Vijana wa Mwema waua tena! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wa Mwema waua tena!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kupelwa, Sep 1, 2012.

 1. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  na Igenga Mtatiro, Tarime | Tanzania Daima - Sept 01, 2012


  JESHI la Polisi limeingia katika kashfa nyingine tena, baada ya askari wake kuwaua kwa risasi watu wawili na kuwajeruhi wengine kadhaa katika vurugu zilizozuka wakati wa jaribio la kuwaondoa wananchi wanaodaiwa kuvamia eneo la Nyamongo la mgodi wa North Mara unaomilikiwa na Kampuni ya Africa Barrick.

  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya, Justus Kamugisha alikiri kutokea kwa mauaji hayo akisema watu hao waliuawa kwa kupigwa risasi za moto na mmoja kujeruhiwa majira ya jioni juzi katika mapambano baina ya polisi na wananchi waliokadiriwa kuwa kati ya 800 na 1000.

  Kamugisha alisema katika tukio hilo, askari polisi mwenye namba E.6059 D/CPL Julius alikatwa panga usoni na kupata majeraha mdomoni na mgongoni na kuanguka wakati wakiwaondoa wananchi katika eneo la mgodi.

  Kamanda huyo aliwataja waliouawa kuwa ni Paulo Sarya (26) mkazi wa Nyangoto, Kata ya Matongo na Rodgers Mwita (18) mkazi wa Kimusi, Kata ya Nyamwaga, Wilaya ya Tarime, mkoani Mara.

  Alimtaja aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi mguu wa kulia ni Mseti Chacha (20), mkazi wa Nyamwaga wilayani hapa.

  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Serikali ya wilayani hapa, Nega Marco, alikiri kupokea maiti na majeruhi hao, lakini akakana kujua lolote kuhusiana na polisi aliyedaiwa kujeruhiwa na wananchi.

  Marco alisema, miili ya marehemu hao imehifadhiwa chumba cha maiti katika hospitali hiyo na kwamba tayari ilifanyiwa uchunguzi na inasubiri kuchukuliwa na ndugu.

  Hata hivyo, ndugu wa marehemu hao, hawakuwa tayari kutoa tamko lolote kuhusiana na mauaji ya ndugu zao wala kujua hatima ya tukio hilo.

  Inadaiwa kuwa, wananchi hao juzi walivamia mgodi huo eneo la Gokona na Rampad uliopo katika vijiji vya Kewanja na Nyangoto wakitaka kupora dhahabu.
   
 2. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2][/h] Jumamosi, Septemba 01, 2012 06:39 Na Timothy Itembe, Tarime

  JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime na Rorya, linadaiwa kuwaua kwa kuwapiga risasi watu wawili, kwa kile kinachodaiwa walivamia mgodi wa dhahabu wa Barrick, uliopo eneo la Nyamongo, kwa lengo la kuiba dhahabu.

  Tukio hilo, lilitokea juzi saa 12 jioni, katika eneo la Rompard karibu na shimo la Gokona, lililopo katika vijiji vya Kewanja na Nyangoto.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, Justus Kamugisha aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa, tukio hilo lilitokea, baada ya wananchi wanaokadiriwa kufikia 800, kuvamia eneo hilo na kutaka kuingia kwa nguvu mgodini kupora dhahabu.

  Alisema baada ya kujaribu kuingia kwa nguvu, polisi walijaribu kuwarudisha, lakini katika hali ya kustaajabisha, walianza kuwashambulia kwa mawe na silaha za jadi.

  Alisema mapambano hayo, yalisababisha askari polisi mwenye namba E.6059 D/CPL Julius, kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa na panga usoni, mgongoni na mdomoni.

  Alisema hali hiyo, ilisababisha Julius kuanguka chini na kupoteza fahamu kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Bomani kupatiwa matibabu.

  Alisema kutokana na hali hiyo, polisi walilazimika kurusha risasi za moto na ndipo wakawapiga watu wawili na kujeruhi wengine kadhaa.

  Kamanda Kamugisha, aliwataja waliouawa kuwa ni Paulo Sarya (26), mkazi wa Nyangoto na Rodcers Nyamboroga (18), mkazi wa Kijiji cha Kimusi.

  Alimtaja aliyejeruhiwa kuwa ni Mseti Chacha, mkazi wa Kijiji cha Nyamwaga, ambaye alijeruhiwa kwa kupigwa risasi kwenye goti la mguu wa kulia.

  Alisema katika mapambano hayo, magari matatu yenye namba za usajili PT 1417 aina ya Toyota Land Cruiser, iliharibiwa kwenye boneti na milango yote miwili kwa kupigwa mawe.

  Magari mengine ni Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili PT 1685, ambayo imeharibiwa kupigwa mawe kwenye kioo cha mbele na Toyota Land Cruiser, yenye namba LV 137, ilipasuliwa kioo cha mbele.

  "Jeshi la polisi mkoani hapa, linawataka wananchi kutii sheria bila kushurutishwa na kuacha tabia ya kuvamia mgodi mara kwa mara, kwa lengo la kuiba dhahabu, wakati wakitambua mwekezaji yule yupo pale kisheria,” alisema Kamanda Kamugisha.

  [h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
   
 3. mnyanyaswaji

  mnyanyaswaji JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 469
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huwezi kusema kundi lla watu 800 wameenda kuiba wote. Kuna kitu kimejificha hapo
   
 4. HASSAN SHEN

  HASSAN SHEN JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tumewazoea hao polisi wa Tarime
   
 5. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yani polisi wa Ccm sijui wanadhani watz ni wajinga sana au?Maana mpaka uone watu 800 wanakwenda kwa pamoja kwenye mgodi haiwezekani iwe kwa sababu za kuiba.Mara nyingi wale watu wanakwenda kutoa malalamiko yao kwa uongozi wa mgodi kutokana na kuweka sumu kwenye maji wanayonyweshea mifugo yao!Sasa kwa kuwa polisi wanatumwa na ccm kuwaua watu wanasingizia eti wameenda kuiba dhahabu!Mara nyingi watu wa mgodi huweka mbwa na walinzi pale getini ambapo huwalisha dawa na bangi ili waume watu na kwa makusudi huwaelekeza kwa wanafunzi wanaopita njia na kuwauma,kuwajeruhi na mara nyingi huwaua kabisa watoto!!!Wazazi hawana pakulalamikia maana mkuu wa wilaya anahongwa dhahabu na pombe,mbunge wa Ccm pale ndo kabisaaa hivyo hawana pakusemea wakienda kulalamika wanaambiwa wameenda kuiba dhahabu..........Ok ipo siku kitaeleweka tu hapo
   
 6. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Sitaki kuamini kwamba walikuwa ni wezi wa dhahabu.ngoja nitafakari nitarudi.
   
 7. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Sio risasi, ni kitu kizito kilichorushwa.
  Chezeya polisi wewe.
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Blood Gold aka Blood Diamond.
   
 9. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,167
  Likes Received: 527
  Trophy Points: 280
  Hao wameuwa na kitu kizito kirukacho(flying object)mambo ya vijana wa Said Mwema
   
 10. m

  mathias juma Member

  #10
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 31, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuongee yote lakini ukweli usiopingika wavamizi wa madini wakivamia hata wewe leo hii unyeshabikia sijui upande upi hautatamani kuzaliwa Tanzania. Unajua wengi tumezoea kupata habari kwenye mitandao kupamba kwa ushabiki watu tu. Siyo kwamba nashabikia kitendo Police walichokifanya la hasha! Damu ya mtu si ya kuchezea hata kidogo. Tujue fika kuwa asilimia kubwa ya Wafanyakazi migodini Tanzania ni Watanzania ingawaje wanalipwa mishahara kidogo kwa mahesabu ya kitanzania. Ombi na wito wangu kwa watanzania tufuate Taratibu na Sheria ili haki ipatikane, ndicho Mwalimu Nyerere alicho fanya na kupewa Nchi kirahisi bila kumwaga damu. Nakerwa sana na Kauli za baadhi ya viongozi wanaojigamba majukwaani baada Maisha ya Watanzania kupotea kizembe kisha kusema Marehemu alikuwa Shujaa kwa lipi? Tukumbuke wao wakiugua tu hata kipanda uso wanakimbizwa Nje ya Nchi, wewe Mtanzania wa kawaida ukishikwa na hoja tiba yako ni jua. Tuache ushabiki wa Vyama tujenge Familia zetu kisha Nchi ikuwe kiuchumi, fikiria mwenzako anapokushawishi kufanya fujo yeye anapata ruzuku na mishahara minono, wewe unashawishiwa kisha unarudi kula Ugali wa matama kwa mrenda. Tubadilike.
   
 11. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Nyamongo vita ile haitakuja kuisha...milele hadi watakapoondoka na kuwapisha wachimbaji wadogo wadogo wapate riziki zao....la sivyo hawatakuja kupoa ni vurugu tu kwenda mbele
   
Loading...