Vikwazo dhidi ya Urusi kuanza rasmi leo

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

Rais Vladmir Putin, nchi yake yawekewa vikwazo


Vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi vitaanza rasmi kutumika leo.

Hata hivyo, vitaondolewa vyote au baadhi yake tu mwezi ujao iwapo kutakuwa na maendeleo katika utekelezaji wa mpango wa amani wa Mashariki mwa Ukraine.

Uamuzi wa kutekeleza vikwazo hivi ulifikiwa jana baada ya mkutano wa pamoja kati ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na viongozi wengine mashuhuri wa EU.

Mchakato huu ulicheleweshwa kwa siku kadhaa kwa hofu ya baadhi ya nchi kwamba vikwazo zaidi vitaharibu matarajio ya kusitishwa mapigano.

Vikwazo hivi vipya vinayalenga makampuni ya mafuta ya Urusi, sekta za fedha na ulinzi.

Pia wameongeza majina mengine 24 katika orodha ya maafisa wa Urusi na viongozi wa waasi nchini Ukraine ambao wanakabiliwa na kunyimwa visa na kuzuia mali zao.


Chanzo
:BBC

http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/09/140912_vikwazo_umojawaulaya_urusi
 
Hii ngoma Russia sijui ataichezaje.
 
Nina uhakika russia anajua cha kufanya, they are the best in this
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…