OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,015
- 114,360
Kichwa cha habari chahusika!!
Nimebahatika kuwa karibu na vijana wa CCM katika maisha ya shule na hata maisha baada ya shule! Wengi watakubaliana nami kwamba kwa awamu ya tatu na nne vijana wengi katika chama walikuwa wakiishi maisha ya ujanja ujanja na kujikomba kwa viongozi wa ngazi za juu
Viongozi wa ngazi za juu katika chama na serikali walikuwa wanamiliki vijikundi vya vijana katika harakati zao. Nitoe mfano kidogo kwa aliyekuwa Spika wa Bunge Mh.Sita yeye walikuwa na vijana kama Nape na Makonda. Mh.Lowasa yeye walikuwa na kina Bashe,katika awamu ya nne tuliona kijana alikuja kwa kasi Mwigulu Nchemba akawanunua kina Shonza na Mtela Mwampamba.
Maisha ya namna ile yaliwafanya vijana kuwa kama watumwa wa wanasiasa,huku wakisubiri teuzi mbalimbali katika chama na serikali.
Maisha hayo yaliwafanya vijana wengine wasio karibu na viongozi hao kufanya jitihada za kujipenyeza ili angalau maisha yaweze kwenda.Wengi wa vijana hawa ni wale wasiokuwa na sifa au elimu zenye mashaka mashaka.
Sasa kwa hali iliyomkuta Mh.Makonda,je itawafanya vijana hawa kukoma kujipenyeza kwa viongozi wa CCM kwa sababu hawatakuwa na nafasi tena?na hata kama wakilindwa jamii itawaanika maovu yao?
Je ni wakati sasa kwa vijana hao kuwekeza kwenye elimu na ujasiriamali badala ya kutumia mda mwingi kujipenyeza?

Vijana Njooni CCM,
View attachment 144394
Miongoni mwa sifa ambazo Chama Cha Mapinduzi kimejipambanua nazo katika Nyanja za kimataifa na kitaifa ni pamoja na utaratibu na mfumo bora wa uendeshwaji wake, kwamba ni Chama kilicho kamili katika muundo wake, misingi yake, kanuni na taratibu zake. Lakini pamoja na hayo CCM inayo historia iliyotukuka si tu ya kuikomboa TANZANIA kutoka katika mikono ya wakoloni lakini pia kusaidia mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la Sahara.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Vivaa Vijana Vivaaa !!!