Kwa kipindi kirefu sasa nimeshuhudia vijana kadhaa wa vyuo/shule wakipoteza mwelekeo kwa kupelekwa mahakamani kujibu tuhuma za makosa mbalimbali ya kukashifu viongozi kwenye mawasiliano yao ya kawaida.
Kijana wa shule ni vizuri akajikita zaidi kwenye mambo muhimu ambayo yatafanikisha ndoto za maisha yake. Kujiingiza kwenye jambo lolote amabalo linaweza kukwamisha ndoto zako za maisha ni uzembe wa hali ya juu. Leo tumesikia kuna vijana wa Chuo cha Kampala - Dar wakiwa wamefikishwa mahakamani kwa kuhusishwa na vikatuni ambavyo vimeonekana ni udhalilishaji kwa mkuu wa nchi.
Sijajua kwanini wanachuo hawajaelewa haya mambo, kiasi cha kuwa wahanga wakuu kwenye hili tatizo. Inawezekana wanachuo wengi hawana taarifa za makosa ya kimtandao. Wakati fulani niliwauliza wanachuo fulani namna ambavyo wanatumia vyombo vya mawasiliano kama TV na Radio ili kujua dunia inaendaje, nilichokigundua ni kuwa wengi hawana muda wakuangalia vipindi vya taarifa ya habari na wamejikuta kwenye taarifa nyingine za whatsap, facebook n.k, na baadhi yao ambao simu zao ni za kawaida wamejikita zaidi kuangalia picha za tamthiliya n.k, pengine wanachuo wa aina hii ndiyo wanaojikuta kwenye matatizo.
Sidhani kama mwanachuo makini mwenye kujua na kufuatilia mambo hasa ya nchi hii anaweza kunaswa kwenye shida za namna hii. Wito kwa wanachuo/wanafuzi ni kuwa wajikite sana katika mambo ambayo yatawasaidia kwenye maisha yao kuliko kujiingiza kwenye shida ambapo hata wazazi wao baadaye wanajikuta wako kwenye shida maana mchuma janga hula na wakwao.