Vijana wa sasa na mapinduzi

Vijana wa sasa na mapinduzi

siara

Member
Joined
Jan 4, 2012
Posts
33
Reaction score
4
Nimekua nikiwaza juu ya msimamo wa vijana wa
leo na mageuzi yanayohitajika katika nchi yetu.
Vijana wa zamani yaani kina Julius K
Nyerere,Zuberi, Kawawa, Malcom X, Che Gue,
Nkurumah na wengineo waliowahi kufanya
mageuzi ya kweli katika wakati wao,msimamo
ndio ilikuwa silaha kuu ya mapambano yao na
mafedhuli wa wakati huo. Wala ushindi wao haukutokana na pesa wala mali ya aina yoyote
ile.
Vijana wa leo wameamua kuuvua utu wao na
kuvaa taswira ya bidhaa ya bei nafuu kama vile
nyanya,kitunguu,carrot,hoho n.k. Vijana wa leo
tunataka kujiaminisha kwamba eti heshima,adhama na hiba inapatikana kwa kupata
pesa nyingi na hivyo tumeamua kuwa kama
tulivyo. Mwaka 2015 ni mwaka ambao wengi
watategwa na kutegeka, ungana na mimi
kukemea huu utumwa wa fedha mpka mtu
kujivua utu wake.
 
Back
Top Bottom