Vijana wa siku hizi mnatoa wapi pesa?

Vijana wa siku hizi mnatoa wapi pesa?

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
31,676
Reaction score
81,663
Ukweli vijana wa siku wamefanikiwa sana zamani wazee wetu walikuwa wanaajiriwa au wanajiajiri lakini walikuwa wakiishi kimsoto msoto sana.

Lakini vijana wa siku hizi unawakuta wanamiliki nyumba hapa mjini pamoja na kumiliki mikoko ya maana huku kila weekend hawakosi kuchoma nyama.

Japo kuna vijana wengine ni msoto lakini baadhi yao wako vizuri kama hawa vijana ambao wamefanikiwa wakiamua kuwapiga tafu wenzio mambo yangekuwa bamba to bamba.
 
Maisha ni mipango mkuu, fursa zipo za mikopo n.k, vijana wa zamani walikuwa wanategemea pesa ya kustaafu kwa walioajiriwa, vijana wa sasa hawana uhakika kama watafikia huo umri wa kustaafu kwa hiyo inawalazimu waishi maisha yao ipasavyo wafurahie na wale bata mapema
 
Ajira zimekua nyingi kutokana na kukua kwa uchumi wa nchi kwa muda wa zaidi ya miaka kumi sasa hivo sekta nyingi zimeajiri vijana wengi sana. Kumbuka nchi yetu bado gharama za maisha ni chini hivo ukipata kazi nzuri unaishi kama mfalme.
 
Ngoja waje watueleze vizur.
Ingawa mara nyingi husingizia kuwa wanafanya kaz kwa bidii na kujituma tu.
 
Ukimwonaa kijanaa mkingaa mjini ana helaa ujue kashamfanyaa mama yake chizii au kashatoaa kafaraa Kwa MTU yyt ktkt familiaa yaan wakinga wana roho ngumu haoo
 
Ajira zimekua nyingi kutokana na kukua kwa uchumi wa nchi kwa muda wa zaidi ya miaka kumi sasa hivo sekta nyingi zimeajiri vijana wengi sana. Kumbuka nchi yetu bado gharama za maisha ni chini hivo ukipata kazi nzuri unaishi kama mfalme.
Nchi ya viwandaa baba,viwandaa n vingii kilaa kona tutakosajee ajiraa na tunalipwa mishaara minono
 
Wengi wao vijana wanaishi hawaangalii maisha ya baadae hivyo wanaigiza maisha utakutana na kijana kavaa jeans 30k viatu 100k koti la 70k simu ya 600k hana ishu yoyote mjini bia kila siku za ofa ukimuona unaweza sema pesa zipo afu anakwambia sina mtaji magu kabana
 
Wanafanya kazi na wako focused!
Wameamka usingizini, sio wahindi na wamanga tu ndiyo wenye uwezo wa kushika Pesa!
 
Tanzania ya viwanda kwasasa kuna viwanda 3000+
Uchumi wa viwanda
Tunapata hela kwa kufanya kazi viwandani
 
Back
Top Bottom