Vijana wa Shia na Suni waswali pamoja eneo la mauaji

Sinoni

JF-Expert Member
May 16, 2011
6,193
10,680
4bk5362ec6c8b87x7d_800C450.jpg

Vijana wa madehebu mbili za Kiislamu za Shia na Suni wamekusanyika katika eneo la Karradah mjini Baghdad ambalo siku chache zilizopita lilishambuliwa kwa mipuko ya magaidi na kuswali swala ya pamoja ili kuonesha mshikamano wa Kiislamu na upinzani wao dhidi ya siasa za kutenganisha Waislamu za kundi la kitakfiri la Mawahabi wa Saudi Arabia.

Makumi ya vijana wa Kishia na Kisuni walitekeleza kwa pamoja Swala ya jamaa ya Magharibi jana jioni katika eneo hilo la Karradah ambalo Jumapili iliyopita lilikuwa mithili ya mto wa damu baada ya magaidi wa kundi la Daesh kushambulia soko la eneo hilo kwa mabumo na kuua zaidi ya watu mia mbili wasio na hatia.


Mashambulizi hayo ya kundi la Daesh yaliyolenga Waislamu katikati ya jiji la Baghdad tena katika mwezi mtukufu wa Ramadhani yamelaaniwa na taasisi mbalimbali kote duniani.


Waziri Mkuu wa Iraq Haidar al Abadi ameapa kulipiza kisasi cha mauaji hayo ya Waislamu wasio na hatia na kutangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kote nchini Iraq.


Watu wasiopungua 200 wameuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi hayo.



Vijana wa Shia na Suni waswali pamoja eneo la mauaji - Pars Today
 
... kulipiza kisasi kwa mauwaji ya waislamu wasio na hatia ... Statements za aina hii huwa sizielewi. Ni mauwaji ya akina nani ndio halali?
 
Back
Top Bottom