Vijibweni wataka tathimini mpya ya mradi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijibweni wataka tathimini mpya ya mradi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sir.JAPHET, Aug 18, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nora Damian
  DIWANI wa Kata ya Vijibweni,wilayani Temeka, Seleman Mathew ,ameiomba Serikali kufanya upya tathmini ya mradi wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni, ili kuwatendea haki wananchi.Alisema mwaka 2008 Serikali ilitoa amri kwa wakazi wa eneo hilo kutoendeleza makazi yao.

  Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa vya ofisi kwa ajili ya ofisi ya Kata ya Vijibweni, Mathew alisema baada ya amri hiyo kwisha wananchi wengi walianza kuendeleza ujenzi wa nyumba zao.
  “Wananchi wanautaka mradi lakini kuna haja ya wao kushirikishwa katika kutoa maoni yao ili mradi huo uweze kufanikiwa,”alisema Mathew.

  Diwani huyo alikabidhi vifaa vya ofisi ikiwemo kompyuta moja, saa na kuweka umeme katika ofisi hiyo na vitu hivyo vyote vimegharimu Sh2.3 milioni.

  Mmoja wa wananchi wa eneo hilo, Zainabu Fatawi, aliiomba Serikali ijipange upya na kwenda kukutana nao kwa sababu amri iliyotolewa tayari ilishapitwa na wakati.“Hakuna ambaye hapendi maendeleo lakini wanapokuja waanze tathmini upya kwa sababu watu wameshajenga,”alisema Fatawi.

  Katika hatua nyingine, diwani huyo alisema anakusudia kukutana na kampuni zinazojishughulisha na na biashara ya mafuta katika eneo hilo, ili kuzitaka zichangie shughuli mbalimbali za maendeleo.
   
 2. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wanautaka mradi wasioujua? Wakaulize wenzao waliokuwa Kipawa
   
 3. M

  Mgelukila JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Diwani aache sanaa aseme yeye anataka tathimini baada ya kuanzisha ujenzi mpya miezi miwili iliyopita kwa kujenga guest house, frem za biashara, bar ya kufa mtu, ofisi na studio ya kurecodi mziki. Anategemea kuzindua bar na guest idd mosi sasa kama kiongozi anatambua zoezi la kuhama kwanini ajenge sasa? Mbona hajawatangazia wananchi wajenge? Anataka tathmini mpya ili achote mabilioni? Uko wapi uadilifu wake? Anakashifa ya kuziba njia mtaani kwake ameshindwa kuvunja ukuta uliofunga njia ktk bar ya malaika pub kwa kuwa naye anatatizo hilohilo, mikutano anayoitisha hataki kuulizwa maswali amekuwa mtu wa magazeti kuficha ukweli. Aache unafiki hana dhamira ya dhati kwa wakazi wa vijibweni.
   
Loading...