Mkuu umejitahidi kumuelezea jamaa lakini hujamtendea haki Vincent Van Gogh...kumueelezea huyu genius mgonjwa wa akili aliekuwa na uwezo hadi wa kuchora upepo unaovuma na kuuweka kwenye mchoro na muhasisi wa sketch za kuchora kwa rangi za mafuta na ajabu zaidi alifanya kazi zake zote kubwa akiwa na matatizo ya akili (ukichaa) kwenye asylum home yaani kama Mirembe vile, ambapo Dunia imekiri kwamba anaqualify kuingia Kwenye kundi la magenius watano wa uchoraji Duniani wa muda wote akiwemo Leonardo Da Vinci, Michelangelo, Vincent Van Gogh, Raphael, Pablo Picasso.Vincent Willem van Gogh (30 Machi 1853 - 29
Julai 1890 ) alikuwa mchoraji kutoka Uholanzi .
Huhesabiwa kati ya waanzilishaji wa uchoraji wa
kisasa. Aliacha picha 864 na vichoro zaidi ya
elfu moja na zote alichora katika miaka 10 ya
mwisho wa maisha yake.
Van Gogh alizaliwa mjini Zundert (Uholanzi)
kama mtoto wa mchungaji wa kanisa la
Reformed. Baada ya shule alianza kazi katika
duka la sanaa la mjomba wake. Kazi hii
ilimpeleka pia London na Paris . 1876 aliacha
ajira hii akaendelea kujaribu kazi mbalimbali.
Alifundisha katika shule, alikuwa msaidizi wa
mchungaji wa kanisa, aliuza vitabu. Wazazi
walimshauri kusoma theolojia lakini aliacha
masomo haya tena. Badala yake alitaka kuwa
mhubiri akaajiriwa kama mmisionari kati ya
wafanyakazi maskini katika migodo ya makaa ya
Ubelgiji . Wakati huu alikuwa ameshaanza
kuchora watu na mazingira alimoishi. Alisaidia
wagonjwa na kufundisha Biblia akijitahidi kuishi
sawa na maskini wa mazingira yake. Mtindo huu
ulipingwa na wakubwa wake, akarudi kwa
wazazi kwa muda mfupi halafu akaamua kuishi
kama msanii.
Tangu 1880 van Gogh alikuwa msanii akafuata
kozi ya uchoraji na kufundishwa na mjomba
wake aliyekuwa mchoraji. 1886 alihamia Paris
alipokaa kwa mdogo wake Theo van Gogh
aliyekuwa mfanyabiashara wa sanaa. 1888
alihamia Ufaransa kusini alipokaa hadi mauti
yake. Aliishi pamoja na mchoraji Mfaransa Paul
Gauguin.
Pamoja na kuchora picha nyingi alipatwa na
matatizo ya kiafya hasa ya kiakili na ya kiroho.
Alitibiwa lakini 27 Julai 1890 alijipigia risasi akafa
siku mbili baadaye.
Wakati wa maisha yake hakufaulu wala
hakutambuliwa isipokuwa na watu wachache.
Aliishi katika hali ya umaskini akipata misaada
ya fedha kutoka kwa Theo, mdogo wake.
Katika karne ya 20 picha za van Gogh zilikuwa
maarufu zikauzwa kwa pesa mamilioni ya dollar .
"Huwa naamini Kazi ya ualimu ni kuyafanya magumu kuwa mepesi" mara nyingi huwa najitahidi kufanya hivi.Wewe Humble African kama sio mwalimu inakubidi uwe mwalimu sasa maana huwa nakuelewa sana
ahsante
Mkuu binafsi Nina imani bado na wewe maana najua kwa sasa unakusanya nondo juu yake Van Gogh.Mkuu Humble African Nikushukuru Kwa Elimu Yako Kuhusu Huyu Mtu.
Maelezo Yote Niliyoyaleta Ni Copy & Paste Kutoka Wikipedia Wala Sijaongeza Chochote.Nimekuwa Nikijitutumua Kusoma Kuhusu Binadamu Maarufu Wa Zama Hizo, Hivi Karibuni Nilisoma Makala Moja Iliyohusu ' Top 5 Artists Of All Time '.Hapo Wa Kwanza Da'Vinci , Wa Pili Ni Vicent Van Vogh Na Wa Tatu Ni Michelangelo Na Wengine Wameendelea.
Hao Wawili( Da'vinci Na Miche') Nawajua ( Shukrani Kwako ), Ila Van Gogh Sikujuwa Namjua Na Nilishangaa Kumkuta Akiwa #2.
Hivyo Ikabidi Nianze Kumsoma Kichaa Huyu Japo Nahisi Bado Sijammaliza Ipasavyo Na Niombe Radhi Kwa Kukopi ' Kimakala ' Cha Wikipedia Ambacho Hakija Mtendea Haki Vicent Van Gogh!
Kwa Heshima Ya Jukwaa, Nakuomba Mkuu Humble African Uje Na Nondo Iliyoshiba Juu Ya Huyu Jamaa, Wengine Kwenye Ile List Nitakuletea Pia Upate Kutujuza Kuhusu Waasisi Hawa Wa Sanaa Ya Kisasa!
Ahsante!
Mkuu Humble,Mkuu binafsi Nina imani bado na wewe maana najua kwa sasa unakusanya nondo juu yake Van Gogh.
Naomba ujichallenge kwa kuileta makala murua kuhusu jamaa iliyoshiba zaidi maana unamsoma vizuri.
Ukitaka kumfahamu zaidi sikiliza huu wimbo theme song kutoka kwa Julio iglesias baba yake na Enrique iglesias bad wana mconsider kama the best Spanish Singer of all time. Alimuimba Vincent Van Gogh kwenye wimbo unaoitwa starry starry night ambao ni mchoro maarufu wa Van Gogh but at the same time wimbo huwa wanauita Vincent. Huu hapa https://www.google.com/url?sa=t&sou...DfsQtwIIJTAB&usg=AOvVaw0esaxLii1HcGys-6PzGd5A
Shukrani mkuu! Tunasubiri makala murua kutoka kwako.Mkuu Humble,
Nimepokea Challenge Na Nitajaribu Kumleta Huyu Mtu Kwa Mapana Yake Mungu Akijaalia.
Na Wengine Waliobaki Pia Nitatumia Mwanya Huo Kujijenga Zaidi Kwenye Intelijensia Ya Manguli Wa Sanaa Wa Nyakati Hizo.
Iyegu.
Salute Chief Iyegu.Ahsante Mkuu Humble,
Changamoto Yako Itanifanya Kuwa Imara Zaidi Kwenye Ulingo Huu Wa Jamii Intelligence!
Iyegu
Salute Humble Afric.."Huwa naamini Kazi ya ualimu ni kuyafanya magumu kuwa mepesi" mara nyingi huwa najitahidi kufanya hivi.
Na watu wengi wananiulizaga Kama Mimi ni mwalimu.. Mkuu Mimi sio mwalimu ila napenda sana kuwa mwalimu.. Huwa nafurahi nikiona nimefanya gumu kuwa jepesi na mtu akanielewa that's my pleasure. Bahati mbaya mimi ni janki tu wa mtaani. Just jobless guy!
Nimefurahi kwa compliment yako mkuu. Shukrani sana.
Da'Vinci hata wewe unajua kuandika vizuri mkuu, ile makala yako ya Sananda na genius Da Vinci zilikuwa ni makala bora na elimishi sana.Salute Humble Afric..
Kama kawaida yako hujawahi kuniangusha kwenye Article zako. Sometimes natamani ningekua wewe yaani you so talented in writting and Describing. Kama ningekua nauwezo kama wako ningeandika mengi sana humu JF basi tu.
Msisahau Kuni-tag huo uzi ukitoka,...any of you mwenye atakuwa tayari kumuelezea Vincent
Baada ya kusoma baadhi ya article za Humble African hapa kwanza ile ya Michelangelo aligusia humo ndani uyu jamaa
Nipo interested sana na uyu jamaa nasubiri Humble African afanye yake tumjue uyu 'Crazy Genius'