Vijana wanawezeshwa vipi katika kujiajiri

zema21

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
619
251
Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri
Inafahamika kuwa ukosefu wa ajira ni tatizo si kwa Tanzania tu bali hata kwa nchi zilizoendelea kama Marekani. Kwa hapa Tanzania limekuwa si tatizo bali ni janga kubwa ambalo hakuna anayelitafutia ufumbuzi wala kulitupia macho. Itakumbukwa kuwa siku za nyuma mbunge ambaye pia alishawahi kushika nyadhifa za juu serikalini alinukuliwa akisema kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu linalosubiri kulipuka muda wowote. Baada ya muda serikali kupitia waziri wake ilikanusha kuwa si tatizo ikatoa takwimu zilizoonyesha kupungua kwa tatizo hilo; lakini baada watu mbali mbali kukosoa vikali takwimu hizo ndipo raisi wa Jamhuri ya muungano alikiri wazi kuwa ukosefu wa ajira ni tatizo.

Hivi sasa serikali inakuja na jibu moja rahisi saana juu ya janga hili kwa vijana kuwa "vijana mjiajiri". Wanatoa jibu hili pasipo utafiti wowote wala ushauri wa kitaalamu, njia bora za vijana kujiajiri na bila kujali changamoto katika kujiajiri, hali halisi ya vipato vyao, uwezo wao kujiajiri na mambo mengine ambayo ni changamoto. Elimu waliyoipata peke yake haitoshelezi kumpa fursa kijana huyu ya kujiajiri.Ndio maana hata katika taasisi mbalimbali tunakuta watu wenye PhDs, professor nao wakiwa wameajiriwa au wanaomba ajira, kwanini wao wasijiajiri kwa kutumia kigezo cha elimu yao? Leo graduate anaambiwa ajiajiri.

Kumfanikisha kijana ajiajiri anahitaji awe mtaji (Capital), ambapo hapa atapata fedha za

  • Fedha za usajili na kupata lesseni ya biashara
  • kupanga ofisi, kupata samani (furniture) za ofisi,
  • vitendea kazi,
  • fedha za kuendesha ofisi kwa miezi kadhaa mpaka pale business itakapata uwezo wa kujiendesha.

Hapo usisahau kuwa huko TRA wanapotoa TIN na leseni na BRELA wanaosajili kampuni au jina la biashara yako, wana ubabaishaji na uswahili mwingi sana wakitengeneza mazingira ya kutaka kupewa mlungula, usipotoa basi itachukua hata miaka miwili kumalizana na nao.

Leo hii mhitimu fresh kutoka chuo anaambiwa ajiajiri pasipo kuangalia changamoto anazokabiliana nazo, mahitaji katika kujiajiri na mambo mengineyo, hivi hii si kejeli kwa vijana hao? hivi kweli tunafikiria? Kama tunafikiria tunatumia nini kufikiria? Nywele, akili au tunatumia vile viungo vile alivyovisema dr masaburi? Vijana kama wangekuwa na uwezo huo wa kifedha ni dhahiri kwamba wasingeomba hata mkopo katika kupata elimu ya juu; wangejisomesha wenyewe. Huku ni kuwatelekeza vijana hao na kuonyesha kutokuwajali kwa tatizo linalowakabili. Matokeo yake utawakuta wengi wakishahitimu masomo wanakimbilia kwenda Dar es Salaam wakiamini huko watapata kazi, badala yake huko utawakuta wanapishana katika taasisi mbali mbali wakitembeza CV zao hususani katika bank, recruitment agency na taasisi nyinginezo, wakiwa wamechoka, wamekata tamaa, huku hawana hata fedha ya kununulia maji ya kunywa baada ya mizunguko mirefu. Huku nako CV zao huchanwa na kutupwa. Kuna kipindi nilihoji kwanini wanachana CV za watu nilijibiwa kuwa kwa wiki moja unaweza kupokea CV za watu 200 tofauti kwa mwezi zinaweza pelekwa mpaka CV 1000 so wanakosa pa kuzitunzia.

Kuna tabaka la Watoto vigogo hawa huwa hawajui wala hawajawahi kuguswa na matatizo yanayowakabili vijana wengine, hawa ndio ambao ni wafanyakazi katika taasisi kubwa kubwa na nyeti kama vile N.S.S.F, BOT, TRA, BANDARI n.k tena mara baada ya kuhitimu masomo yao. Hata siku moja haijawahi kusikika kuwa kuna mtoto wa kigogo ambaye ni mwalimu, nesi au afisa kilimo. Hawa huwa ndio mabosi au wafanyakazi wa ngazi za juu katika tasisi kubwa kubwa zenye malipo manono.

Hakuna chombo cha kuwatetea vijana au kuwaunganisha vijana ambao wanatokea katika familia za kawaida na za chini, kuwasaidia katika matatizo mbali mbali, hapo mwanzoni iliahidiwa kuwa lingeundwa jukwaa la vijana lakini imekuwa ni ahadi isiyotekelezeka. Ndio maana wengi wao wanakosa pa kwenda kuzungumza au kusemea matatizo yao wanaishia kuwa walalamishi tu katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Serikali inasema kuwa kuna fedha zimepelekwa kila halmashauri kwa ajili ya vijana wanaotaka kujiendeleza, ukienda huko halmashauri utaambiwa ujiunge na saccos ndipo uweze kukopa fedha hizo, na inafahamika wazi kuwa sharti la kukopa katika hizo saccos ni kuweka kwanza ndipo ukope, tena unaweka 1/3 ya kile unachotaka kukopa, mathalani unataka kukopa milioni 3 lazima uweke milioni 1 ndipo ukope hizo tatu. Sasa huyu mhitimu ambaye ametoka kwenye familia ya kawaida ambayo inamtegemea amemaliza chuo ndio aje kuwakomboa ataweka fedha toka wapi?

Kwa mtindo huu vijana tunabaki kukosa dira,tunaendelea kuwa walalamishi kama mzazi wako hajawi kuwa kigogo wa taasisi yeyote ile basi utaendelea kuwa chini na wale wenye nacho watazidi kuongezewa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom