nasema huu ni utapeli jamani mtatuua watanzania.
 
Kwa Arusha kingamuzi cha Continental pia kina shida za aina hiyo, yaani hii kitu TCRA ilisema digital hawakufanya utafiti zaidi ya kula 10% za waingizaji wa hivi vingamuzi, au ni mkakati wa maksudi wa kuwanyima Watanzania habari. Ndugu zangu Arusha msinunue Continental decoder ni majanga.
 
hata Dar na sisi tulionunua vya startimes naona mambo kama huko TING na Continenta, eeee TCRA mtunusuru na haya majanga ya wachina
 
Hapa tanga naonna chanel nne tu startv, itv,atn na tbc lakin najiuliza zile chanel 5 walizosema TCRA mbona mara ving'amuz vingine zipo 2,3 au 4 badala ya 5?
 
Poleni sana mi niko Dar naifurahia Azam kwa raha zangu, kitu HD!
 
StarTimes huku Tanga ni channel mbili tu ndio free chanel TBC1 na Chanel Ten. TCRA ni wapu**fu. anaangalia maslahi yao tu, angalau haka kachanel kapya tv one kanatulwaza
 
sawa azam, lakini mbona nawao hawaonyeshi baadhi ya local Tvs??? na pia wana channel chache, kwa mlalahoi bado king'amuzi cha Star time kipo bora aisee!!1
 
Hii thread imeanzishwa na mtoto wa Bakhresa (Azam).
 
Kiukweli natumia AZAM TV na naenjoy ile mbaya!!

AZAM TV funga kazi.
 
dah uku morogoro kwenye star times tushasahau eatv na itv atujui hata shida ni nini
 
Back
Top Bottom