Vijana wazelendo vyuo vikuu wamshukia Mbowe

Vijana wazelendo vyuo vikuu wamshukia Mbowe

von Meshak

Member
Joined
Aug 20, 2014
Posts
12
Reaction score
3
Sisi ni vijana wasomi wazalendo kutoka
vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko Dar es
Salaam, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM); Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU); Dar
es salaam University College of Education
(DUCE); USTAWI WA JAMII; Chuo Kikuu
cha Mtakatifu John (St. John); Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM); Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania (OUT); Kampala
International University (KIU); Dar es
Salaam Institute of Technology (DIT);
Institute of Adult Education (IAE);
Tanzania School of Journalism (TSJ);
College of Business Education (CBE), Chuo
cha Uhasibu (TIA) na Chuo cha
kumbukumbu ya Mwl JK Nyerere.
Tunachukua fursa hii kulaani vikali kauli
zilizotolewa na Mh. Freeman Mbowe
ambae ni Mwenyekiti wa CHADEMA ya
kutaka kuitisha maandamano ya nchi
nzima bila kikomo pamoja na
kuhamasisha asasi nyingine za kiraia
kufanya na kuratibu maandamano kama
hayo ya CHADEMA kwa ajili tu ya kupinga
kuendelea kwa Bunge Maalumu la Katiba.
Tunawaambia watanzania wenzetu kuwa
tumekerwa na kusononeshwa sana na
kauli ya kibabe ya kiongozi huyu wa
CHADEMA ya kuhamasisha vurugu
ambazo tumezishuhudia zikisambaratisha
umoja wa nchi nyingi na kuwa chanzo cha
vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo
huwa haviishi na hatimaye kuendelea
kulipakazia Bara la Afrika kuwa
halijastaarabika na siasa za kidemokrasia.
Tulimsikia akiahidi maandamano bila
kikomo kwa kibali cha polisi au bila kibali
cha polisi mbele ya wajumbe ambao
wengine sio watanzania.
Ndugu watanzania wenzetu, kauli kama hii
haiwezi kusemwa hata na Rais yeyote
ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu anaeongoza
kwa kufuata misingi ya sheria na utawala
bora, je Mh. Mbowe anapata wapi uhalali
na ujasiri huo? Maana Rais na Amiri Jeshi
Mkuu ambae ni dikteta anaweza kusema
lakini yule anaetawala kwa misingi ya
sheria, katiba na utawala bora kamwe
hawezi kusema kauli kama hizo.
Maneno aliyoyasema Mh. Mbowe
amejivalisha madaraka zaidi hata ya yale
ya Rais wetu ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu
wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama. Lakini
kwa mtazamo wetu ni kuwa Mh. Mbowe
amejivalisha UDIKTETA ambao unatakiwa
kulaaniwa na kila mtanzania aliyeko
ndani na nje ya nchi hii. Uzito wa kauli
zake haubebeki na mtu yeyote kwenye
taifa hili. Hatuna shaka kuwa ametoa kauli
mbaya sana kuliko zote za kisiasa ambazo
zimewahi kusemwa majukwaani.
Watanzania kwa ujumla wetu na makundi
yetu tukikaa kimya bila ya kuzilaani na
kuzikemea vikali kauli zake, tutakuwa
hatujitendei haki sisi wenyewe na pia
hatutavitendea haki vizazi vijavyo vya nchi
yetu. Ndugu zetu watanzania, kama
ambavyo yeye mwenyewe alisema kabla
ya kutoa amri kwa watu kuandamana
kuwa anaamini watanzania wapo tayari
kufanya mageuzi ili chama chake kingie
IKULU ya Magogoni.
Hayo yatafanikiwa endapo tu vijana
wataacha uoga, maneno ambayo
yanaashiria kutaka kuchukua uongozi kwa
nguvu bila kufuata misingi ya
kidemokrasia inayosimamiwa na serikali
iliyo madarakani.
Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo
vya elimu ya juu Dar es Salaam tunasema
kuwa uzito na ubaya wa kauli hizi
unaonesha wazi kuwa Mh. Freeman
Mbowe hafai kupewa dhamana ya kuwa
Rais wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa
vikosi vya ulinzi na usalama na pia
amedhihirisha kuwa CHADEMA haina sifa
ya kuiongoza nchi hii kwa sasa kwa
kufuata misingi ya demokrasia na
kudumisha amani, utulivu na mshikamano
wa watanzania kwa lengo la kudumisha
umoja, na muungano wetu.Tunaomba
watanzania mkumbuke na mtilie maanani
kuwa, Mh. Freeman Mbowe katoa kauli
hizi akiwa raia tu wa kawaida.
Je itakuwaje akiwa Rais wa nchi na Amiri
Jeshi Mkuu wa Vikosi vyetu vya Ulinzi na
Usalama wa nchi hii? Kwa maoni yetu ni
kuwa kwa upeo na mtazamo wa akili yake
hakuna atakaebaki salama ndani ya nchi
hii kwa kuwa atatuingiza kwenye vita vya
wenyewe kwa wenyewe na pia atatuingiza
kwenye vita na nchi majirani. Hafai, hafai,
hafai hata mara moja kuwa Rais na Amiri
Jeshi Mkuu.
Ndugu watanzaia, hivi ni mtu gani
anaeweza kuishi kwa amani na viongozi
kama Mbowe na wenzake wanaotumia
ubabe kwenye maisha ya kawaida ya kila
siku?
Na hapa ndipo wanatuthibitishia kuwa
Mh. Freeman Mbowe na Kikundi cha
viongozi wa chama chake wote karibu
wameshindwa kuzichunga na kuziweka
pamoja familia zao na hatimaye
zimesambaratika kwa ubabe huo huo,
hivyo hawataweza kutuongoza na
kutuweka pamoja watanzania ili tuishi
kwa amani.
Ndugu watanzania wenzetu tumebaini
kuwa Mh. Freeman Mbowe na viongozi
wenzake wa CHADEMA wanatumia
maandamano na damu za watanzania
kutafuta fedha kwa wafadhili wao ambao
hawaitakii mema nchi yetu.
Wakiaandaa maandamano, wanapiga
picha na kuwapelekea wafadhili wao,
wanapata fedha, wanajenga majumba na
kununua magari ya kifahari na kusafiri
ulaya, marekani na familia zisizo rasmi
kwa kujificha kwenye pazia la
DEMOKRASIA huku watanzania
wakiendelea kuathirika na maandamano.
Hapo ndugu watanzania hakuna
DEMOKRASIA bali tunaona DOMO-KRASIA
na BONGO-KRASIA, yaani wanatumia
ulimi na akili ndogo za kitoto kujinufaisha
na familia zisizo rasmi kwa siasa za
ulaghai, ghilba, fitina, majungu, choyo,
chuki, usanii wa kisiasa na uhaini
alioutangaza Mh. Mbowe.
Ndugu zetu watanzania, fahamuni kuwa
Mh. Freeman Mbowe, Dk. Wilbroad Slaa,
Tundu Lissu, Godless Lema, Mchungaji
Peter Msigwa, Hezekiah Wenje na wengine
wana familia. Swali je mmeshawahi
kuwaona wake, watoto, na ndugu zao wa
karibu kwenye maandamano yoyote yale
waliyowahi kuyaandaa? Siku zote
huwaambia watu wao
hao bakini majumbani mtadhurika.
Pale damu za watanzania zinapomwagika
kwenye maandamano baadae huwa
wanajifungia na kushangilia ushindi
mkubwa wa kuvuna mabilioni ya fedha za
kigeni, kwa kuwa huwa wanapiga picha
matukio hayo na kwenda kuonesha
wafadhili wao kwa taswira kwamba
demokrasia inanyanyaswa.
Wanakinga mabilioni ya fedha za kigeni
wanatia kwenye akaunti zao,
wanagawana, na mambo yao yanaenda
sawasawa, huku watanzania wengine
wakiwa wana vilio vya kupoteza ndugu na
baba zao, waume, wake, wapenzi/
wachumba, na watoto wao na kadhalika.
Swali, kwanini hawaoni umuhimu wa
kujali utu, ubinadamu na uhai wa
watanzania wengine? Sisi umoja wa vijana
wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar
es Salaam tunapenda kuwahakikishia
kuwa thamani ya maisha ya watanzania
wote au hata kwa mtanzania mmoja ni
kubwa sana kuliko hiyo katiba mpya
wanayoidai.
Tunawaomba watanzania wenzetu
msikubali kufanywa kama mbuzi wa
kafara na watu wenye tamaa, pupa,ulevi,
na uroho wa madaraka kama hawa akina
Mbowe na kundi lake. Tusijiendee tu kama
kuku aliekatwa kichwa halafu akaachiwa
atembee, na tusishikiwe akili zetu kama za
mbayuwayu kwani “Akili za Kushikiwa,
ongeza na zako”. Tuwakataeni wanasiasa
uchwara waliofilisika kihoja na kutaka
kuwatumia ili kujinufaisha.
Wanataka kutupeleka wapi? Ni dhambi
isiyosameheka kulitumbukiza taifa hili
katika machafuko yenye majuto makubwa
kama ya Misri, Syria, Afrika ya kati, Libya,
Sudan ya Kusini na kwingineko.
Tusikubali watupeleke huko, waacheni
waende wenyewe kama wanaweza. Kwani
nchi yetu ina mgogoro wa kisiasa?!!!!!
Waulizeni wanataka nini?
Ndugu watanzania wenzetu, tunaomba
mjue kwenye nchi hizo hizo zenye
demokrasia pevu watu wa aina ya Mh.
Freeman Mbowe (hasa kwa kauli zake
alizozitoa juzi tarehe 14.09.2014)
wanaotaka kuvuruga na kuvunja misingi
mikuu ya utaifa wao (core values) kama
vile amani, usalama na umoja huwa
hawavumiliwi hata kidogo.
Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo
vya elimu ya juu Dar es Salaam
tunaviomba vyombo vyetu vya dola
visizivumilie kauli kama hizi zilizotolewa
na Mh. Freeman Mbowe hata mara moja.
Kwani vyombo vya dola vina dhamana ya
kulinda, kutunza na kuendeleza amani na
utulivu wa nchi yetu. Umoja wetu, kwa
heshima na taadhima
kubwa, tunaviomba vyombo hivi
kumchukulia hatua kali za kisheria Mh.
Mbowe kwa kauli hii ya kutishia uvunjifu
wa amani kabla hajaiingiza nchi yetu
kwenye machafuko ya kisiasa.
Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo
vya elimu ya juu Dar es Salaam hatutaki
kuona vijana wenzetu na watanzania wote
kwa ujumla wakiathirika kwa ujinga huo
wa maandamano yanayofanywa mradi wa
kutafuta fedha.
Kwani maandamano hayo yatawaathiri
wana vyuo wa Dar es Salaam pamoja na
kuathiri shughuli nyingine za kiuchumi, na
kijamii za wananchi wa kawaida. Kwa nini
shughuli zetu na za wananchi zisimame
kwa sababu tu ya machafuko ili Mh.
Mbowe apate picha za kwenda kuuza huko
kwa wafadhili wao?
Sisi umoja wa vijana wazalendo wa vyuo
vya elimu ya juu Dar es Salaam tulisikiliza
na kutazama hotuba ile kwa umakini wa
hali ya juu,tunapenda kuwathibitishia
kuwa hotuba ile haikuwa ya kisomi,
ilikuwa haijengi chama chake wala ilikuwa
haijengi nchi yetu isipokuwa ilikuwa ya
kibabe, ilikuwa ya kejeli,ilikuwa ya
kichochezi iliyolenga kuvunja misingi ya
amani na utulivu wa nchi yetu.
Ni matumaini yetu kuwa hata kwa
mwanafunzi wa shule ya msingi hawezi
kujifunza kitu chochote cha maana kutoka
kwenye hotuba ile. Hotuba ya Mh. Mbowe
haiwezi kutusaidia kujenga taifa lenye dira
kwa vizazi vijavyo.
Mwisho, Sisi kama umoja wa vijana
wazalendo wa vyuo vya elimu ya juu Dar
es Salaam, tunawataka watanzania
wenzetu mzipime na kuzitafakari kwa
makini kauli za Mh.Mbowe, na kujiuliza je
anafaa kuwa kiongozi wa nchi hii?
Asanteni kwa kutusikiliza, Mungu Ibariki
Tanzania, Mungu Ibariki Afrika Imesomwa
na Mussa Omari, Mwanafunzi OUT, kwa
niaba ya umoja wa vijana wazalendo wa
Vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam.
Tarehe 17.09.2014
 
waache ujinga mbona mafisadi hawawashikii mabango?
:angry::angry::angry:
 
Hatuwashangai kwani hata kipindi cha utumwa wabantu ndiyo waliokuwa wanawakamata waafrika wenzao na kuwapelekea waarabu ili wakauzwe utumwani kwa URIJA wa shanga,tende na halua tu!!!!!!!
 
Nilikuwa napita ,Kumbe nao wasomi hawana akili, yani wanapost upumbavu, ni bora tusio soma.
 
dah kweli njaa mbaya,mbona hatukuwackia kipind kile wazir mkuu alipowahamasisha polisi wawapige raia? mbona hatukuwackia kipind kile John komba aliposema ataingia msituni endapo zitapitishwa serikal 3?ACHENI UNAFIKI
 
Ah wasomi malizeni huko vyuoni tunawasubiri huku na vyeti vyenu tuwe wwote machinga pamoja na hayo makaratasi yenu myaitayo vyeti. Hiyo buku unayopokea haikufikishi mbali maana haitamnunulia mwanao hata kalamu endapo utaamua kumpata.
Funguka usije ukajutia huu muda wako wa wa kuipigania haki yako na huifanyii kazi. Usikubali kuitwa mjinga maana una nafasi na nguvu za kupigania haki yako na huitumii ni nani atakupigania wewe upokee vibahasha? Kipindi kile cha Nelson Mandela watu wa fikra zako walimwona ana kiherehere na anawapotezea wananchi muda wao, mbona sasa nchi nzima wanamwita tata Mandela? Nakusikitikia unayejiita msomi unashindwa kuiona kesho ina nini kwako na kwa uzao wako.
 
Niwape habari za huyo Musa OMaRI? Ni mpishi pale Mnazi mmoja kaambiwa akaongeze Elimu ili afikiliwe promotion mtayasikia mengi kutoka kwake
 
Sisi ni vijana wasomi wazalendo kutoka
vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko Dar es
Salaam, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM); Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU); Dar
es salaam University College of Education
(DUCE); USTAWI WA JAMII; Chuo Kikuu
cha Mtakatifu John (St. John); Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM); Chuo Kikuu
Huria cha Tanzania (OUT); Kampala
International University (KIU); Dar es
Salaam Institute of Technology (DIT);
Institute of Adult Education (IAE);
Tanzania School of Journalism (TSJ);
College of Business Education (CBE), Chuo
cha Uhasibu (TIA) na Chuo cha
kumbukumbu ya Mwl JK Nyerere. .......[snip]

..........................Imesomwa
na Mussa Omari, Mwanafunzi OUT, kwa
niaba ya umoja wa vijana wazalendo wa
Vyuo vya elimu ya juu Dar es Salaam.
Tarehe 17.09.2014

Hao ndo wanaojiita vijana wasomi. Matatizo ya div.5. wale ambao hata wakiitwa interview hawajui jinsi ya kujitambulisha. Ktk nchi hii imekuwa ni kawaida kwamba wasio na sifa za kielimu kuwafanya wajiunge na vyuo vya maana au kutosha kuwapatia kazi, hulazimika kujiunga na CCM ili iwe ndo sifa ya kulazimisha. Yaani ukishasema ni mwana CCM safi basi ubebwe bila kitu kichwani. Ndo hawa!

Ndo hawa ambao hawana ajila lakini hawajitambui. Hawathaminiwi lakini hawajitambui. Sasa wameibuka na uzalendo, sijui kama wanao, lakini hilo la usomi nina hakika hawana kabisaaaa!

Hebu angalia huyu naye aliyeleta mada;
Jina: von Meshak
Join Date : 20th August 2014
Posts : 9
Rep Power : 306
Likes Received:1
Likes Given:0

Ameandika posts 9 lakini bado hajui kupanga maneno hapa JF. Aya ni nusu nafasi ya ukurasa alionao. Nahisi naye ni kijana mzalendo msomi anayeaminiwa kwenye kundi, sasa kaambiwa peleka, we ndo kiboko! Hivi! Hopeless!
 
Vijana wazalendo? vyuo vikuu?
hapa hakuna uzalendo ni ushabiki maana kama nikauli kali zilishatoka kauli kali na chafu chama tawala mfano,serikali 3 zikipita naingia msituni,kushitaki mahakamani nisawa nakumpigia mfalme mziki ili acheze,wapigwe tu,tutawatia adabu,na hili lakuwapiga waandishi wa habari haliashirii uvunjifu wa amani? kama nyie ni wazalendo mlitoa kauli gani?achen ushabiki hakuna cha uzalendo.
 
mnaojiita wasomi endeleeni kuwa walamba nyayo na vikaragosi wa ccm, malizeni hivyo videgree vyenu muje mtaani na kuingia kwenye jeshi la wasio na ajira
 
Hakuna wanazuoni wajinga kama huyo aliyeweka post hapa juu na isitoshe we mjinga kama baba yako sita tena tunaomba usitupost vitu vibovu kama hivyo we mjk
 
Msomi hufuta tamaa zake, matamaniyo yake, matakwa yake, mihemko yake na mahitaji yake. Baada ya hapo hufanyia kazi facts kwa kutumia historia, kilichopo na tarajiwa. Halafu hutoa facts pamoja na faida zake na hasara zake na mwisho hutoa tahadhali kwa makundi ya faida na hasara. Msomi hakurupuki kwa matusi na kutegemea nguvu za umma. Uzalendo, busara na subira ndiyo umenisukuma kuandika haya.
 
migomo nchi nzima,harakisheni,wasioenda makazini kwao wengine wanaajiriwa haraka,kuna mamilioni wanatafuta kazi,nyie fanyeni mgomo. Nadhani Mbowe na jamaa zake hawajiamini,kwani mtu wa mwisho wa kupitisha hiyo rasimu si mwananchi? Kama Ukawa na Mbowe wana hakika ya rasilimali watu ni kwa nini hawawaandai wananchi kukataa hiyo hiyo rasimu? Nadhani hayo maandamano yana manufaa binafsi kwa wanasiasa.
 
Hakuna wanazuoni wajinga kama huyo aliyeweka post hapa juu na isitoshe we mjinga kama baba yako sita tena tunaomba usitupost vitu vibovu kama hivyo we mjk

Mm nadhani kila mtu anayo haki ya kutoa maoni yake humu jf, shindaneni kwa hoja sio kwa matusi, kulazimisha wengine wakubaliane na mtazamo wako sio sahihi sana ,toa hoja ijadiliwe
 
ndiyo wasomi tena wazalendo wamesema kweli hata sisi ni wananchi wa nnchi hii, maana wengine mnajiona eti ndio wananchi?

Tatizo la mtandao. Hata asiye na meno hucheka bila kuziba mdomo.

sauti ya kijiji
Join Date : 9th August 2014
Posts : 2
Rep Power : 0
Likes Received 0
Likes Given 0
 
Back
Top Bottom