Manumbu
JF-Expert Member
- Oct 28, 2009
- 1,746
- 1,282
Kuna jamaa yangu ana biashara ya usafirishaji. ana miliki malori mawili. kila lori lina uwezo wa kubeba tani 20. ila kwa mujibu wa mizani ya Tanzania inabidi kila lori libebe tani 14 ili lisizidi kwenye mizani ya barabarani. siku moja jamaa kabeba kreti za soda toka dar kwenda Tanga. alipopita kwenye mzani pale kibaha maili moja, mzani ulisoma GVM 26,000 ambazo ndo uwezo wa mwisho anaoruhusiwa kuwa nao barabarani. akapita bila matatizo. alipofika Msata kupima akakutwa ana 26,300 GVM. wakaanza kukwaruzana. haiwezekani uzani kuongezeka wakati dizeli imetumika zaidi. na haiwezekani kuongeza mzigo njiani kwani zile soda zote zilikuwa zinapelekwa Tanga kwa order maalum toka kiwandani. Ili kumalizana, ilibidi mwenye gari alipe faini japo faini ilikuwa ya kionezi! wajasiriamali wasafirishaji mmewahi kukutwa na zahma za mizani barabrani? lets share!