Vimbwanga na vitisho vya nyumba niliopanga

Atclkwanza

JF-Expert Member
Dec 20, 2015
823
998
Wana JF,

Kuna nyumba nimepanga mitaa yaTabata usiku shida tupu, kukabwa kila siku, nikiamka asubuhi nakutwa nimechanjwa chale mgongoni, kifuani na kwenye mapaja karibu na yale mawe mawili.

Kilichoniogopesha hapa binti yangu usiku wa kuamkia jana amepigwa konzi ameamka analalamika kuwa kuna mtu kampiga konzi bila kumuona na anasikia kichwa kinauma.

Wife wangu ni mlokole sasa yeye ndo shida zaidi ila yeye kuchanjwa hachanjwi ila anaota wanamfukuza na mapanga au wanamtumbukiza kwenye shimo mara zote, huwa anawashida ila akikurupuka pressure inashuka anakuwa hoi.

Wakuu jana usiku nimechelewa kulala kidogo sasa mapaka yakawa yanalia dirishani kwangu kwa sauti ambazo siyo kama paka wa kawaida.

Nikatoa amri kwamba nawajua nyie siyo paka, cha kushangaza nikasikia filimbi ikipigwa hapo hapo dirishani kwangu nikaogopa sana, nikastahimili uoga usinishinde nikatoka nje ya nyumba yangu bila kukuta kitu ila nilihisi kama mtu nimepishana naye mangoni.

Hili suala linanitokea karibu kila siku hasa kuchanjwa chale usiku, ilibibidi nifuatilie historia ya nyumba kidogo ila jibu nililoambiwa na huyo mtu ni kwamba ilikaa bila mtu kwa muda wa miezi sita, nilijaribu kumuuliza ni kwanini ilikaa bila mtu wakati nyumba iko vizuri a kaniambia hajui.

Wakuu kwa sababu nyumba ni ya kupanga nitahama, nimeamua nilete maswaibu hapa ili kama kuna mtu yalishawahi kumsibu au anaidia na haya mambo naomba ushauri wake kwa maswali haya.

A)Kwanini nachanjwa mwilini?

B)Kule kuhisi kama mtu napishana naye halafu simuoni na hili limeekaaje na kuhusu mtoto wangu kupigwa konzi Je?

B)Na wife kukimbizwa na mapanga na kujaribu kumtumbukiza kwenye shimo hili nini?

N:B Kuna mama jirani akimuona mke wangu au mimi anatuogopa kabisa hata tukimsalimia anatuitikia bila kutuangalia usoni hapa ni hisia tu.
 
Binti yako ana umri gani?

Usiniambie, nitakwambia.

Binti yako ana umri kati ya miaka 12 na 14.

Halafu vimbwanga vimetokea.

Vimbwanga ni spirit beings. Vina uwezo wa kufanya mambo hayo kwa kutumia etheric energy ya msichana ambaye hajavunja ungo.

You are not in danger. Hakuna kutoka kwa vimbwanga (poltergeists)
 
Ushirikina ukizidi sana hata mkwaruzo utasema chale na hizo ndoto ni matokeo ya hofu na hisia ambazo akili yako /familia yako inaamini na inatsfiriwa na ubongo wakati ukiwa usingizini
 
Mtangulize mola wako na umuhimidie yeye. Hakuna utachogopa. Huoni mkeo anaafadhali?!
 
Ushauri wangu kwa mtoa mada hapo ulipopanga kuna vita kubwa ya kiroho inayoendeshwa na wachawi cha msingi ni kumkubali Yesu kama mwokozi wa maisha yako au hama.
 
Shyeeeh...!!! Itabidi binti yako umvalishe helmet ya toyo kila ifikapo usiku kwa usalama wa kichwa yake.

Vile vile mkeo umnunulie jezi na viatu vya riadha kuna siku anaweza ota anakimbizwa na John The Rhino km hana vifaa bora atakamatwa nakupigwa pipe tu maana John harembi mwandiko.
[HASHTAG]#John[/HASHTAG] still alive.
 
Chakukushauri hapo mkuu nikuhama tu maadam nyumba sio yako isikutese kiasi hicho nyumba ya mpangaji ipo mfukoni mwake
 
Binti yako ana umri gani?

Usiniambie, nitakwambia.

Binti yako ana umri kati ya miaka 12 na 14.

Halafu vimbwanga vimetokea.

Vimbwanga ni spirit beings. Vina uwezo wa kufanya mambo hayo kwa kutumia etheric energy ya msichana ambaye hajavunja ungo.

You are not in danger. Hakuna kutoka kwa vimbwanga (poltergeists)
Duhh,Nyerereeeeeee...
 
Wana JF,

Kuna nyumba nimepanga mitaa yaTabata usiku shida tupu, kukabwa kila siku, nikiamka asubuhi nakutwa nimechanjwa chale mgongoni, kifuani na kwenye mapaja karibu na yale mawe mawili.

Kilichoniogopesha hapa binti yangu usiku wa kuamkia jana amepigwa konzi ameamka analalamika kuwa kuna mtu kampiga konzi bila kumuona na anasikia kichwa kinauma.

Wife wangu ni mlokole sasa yeye ndo shida zaidi ila yeye kuchanjwa hachanjwi ila anaota wanamfukuza na mapanga au wanamtumbukiza kwenye shimo mara zote, huwa anawashida ila akikurupuka pressure inashuka anakuwa hoi.

Wakuu jana usiku nimechelewa kulala kidogo sasa mapaka yakawa yanalia dirishani kwangu kwa sauti ambazo siyo kama paka wa kawaida.

Nikatoa amri kwamba nawajua nyie siyo paka, cha kushangaza nikasikia filimbi ikipigwa hapo hapo dirishani kwangu nikaogopa sana, nikastahimili uoga usinishinde nikatoka nje ya nyumba yangu bila kukuta kitu ila nilihisi kama mtu nimepishana naye mangoni.

Hili suala linanitokea karibu kila siku hasa kuchanjwa chale usiku, ilibibidi nifuatilie historia ya nyumba kidogo ila jibu nililoambiwa na huyo mtu ni kwamba ilikaa bila mtu kwa muda wa miezi sita, nilijaribu kumuuliza ni kwanini ilikaa bila mtu wakati nyumba iko vizuri a kaniambia hajui.

Wakuu kwa sababu nyumba ni ya kupanga nitahama, nimeamua nilete maswaibu hapa ili kama kuna mtu yalishawahi kumsibu au anaidia na haya mambo naomba ushauri wake kwa maswali haya.

A)Kwanini nachanjwa mwilini?

B)Kule kuhisi kama mtu napishana naye halafu simuoni na hili limeekaaje na kuhusu mtoto wangu kupigwa konzi Je?

B)Na wife kukimbizwa na mapanga na kujaribu kumtumbukiza kwenye shimo hili nini?

N:B Kuna mama jirani akimuona mke wangu au mimi anatuogopa kabisa hata tukimsalimia anatuitikia bila kutuangalia usoni hapa ni hisia tu.

Hizo chale unachanjwa, makovu yanabaki au yanapotea?
 
Mkuu hiyo unayopewa ni warning.. Siku c nyingi watakuchukua Msukule wewe na binti yako.
Hama fasta, hata kama huna hela kopa ukalipe kodi ya chumba kimoja uswazi ili uishi kwa usalama...
 
Kuna hiii michezo wanachezaga wenye nyumba.

Unalipa miezi sita unahamia ,unafanyiwa vituko , ndani ya wiki mbili unahama mwenyewe.

Then mchezo unaendelea kwa mpangaji mpya
 
Back
Top Bottom